This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, May 29, 2013

PICHA ZA BAADHI YA WASANII WALIOHUDHULIA KIKAO CHA MSIBA WA MSANII "ALBERT MANGWEA" PALE LEADERS CLUB.

Kala Jeremiah amemwelezea Ngwea kama msanii wa pekee alikuwa 100% mkali wa Free Style na alimpenda kwa nyimbo kali kama Ghetto langu iliyom inspire kuingia kwenye Game.

Mwana FA amesema ni vitu vingi vya kukumbuka kutoka kwa Ngwea lakini kikubwa ni uwezo wake wa kuandika na mashairi yake kutojirudia hadi akatoa mfano kuwa mara nyingi alikuwa akimwambia Ngwea kwamba ana Range anatembea nalo kichwani lakini Ngwea alimjibu kuwa si Range moja tu bali mawili anamiliki kichwani kwake so tunaweza kuona jinsi gani alikuwa mtu muhimu kwenye game.
P Funk majani nae amezungumza lakini alishindwa kutokana na uchungu aliokuwa nao juu ya msiba kwani bado haamni kama Ngwea hayupo tena.


Noorah, Mez B na Proffesa Jay

KIFO CHA NGWEA: LADY JAYDEE NAYE ASITISHA SHOW YAKE

Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, mwanadada Judith Wambura Maarufu kama Lady Jaydee ametangaza kuahirisha shughuli ya maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge kupisha msiba wa kifo cha msanii Albert Robert Mangweha aliyeripotiwa kufariki nchini Afrika Kusini jana.

Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
  
Jaydee ameeeleza uamuzi wake wa kutitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.
 

Tangu amekaribishwa studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonzi sana kiasi cha kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na kukabwa na kilio.

"SITAKI KUSIKIA NYIMBO ZA NGWEA ZIKIPIGWA CLOUDS FM..WAO NDO WALIOMFANYA AANZE KUVUTA BANGI ILI KUONDOA MAWAZO"...P FUNK




Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.

HIVI NDIVYO MAMA DUDE ALIVYOZIKWA


Jeneza lililobeba mwili wa marehemu.
Mwili ukipelekwa makaburini.…
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu.
Mwili ukipelekwa makaburini.
  Dude (aliyesimama) akiwa katikati ya waombolezaji.
Umati wa wanaume waliohudhuria kwenye msiba huo ukiwa nyumbani kwa mama Dude, Ilala, Dar.
  Wasanii wa filamu, Mzee Chillo na Cloud (waliokaa chini wamevaa baragashia) wakijadiliana jambo.
  Kala Jeremiah naye alikuwepo (aliyevaa kofia nyekundu iliyochanganyika na nyeusi).
Wasanii wa filamu kwa upande wa wanaume.
    Wasanii wa filamu kwa upande wa wanawake.
MAMA wa msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, marehemu Mwadodo Ramadhan ‘Bi. Dodo’ leo amezikwa katika makaburi ya Malapa yaliyopo Buguruni-Malapa jijini Dar ambapo mazishi hayo yamehudhuriwa na watu kibao wakiwemo wasanii wa filamu, vichekesho na wa Bongo Fleva. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen!

HEE NESII!


