This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, April 17, 2013

WEMA AIBU YAKE! ADAIWA KUPIGIA SIMU DIAMOND NA KUJITONGOZESHA UPYA

Aibu imemshuka, imemfika, imemwenea na imemtapakaa kila upande, Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu.

Hivi leo, endapo utamkuta Wema akiwa ametulia kisha ukamtishia ukitumia sauti ya juu kuyataja majina ya Diamond na Penny, kuna uwezekano mkubwa mrembo huyo akavunja mguu kwa kukimbia ‘spidi’ kali.
Ikamshuka Wema; Jumatatu iliyopita, usiku mkubwa, inadaiwa kuwa mrembo huyo akiwa katika hali ya utulivu kabisa, akaamua liwalo na liwe, hawezi kulikosa penzi la mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, wakati ni wake tangu na tangu.…
Aibu imemshuka, imemfika, imemwenea na imemtapakaa kila upande, Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu.
Hivi leo, endapo utamkuta Wema akiwa ametulia kisha ukamtishia ukitumia sauti ya juu kuyataja majina ya Diamond na Penny, kuna uwezekano mkubwa mrembo huyo akavunja mguu kwa kukimbia ‘spidi’ kali.
Ikamshuka Wema; Jumatatu iliyopita, usiku mkubwa, inadaiwa kuwa mrembo huyo akiwa katika hali ya utulivu kabisa, akaamua liwalo na liwe, hawezi kulikosa penzi la mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, wakati ni wake tangu na tangu.

Simu ikapigwa; inadaiwa kuwa Wema aliamini Diamond hapindui kwake, kwa hiyo alipiga simu kwa kujiamini.
Kilichozungumzwa; baada ya simu kupokelewa, inadaiwa kwamba Wema aliomba Diamond afungue moyo ili penzi lao lirudi kama zamani.
Diamond kwa misifa; Diamond kwa kiasi fulani alipikwa kimuziki na Dully Sykes ‘Mister Misifa’ na meneja wake wa zamani anaitwa Papa Misifa, kwa hiyo naye ni zao la Misifa.
Misifa kazini; Diamond aliposikia sauti ya Wema ikimbembeleza, ‘bichwa’ likamvimba, papo hapo, akaanza kumrekodi mrembo huyo.
Kilichosikika; sauti ya Diamond inasikika kwa juu, huku ile ya Wema ikitokelezea kwa mbali. Kimazungumzo ni kuwa M’bongo Fleva huyo, anaeleza kwamba hivi sasa yupo kwenye uhusiano ‘siriaz’ na mtangazaji, Penniel Mungilwa ‘Penny’, kwa hiyo hawezi kumwacha.
Eti Diamond hataki ‘drama’; mwanamuziki huyo, anasikika akimjibu Wema kwamba hawezi kurudiana naye kwa sababu itaonekana wanafanya drama (maigizo).
Diamond anafunguka: “Hapa hakuna drama wala nini, wala sikufanyii drama. I am in love with Penny (nipo kwenye penzi na Penny) na wewe unajua. Sipendi na sipendezewi kwa sababu mwisho wa siku yatakuja kutokea matatizo, sitaki.”
Penny naye; mrembo huyo anayemmiliki Diamond kwa sasa, aliingilia mazungumzo kati ya M’bongo Fleva huyo na Wema, kisha anasikika akimpa vidonge vyake, mrembo huyo: “Wema unaweza kutuacha tulale?”
Wema akasalimia; mrembo huyo ambaye juzijuzi alikata shilingi milioni 13 kumtolea faini msanii Kajala Masanja na kumwokoa na jela, hakutetereka kusikia sauti ya Penny kwenye simu, badala yake akamsalimia: “Uko poa?”
Penny akaliendeleza: “Yeah, niko poa mamy wangu. Hivi kwa nini hutaki kitu kitakachokufanya uwe na amani? Sisi hatutaki matatizo na wewe.”
WEMA ANASEMAJE?
Alipohojiwa na paparazi wetu kuhusiana na ishu hiyo, Wema alikataa katakata kwamba sauti inayosikika kwenye rekodi ya mazungumzo hayo siyo ya kwake, akaongeza kuwa alishaachana na Diamond siku nyingi zilizopita na kamwe hawezi kufanya kitu kama hicho.
“Hao kama wananichokonoa wapate ‘kick’ wafanye kimpango wao na siyo kutumia jina langu, mimi ni staa mkubwa Tanzania na kila mtu ananijua, waniache na maisha yangu kwa sababu sipendi kuongeaongea. Hata hili kama usingeniuliza, nisingesema chochote,” alisema mrembo huyo.

