This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, March 30, 2013

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO

..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..

MAHAKAMA YASEMA Uchaguzi Kenya ulikuwa huru na wa haki




Willy Mutunga rais wa mahakama ya juu zaidi Kenya
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.

Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.

Uamuzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao
Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.


Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Uhuru alishinda uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya uchaguzi kwa kura 8,100.


Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.


Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.


Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.


Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha uchaguzi mpya.Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.


Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.


Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa wapiga kura.


Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.


Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.


Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo....


Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.

MAUNO YA AUNTY LULU NUSURA YAUE


Na: Gladness Mallya

SI mnalikumbuka lile wowowo la Lulu Mathias Semagongo au Aunty Lulu? Si mnakumbuka jinsi  mwenyewe anavyolisifia kwamba analipenda sana na siku akiamka akakuta halipo atakwenda kwa mchungaji aombewe? Sasa safari hii nusura liue. Twende pamoja.…


Na: Gladness Mallya
SI mnalikumbuka lile wowowo la Lulu Mathias Semagongo au Aunty Lulu? Si mnakumbuka jinsi  mwenyewe anavyolisifia kwamba analipenda sana na siku akiamka akakuta halipo atakwenda kwa mchungaji aombewe? Sasa safari hii nusura liue. Twende pamoja.
Njemba ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amenusurika kifo kufuatia kuanguka ghafla na kupoteza fahamu kwa madai ya kuchanganywa na mauno ya Aunty Lulu, ni Risasi Jumamosi tu ndiyo lina habari hiyo.
Mkasa huo ulijiri kwenye sherehe ndogo ya watu wa karibu baada ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kufunga ndoa na Gardner Dibibi, Kinondoni, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Ilikuwa ni wakati wa ndugu, jamaa na marafiki wakipata msosi sanjari na vinywaji huku muziki ukipigwa nyumbani kwa familia ya bibi harusi, Kinondoni, ndipo Aunty Lulu alipoanza kukata mauno na kushangiliwa.
Wakati watu wakimpa dole Aunty Lulu, jamaa huyo alimtolea macho pima na kuanza kuchanganyikiwa na mauno hayo.
Polepole jamaa, mkono mmoja ukiwa umeshika sahani yenye msosi mwingine soda, aliganda kwa sekunde kadhaa kama vile haamini anachokiona.
Kufumba na kufumbua, njemba alikwenda chini ghafla na kupoteza fahamu.
Hali ya hewa ilichafuka kuanzia hapo, ikawa patashika nguo kuchanika.
Hata hivyo, wanaume majasiri waliokuwa eneo la tukio walimpepea jamaa huyo ambapo baadaye alizinduka.  
Jamaa huyo baada ya kurejewa na fahamu alisikika akisema: Ukweli wowowo la huyu dada (Aunty Lulu) limenichanganya, nusu linitoe roho jamani.
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kilichomtokea jamaa huyo ni mfadhaiko.

PINDA ATEMBELEA GHOROFA LILILOPOROMOKA DAR

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwasili leo katika jengo lililoporomoka jana
Kamanda Suleiman Kova akimpa maelezo Mh. Pinda na viongozi wengine
Mtunzi Maarufu Eric Shigongo (kushoto) akiwasili eneo la…
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwasili leo katika jengo lililoporomoka jana
Kamanda Suleiman Kova akimpa maelezo Mh. Pinda na viongozi wengine
Mtunzi Maarufu Eric Shigongo (kushoto) akiwasili eneo la tukio
Shigongo akijionea maafa yaliyotokea baada ya kudondoka kwa jengo hilo
Shigongo akisaidiana na waokoaji wengine kutoa kifusi
Wananchi wa jiji la Dar es Salaam wakiangalia jengo la gorofa 16 lililodondoka, jana asubuhi.
Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushuhudia maafa hayo.
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari.