This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, July 14, 2013

WANAJESHI 7 WA TANZANIA WAMEUAWA HUKO DARFUL- SUDAN



Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa.


Taarifa zilizotufikia jana  zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.



Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.



Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.



Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo.



Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.



Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji.



Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.


Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.


Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur.



Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC.



Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanzania imepeleka wanajeshi 850.

“Tanzania imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na ushauri kwa nchi nyingi,” alinukuliwa Kanali Mgawe, na kueleza kuwa majeshi ya Tanzania yamekuweko katika vikosi vya kulinda amani huko Lebanon, Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya Comoro na Liberia. Liberia waliuawa wanajeshi wa Tanzania 11.

“Tanzania daima haiendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa,” alisema.

STARS KIMENUKA, YALALA 1-0 TAIFA


 Stars wakiwa vichwa chini baada ya matokeo ya leo.
MATUMAINI ya timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kushiriki fainali za CHAN nchini Afrika Kusini imefifia baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes'. Taifa Stars imelala katika mechi ya kwanza iliyopigwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo, Stars inasubiri mechi ya pili…



WALIOMRUHUSU MASOGANGE APITE NA 'UNGA' AIRPORT NI HAWA!


HAKUNA sababu ya kumkamata ‘mchawi’  kwenye skendo ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kukamatwa na madawa ya  kulevya nchini Afrika Kusini wakati ukweli upo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 Watu mbalimbali ambao wamesoma sakata hili kwenye vyombo vya habari, walitoa maoni yao wakisema kuwa watu wanaotakiwa kuwajibishwa ni waliokuwa uwanjani hapo siku Masogange aliposafiri na kuruhusu mizigo ya mrembo huyo na mdogo wake, Melisa Edward ipite bila ukaguzi makini.…
Stori: Mwandishi Wetu
HAKUNA sababu ya kumkamata ‘mchawi’  kwenye skendo ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kukamatwa na madawa ya  kulevya nchini Afrika Kusini wakati ukweli upo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Watu mbalimbali ambao wamesoma sakata hili kwenye vyombo vya habari, walitoa maoni yao wakisema kuwa watu wanaotakiwa kuwajibishwa ni waliokuwa uwanjani hapo siku Masogange aliposafiri na kuruhusu mizigo ya mrembo huyo na mdogo wake, Melisa Edward ipite bila ukaguzi makini.
“Kuna uwezekano kabisa wa kuwajua watu hao,” alisema msomaji wetu, Mbande Kinaka, mkazi wa Kariakoo, Dar.
Risasi Jumamosi lilimtafuta Mkuu Kitengo cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamanda Godfrey Nzowa, alipopatikana na kuulizwa namna ya kuwabaini waliomruhusu Masogange akapenya na mzigo airport, alisema lazima watawapata.

Taarifa tulizozipata zinasema Agnes na mdogo wake Melisa Edward  waliondoka nchini Julai 5, mwaka huu kwenda Afrika Kusini.


MWANAFUNZI WA IFM AFARIKI DUNIA AKIOGELEA KATIKA UFUKWE WA BAHARI YA HINDI



Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi wa Kompyuta wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Wendy Habakuki Lwendo amefariki dunia katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni akiogelea na wenzake watatu jana jioni.

Taarifa kutoka kwa  kaka wa Marehemu, Sammy Lwendo amesema mdogo wao alipatwa na masaibu hayo akiwa na rafiki zake hao watatu wakiogelea baharini na wakati wanaogelea walikuwa katika eneo la kina kifupi cha maji yaliyokupwa na mara maji hayo yaka jaa na walipokuwa wakijaribu kutoka ndipo Wendy akazidiwa na maji.

Lwendo amesema kuwa wenzake walifanikiwa kumtoa majini lakini hali yake tayari ilikuwa mbaya na kwakuwa hawakuwa na ujuzi wa kutosha wa kutoa huduma ya kwanza kwa mtu 

aliyezama majini walihangaika kwa zaidi ya dakika 40 kumsaidia ndipo wakapata msaada wa Polisi  kumkimbiza kituo cha afya Kibaoni huko Kigamboni lakini jitihada za kuokoa maisha yake ziligonga mwamba.



Aidha alisema kuwa mwili wa Marehemu ulihamishiwa katika Hospitali ya Wilaya Vijibweni na sasa ndugu wamefika na kuhamishia mwili huo Hospitali ya jeshi Lugalo.

Msiba kwa sasa upo Kinondoni nyuma ya Vijana, huku wakisubiriwa wazazi wa marehemu pamoja na ndugu wengine ili kujua taratibu kamili za maziko.

Wazazi wa Wendy, Mchungaji Habakuki Lwendo ni mwalimu wa Chuo cha Uchungaji Makumira mkoani Arusha.

---
Taarifa via Mroki Mroki



MKUU WA MKOA MOROGORO AFUNIKA KWA KUCHEZA KWAITO UKUMBINI

Stori:Dustan Shekidele,Morogoro

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera juzikati alionyesha wananchi wake umahiri mkubwa wa kuucheza muziki mtindo wa Kwaito huku akiwafunika vibaya vigogo wa Benki ya NMB Mkoa wa Morogoro waliokuwa wakicheza naye.
Hapa Akikonga kwaito na wazee wenzake
Bendera alionyesha umahiri huo ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Morogoro kwenye sherehe kabambe ya kumuaga aliyekuwa Meneja wa Benki ya  NMB Tawi la Wami aliyefahamika kwa jina moja tu la Bushiri aliyehamishiwa Wilaya…
Stori:Dustan Shekidele,Morogoro
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera juzikati alionyesha wananchi wake umahiri mkubwa wa kuucheza muziki mtindo wa Kwaito huku akiwafunika vibaya vigogo wa Benki ya NMB Mkoa wa Morogoro waliokuwa wakicheza naye.
Hapa Akikonga kwaito na wazee wenzake
Bendera alionyesha umahiri huo ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Morogoro kwenye sherehe kabambe ya kumuaga aliyekuwa Meneja wa Benki ya  NMB Tawi la Wami aliyefahamika kwa jina moja tu la Bushiri aliyehamishiwa Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro ambapo mkuu wa mkoa alisakata Kwaito kwa mbwembwe nyingi.
“Hakika Bendera ni mwanamichezo, kumbe siyo kwenye soka tu bali hata kwenye dansi yumo, umeona pale ni kama wanashindanishwa lakini kama ni ushindi basi angepewa yeye,” alisikika akisema mwalikwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina na John Sheki.
Licha ya kuwa mwanasiasa na kuonesha umahiri wa kucheza dansi, Bendera aliwahi kuwa Kocha wa Timu ya Taifa, Taifa Stars mwaka 1983 hadi 1986 na akawa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira wa Miguu (FAT) mwaka1978 hadi 1979.
Sherehe hiyo iliyofana ilihudhuriwa na wafanyakazi wa matawi yote ya NMB Mkoa wa Morogoro na baadhi ya wateja wa benki hiyo ambao walikuwa wageni waalikwa na ilianza saa 2 usiku ikafika tamati saa 6 usiku huku gumzo likiwa ni usakataji wa Kwaito wa Bendera.

RAY C AFUTUKA

Stori: Mwandishi  Wetu
Mwanamuziki staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka.
Hivi karibuni, Ray C ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na mashabiki wake.
Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na alivyozoeleka.

UNENE UNATOKANA NA DOZI?
Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’.
Hata hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya unga.

AFUTUKA
Katika picha hizo, Ray C anaonekana kufutuka usoni, kifuani na mapajani ambapo awali kabla ya matatizo hakuwa hivyo.
Wengi walimshukuru Mungu kumuona tena Ray C akiwa mzima pamoja na ukimya wake katika muziki.
Ray C amekuwa akitundika picha hizo kwa ajili ya mashabiki na marafiki hasa kupitia Instagram akiambatanisha na maelezo huku nyingine zikizungumza zenyewe.

HATAKI KUTAJA ANAPOISHI
Maelezo ya picha hizo yamekuwa yakielezea maisha ya Ray C kwa sasa akiwa kwenye mjengo wa maana bila kutaja ni sehemu gani.
Kwa mujibu wa mashabiki wa Ray C, mwanadada huyo kwa sasa anakula bata tu huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’ kwa kuwa ndiye aliyemsaidia kimatibabu.

DAKTARI ANASEMAJE?
Daktari mmoja maarufu jijini Dar aliyehojiwa na gazeti hili, alibainisha kuwa kinachosemwa na mashabiki wa Ray C kwamba kinachomnenepesha ni dozi ya kuacha madawa ya kulevya, kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli.
Aliongeza kuwa kunenepa kunachangiwa na vitu vingi kama kupata maisha mazuri yasiyohusisha msongo wa mawazo au mihangaiko ya hapa na pale hivyo anachofanya ni kula, kulala na kustarehe tu.

SHEIKH MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AMWAGIWA TINDIKALI NA KUUMIZWA VIBAYA



Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.

Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.

Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.

Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.

Alisema hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa amesimama jirani na mlango.

Alieleza kuwa wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu
huyo akiinua mkono na kumwagia maji yaliyompatia maumivu makali usoni na kifuani.


‘’Wakati natoka msalani nikipitia uwani kwangu niliona kama mtu ameinama pembeni yangu wakati najaribu kumsogelea ili nijue ni nani nilihamaki mtu huyo akinimwagia maji yaliyonisababisha maumivu makali sana yenye asili ya moto na ngozi kuanza kubabuka,’’ alisema shekhe huyo.

Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alianza kupiga kelele kuomba msaada ambapo majirani walijitokeza na kumpa msaada wa kumpeleka hospitali, kwa vile wakati huo macho yake yalikuwa hayaoni na wakati wote alikuwa  akilia.

Pamoja na kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni, kifuani na  mgongoni, pia ana majeraha  kwenye mikono na machoni na hali yake bado ni mbaya japo madaktari wanaendelea kumpatia matibabu.

Kaimu Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud akizungumzia tukio hilo alieleza kushitushwa nalo akisema limefanana na lile la Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka jana alilipuliwa kwa bomu nyumbani kwake akiwa amelala.

Alisema kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia huku wahusika wakishindwa kutiwa mbaroni na kudai kuwa matukio hayo yanahusiana na masuala ya kigaidi. Aliongeza kuwa pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini wamekuwa hawapati matunda ya kukamatwa kwa watuhumiwa ingawa alisema wanajulikana.

Kwa upande wake,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zitatolewa pindi washukiwa watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado unaendelea na kwamba hakuna  mtu anayeshikiliwa hadi sasa.