DIAMOND JE?
Diamond alipozungumza na ripota wetu, alisema kuwa sauti hiyo alimrekodi Wema kwa lengo la kumwonesha ni kiasi gani hivi sasa yupo kwenye uhusiano ‘siriaz’ na Penny.

AUNT:WABUNGE WANATAKA KUNIVUNJIA NDOA

Stori: IMELDA MTEMA
DIVA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa chake na kudai kwamba kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata penzi kwake, Amani linasimulia aliyoyasema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar, Aunt alisema waheshimiwa hao wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho anaamini kinaweza kuhatarisha ndoa yake.…
Stori: IMELDA MTEMA
DIVA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa chake na kudai kwamba kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata penzi kwake, Amani linasimulia aliyoyasema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar, Aunt alisema waheshimiwa hao wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho anaamini kinaweza kuhatarisha ndoa yake.
“Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua tayari nimeolewa lakini wananitongoza, mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza: “Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu wazito, hawezi kuwa na amani, bado naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.”
 Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunday Dimonte, Dubai na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume

"WAISLAMU PEKEE NDO WARUHUSIWE KUCHINJA NYAMA YA BIASHARA"....HII NI KAILI YA LEO YA RAIS MWINYI




Hii  ni  video  ikionesha  kauli  ya  Rais  Mwinyi  kuhusu  suala  la  kuchinja.Kauli  hii  amaitoa  leo  alipoongea  na  waandishi  wa 

MUNGU AILAZE PAHALI PEMA PEPONI


Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia leo mchana  huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. 

Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa nazi na hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102. 

Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....


Mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.

Bi Kidude pia aliwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni


Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen

"COME- ON.....FU*KY YOU"......HILI NI TUSI LA NGUONI TOKA KWA SERUKAMBA BUNGENI LEO....USHAHIDI UPO


Baada ya kuona kusitisha bunge kurushwa live kumepigwa vita, sasa wabunge wamekuja kwa staili ya matusi ili wananchi wasiwe na hamu kabisa ya kuliangalia bunge....

LEO kwa mara nyingine tena, Mh.Peter Serukamba amesikika waziwazi kabisa akitoa tusi mbele ya bunge na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake.

Bila woga wala aibu ya kuwa huenda anasikilizwa na wakwe zake ,Serukamba amesikika akisema "Come-on F.U.C.K Y.O.U."

 

TUKIO  LENYEWE  LILIKUWA  HIVI: 
 
Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliitaka serikali iwachukulie hatua kali wahusika wote wanaohusika na matukio ya utekwaji na uteswaji wa baadhi ya watu,kwa kutolea mifano ya Dr.Ulimboka na Kibanda.katika hotuba hiyo,kambi imeonesha kutoridhika na mwendendo wa utendaji wa idara ya usalama wa taifa.
Aidha hotuba hiyo kuna mahali imemtaja Rwakatare na mwenendo wake kabla ya kukamatwa.

Shida imeanza pale ambapo Mh.Serukamaba aliomba mwongozo wa spika,na kusema kuwa,kuna baadhi ya maswala yaliyomo ktk hotuba hiyo( hasa kuanzia ukurasa wa 1-4) yanazungumzia kesi ya Rwakatare ambayo tayari ipo mahakamani.
Na kwamba kuendelea kusomwa kwa hotuba hiyo ingekuwa ni kuingilia mwenendo wa kesi na kwamba hapo ingekuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Katika kutetea hoja zao,wabunge watatu wa kambi ya upinzani(H.Mdee,J.Mnyika na T.Lisu) walisimama na kujaribu kuonesha uhalali wa hoja zao.Wote watatu walijieleza kwa kadiri walivyoona inafaa.
Baada ya hapo ndipo aliposimama Mh.Serukamba na kusisitiza uhalali wa hoja yake.
Sasa kile kitendo cha yeye kusimama tena,inaonekana kulikuwa na minong'ono upande wa pili(lakini hiyo haikusikika) ndipo kwa kujisahau alipojikuta ametupia hewani TUSI HILO  la  "Come-on F.U.C.K Y.O.U."!

Kwa jinsi alivyotukana,aliunganisha haraka na maelezo yake kiasi kwamba Mh.J.Ndugai(aliyekuwa akiongoza) hakumkatisha, akamwacha aendelee.
Baada ya maelezo ya Mh.Serukamba,naibu spika(mwenyekiti) alitoa kauli yake rasmi.
Ndugai amesema kuwa mgogoro huu una mtazamo wa kikanuni,kwa hiyo ameagiza kamati ya kanuni ya bunge ikutane mara moja kujadili swala hilo kisha itoe ushauri kwa kiti cha spika jinsi gani ya kshughulikia mambo hayo yanayoonekana yana utata.
Aidha amesema hotuba hiyo ya kambi rasmi ya upinzani itaendelea kusomwa kipindi cha jioni.