This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, July 11, 2013

UGANDA CRANES YAWASILI KWA MPAMBANO WA JUMAMOSI

Mashabiki wa Uganda waliofika uwanjani kuipokea timu yao.

Wachezaji wa The Cranes walipowasili.
Kocha Sledojovik Micho na msaidizi wake, Sam Timbe, wakiwai na kikosi hicho.…
Mashabiki wa Uganda waliofika uwanjani kuipokea timu yao.
Wachezaji wa The Cranes walipowasili.
Kocha Sledojovik Micho na msaidizi wake, Sam Timbe, wakiwai na kikosi hicho.
Wakiingia kwenye basi waliloandaliwa.
Mwenyekiti wa Waganda wanaoishi Tanzania, Hellen Tusiime,  alikuwa mkuu wa mapokezi hayo.
Wakiwa tayari kwa safari kuingia jijini.
TIMU ya taifa ya Uganda (The Cranes)  mchana huu imewasili uwanja wa ndege Dar es Salaam kwa ajili ya kujiwinda kwa mchezo wao dhidi ya timu ya taifa  (Taifa Stars) unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii.

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL  

SHUGHULI MBALIMBALI ZA RAIS KIKWETE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO JULY 11, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es Salaam.…
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana  na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Hamisi Amir Msumi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Hilda A. Gondwe kuwa Mjumbewa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Celina Augustine M. Wambura kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakipiga picha ya pamoja na Mwenyekiti mpya wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Serikali Mhe Hamisi Amiri Msumi pamoja na wajumbe wapya Mhe Hilda A. Gondwe na Mhe Celine Augustine M. Wambura na viongozi wa Tume hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA IKULU)

UGANDA CRANES YAWASILI KUIKABILI STARS


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes'.
Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) imewasili Dar es Salaam leo tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati yake na Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

The Cranes inayofundishwa na Mserbia Sredojvic Micho imetua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda, na imefikia hoteli ya Sapphire.

Timu hiyo leo (Julai 11 mwaka huu) itafanya mazoezi saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Karume, wakati kesho saa 9 alasiri itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, kabla ya kuipisha Taifa Stars itakayoanza…
Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) imewasili Dar es Salaam leo tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati yake na Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
The Cranes inayofundishwa na Mserbia Sredojvic Micho imetua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda, na imefikia hoteli ya Sapphire.
Timu hiyo leo (Julai 11 mwaka huu) itafanya mazoezi saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Karume, wakati kesho saa 9 alasiri itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, kabla ya kuipisha Taifa Stars itakayoanza mazoezi saa 10 kamili jioni.
Taifa Stars inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen, na kudhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, leo kwa mujibu wa program yake haitakuwa na mazoezi.
Wachezaji wanaounda The Cranes ni makipa Ismail Watenga, Kimera Ali na Muwonge Hamza. Mabeki ni Guma Dennis, Kasaaga Richard, Kawooya Fahad, Kisalita Ayub, Magombe Hakim, Malinga Richard, Mukisa Yusuf, Savio Kabugo na Wadada Nicholas.
Viungo ni Ali Feni, Birungi Michael, Frank Kalanda, Hassan Wasswa, Kyeyune Said, Majwega Brian, Mpande Joseph, Muganga Ronald, Ntege Ivan, Owen Kasule, wakati washambuliaji ni Edema Patrick, Herman Wasswa na Tonny Odur.

MAMA MZAZI WA PROFESA JAY AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI DUNIA....


Picha kushoto ni Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake...
 
Mama  mzazi  wa  Msanii Profesa Jay  amefariki dunia  usiku  wa  kuamkia  leo  baada  ya  kugongwa  na  gari  maeneo  ya  mbezi  juu  jijini  Dar  alikokuwa  anaishi  na  mwanae.


Habari  zinadai  kwamba, marehemu Bi. Rosemary Manjara  Haule  aligongwa na gari akiwa  anavuka barabara kuelekea  dukani  mida ya saa mbili  na  kwamba  baada  ya  kugongwa  wasamaria  wema walimkimbiza  hospitali  ya  Tumbi  kwa  kutumia  bajaji ambako  mauti  ilimkuta  huko

Profesa  Jay  amethibitisha   hilo  na  kudai  kwamba  ilikuwa  ni  vigumu  sana  kuamini.Mama  yake  alimpigia  simu  na  kumwambia  kuwa  kagongwa  na  gari  na  kwamba  yuko  polisi.Ghafla  simu  yake  ikawa  haipatikani...


Profesa  anasema  kwamba  wakati  anapigiwa  simu  alikuwa  katika  mgahawa  wa  nyumbani  lounge,Namanga Dar  ambako  alikuwa  katika  kikao  na  Lady  jaydee  na  mumewe.

"MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NAGARI....NJONI KOPOLISINAANDIKISHA....   MWANANGU NAKUFA....  ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU. 

Mungu  ailaze  roho  ya  marehemu  mahali  pema  peponi.

RAIS KIKWETE AWASHANGAA CHADEMA KUTAKA KAMBI YA KUJILINDA...DR. SLAA NAYE AWATAKA POLISI WAYAVUNJE MAKAMBI YA CCM


Rais wa Tanzania amewashangaa na kuwalaani CHADEMA kwa kutangaza kufundisha vijana namna ya kujilinda na kusema kuwa ni watu wa ajabu kama wamefikia huko.

Mh. Rais kayasema hayo katika kuhitimisha kongamano la amani  huku bwana Cheyo  nae akisema  kuwa  hata kama  ni kutaka kuwa rais wa nchi CHADEMA wamefika kubaya....


Wakati  mh. Rais  akiwashangaa CHADEMA,Katibu Mkuu wa chama  hiyo,  Dr Wilbroad Slaa amelitaka jeshi la polisi kuvunja mara moja makambi yote ya CCM nchini yanayotoa mafunzo kwa vijana wanaoitwa Green Guards.
 

Kauli  hiyo  ya Dr. Slaa  imekuja  baada  ya  polisi  kuwazuia  CHADEMA kuanzisha  kambi  yoyote  ya  kujihami  na  kwamba  hatua  kali  za kisheria  zitachukuliwa  dhidi  yao  endao  watakaidi  agizo  hilo

Dk. Slaa, amesema kauli ya Jeshi la Polisi inadhihirisha namna wahusika wasivyofahamu sheria kwa kile alichoeleza kuwa wao hawaundi majeshi bali vikundi vya ukakamavu.

Alisema ni heri msemaji wa jeshi hilo angekaa kimya kuliko kulifedhehesha Jeshi la Polisi kwa tamko lisilokuwa na ushawishi wa kisheria.


“Nawashauri hawa waanze na Tendwa…ila kwanini wameanza leo sisi tulishayalalamikia makundi ya CCM kwa barua na hata walipomaliza mafunzo yao kule Igunga tukapiga na picha wao hawakuinua mdomo kuliongelea,” alisema Dk. Slaa.

Alisema katika miaka minne iliyopita CHADEMA ilikuwa ikionyesha kwa ushahidi namna vijana wa CCM wanavyopewa mafunzo ya kijeshi, ikwamo silaha kutoka nje ya nchi huku wahusika wakiendelea kukaa kimya.

Aliongeza kuwa hali hiyo ya kuamka baada ya kauli ya CHADEMA inatia nguvu shaka yao, aliyodai kuwa makundi ya CCM yanafanya mafunzo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Dk. Slaa alitolea mfano kundi la vijana wa CCM walioweka kambi katika shule ya wazazi katika Kata ya Ivumwe, Mbeya mjini na kisha kuwateka katibu wa CHADEMA Mbeya mjini na baadhi ya wanachama wake.

Alisema katika tukio la Ivumwe wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani wa hivi karibuni, CHADEMA walitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Mbeya ambaye aliwajibu kuwa wapeleke ushahidi kama vijana hao ni wahalifu.

Alibainisha kuwa CCM imekuwa na kawaida ya kukusanya vijana kutoka maeneo tofauti na kisha kuwapa mafunzo ya kijeshi na silaha kwa ajili ya kuwadhuru wapinzani na kutolea mfano Kambi ya Ulemo aliyosema ilikuwa na vijana waliopewa mafunzo ya kijeshi.

“Tunawasubiri tuone hatima yao ni nini, sisi tunajua Jeshi la Polisi limeshajitoa  kulinda viongozi wa CHADEMA sasa kwanini tusijilinde wenyewe,” alisema Dk. Slaa.

Source: BBC, Tanzania Daima,Jamii Forum

PICHA YA MREMBO AKIWA KATIKA POZI LA NUSU UCHI YADAKWA

 Katika  hali  ya  kushangaza, mrembo huyu   anayejiita  Emmy  alijikuta   akitupia  picha  yake  ya  uchi ( kifua wazi ) katika  mtandao  wa Badoo....

Haijafahamika  mara  moja  kama  picha  hiyo  iliwekwa  makusudi  au  kimakosa  maana  iliondolewa  ndani  ya  dakika  chache  tangu iwekwe......
 Profile  ya mrembo huyo  katika mtandao huo  inaonesha  kwamba  yupo Arusha.

MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI

Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
 
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
  
Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela  
 
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
Na  Mbeya yetu