Na Waandishi Wetu
MUUGUZI wa kike, Violet Shoo, mkazi wa jijini Dar ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni, Ilala baada ya kunaswa katika jaribio la kutaka kumchoropoa ujauzito msichana mmoja aliyepandikizwa kama mwanafunzi kwa mtego makini ulioratibiwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’.
Violet Shoo (kushoto) akidhibitiwa na polisi baada kunaswa katika jaribio la kutaka kumchoropoa ujauzito 'Denti'.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita, saa 11 jioni kwenye zahanati iliyopo Tabata Matumbi, jijini Dar es Salaam.
ILIKUWAJE?
Muuguzi huyo alikutwa ndani ya zahanati hiyo akiwa na zana mbalimbali zinazodaiwa ni za kutolea mimba huku msichana huyo akiwa juu ya kitanda, tayari kwa kufanyiwa zoezi hilo haramu.
...Vitendea kazi anavyotumia Violet Shoo kuchoropoa mimba.
Awali, Ijumaa ya Mei 23, mwaka huu baadhi ya wakazi wa eneo hilo walilitumia ujumbe gazeti hili wakimlalamikia muuguzi huyo kwamba amekubuhu katika matukio ya utoaji mimba hivyo wakaomba ikiwezekana OFM imuandalie mtego wa kumnasa ili kukomesha kitendo hicho.
“…huyu nesi amekuwa akiwatoa watoto wetu mimba, kwa siku anaweza kutoa hadi nne, sisi wazazi tumechoshwa, tunaomba mje. Anaitwa Violet…” ilisomeka sehemu ya meseji hiyo huku ikielekeza zahanati anapopatikana.
...'Denti' akiwa tayari kuchoropolewa mimba.
OFM YAJIPANGA, YAENDA KUCHUNGUZA
Baada ya malalamiko hayo, kikosi cha upelelezi cha OFM chenye wasichana wawili kilikwenda kwenye zahanati hiyo na kukutana uso kwa uso na muuguzi huyo ambapo msichana mmoja aliomba kutolewa mimba na nesi huyo ambapo aliambiwa ni shilingi 50,000.
Zahanati yenyewe hii hapa.
Kikosi kiliondoka kwa kumwambia muuguzi huyo kwamba wanafuata fedha mahali na wangerejea jioni wakiwa na ‘keshi’ mkononi.
Takataka kutoka katika zahanati hiyo.
POLISI WASHIRIKISHWA
Timu ya waandishi wa habari wa gazeti hili pamoja na Jeshi la Polisi waliweka mtego baada ya wakazi wa maeneo iliyopo zahanati hiyo kulalamika juu ya kukithiri vitendo vya utoaji mimba vinavyofanywa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.
Wakazi wa maeneo hayo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, walidai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupiga simu katika chumba cha habari kuwa idadi kubwa ya wanawake wanatolewa mimba kwa siku katika zahanati hiyo bubu ambayo haina jina wala hadhi ya kutoa huduma.
Mtuhumiwa akizidi kutulizwa na polisi.
Baada ya hapo, waandishi hao wa kike walirejea ofisini na kutoa taarifa kwa mabosi wao ambapo timu kamili ilipangwa.
Mkuu wa timu hiyo alianzia Kituo cha Polisi Buguruni ambapo alitoa taarifa kuhusu malalamiko ya wakazi wa eneo hilo na jinsi muuguzi huyo alivyofikia hatua ya kutaka alipwe elfu hamsini ili kukamilisha zoezi.
...akiwa chini ya ulinzi.
Afande mkuu akatoa maagizo kwa watu wa chini yake watatu, akiwemo askari wa kike mmoja kwa ajili ya kwenda kumnasa nesi huyo.
NESI AENDA KUSUKA KWANZA
Msichana aliyepandikizwa kutolewa mimba akiwa na mwenzake walitangulia kufika kwenye zahanati hiyo lakini hawakumkuta muuguzi huyo.
...mikononi mwa polisi.
Mfanyakazi mmoja wa zahanati hiyo alimweleza ‘mtolewa mimba’ kwamba nesi huyo alikwenda kusuka na tayari ameshawasiliana naye hivyo wasubiri.
SAA 10:30 alasiri, NESI ATOKEA
Saa kumi na nusu, muuguzi huyo aliwasili kwa ajili ya kazi hiyo huku mawasiliano yakifanyika kati ya mtolewa mimba na waandishi waliokuwa jirani na eneo la tukio.
Ndani ya dakika kumi, waandishi na polisi waliitwa eneo la tukio wakijulishwa kwamba ‘mjamzito’ huyo ameshavua nguo tayari kwa kazi ya kuchoropolewa mimba.
...tayari kwa safari ya kuelekea polisi.
USO KWA USO
Kikosi kazi kilivamia zahanati hiyo ambapo walikuta zoezi linaendelea. Polisi wenye ujuzi wa kazi za kunasa matukio walimtia mbaroni muuguzi huyo akiwa na zana za shughuli huku wakimwambia kosa lake.
Wakati huo, mjamzito alikuwa yupo kitandani katika maandalizi ya kutolewa mimba.
MAJIRANI MENO NJE
Wananchi waliokuwepo eneo la tukio wakati mtanange ukiendelea, walionekana kufurahishwa na kitendo cha kukamatwa kwa muuguzi huyo huku wakidai walikuwa wamechoka naye kutokana na vitendo vyake vya kutoa mimba hadi kwa wanafunzi.
“Tumekuwa tukijitahidi kutoa taarifa katika vyombo vya dola ikiwemo ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu lakini hakuna hatua zozote zilizokuwa zikichukuliwa, ndiyo maana tukaamua kuwasiliana na nyie waandishi wa habari ili mtusaidie,’’ alisema mkazi mmoja bila kutaja jina lake.
...safari ya kuelekea polisi ikaanza.
SWALI KWA MUUGUZI
Muuguzi huyo alipoulizwa kwa nini amekuwa akijihusisha na vitendo hivyo, alikaa kimya.
MJUMBE ASHUHUDIA
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina Namba 26, Tawi la Mandela, Rogasian Chadima alikuwepo katika eneo la tukio baada ya kufuatwa na polisi, naye aliahidi kufuatilia suala hilo akisema kwanza hakujua kama kuna zahanati katika eneo lake.
SAFARI YA KWENDA POLISI
Safari ya kwenda polisi kwa mahojiano ilianza hapo huku muuguzi huyo akiwa na ‘ushahidi’ wake mkononi. Muda mwingi alionekana asiyeamini macho yake kwa kile kilichomtokea.
Imeandikwa na Makongoro Oging’, Mwaija Salum, Musa Mateja na Joan Lema.

Tuesday, May 28, 2013

"SINA SHAKA NA UMAARUFU WANGU"....LOWASSA


MBUNGE wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amesema hana shaka na umaarufu wake Monduli wala Tanzania kwa ujumla.
 
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akifungua kampeni za udiwani wa Kata ya Makuyuni huku akikishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kupeleka mgombea wake katika Kata hiyo.


“Eti hawa wanathubutu kujinadi na kujigamba kushinda udiwani Monduli ya Lowassa wakisema watapata kura kwa asilimia 90 jamani haya ni kweli?,” alihoji Lowassa na kuongeza:

“Ndugu zangu sina shaka na umaarufu wangu Monduli wala Tanzania.”

Katika mkutano huo, aliwaambia wananchi kwamba anahitaji kuona wakikiadhibu CHADEMA kwa kukipa pigo ambalo hawajawahi kulipata mahali popote nchini.

“Ndugu zangu atakayewapa kura hawa CHADEMA wana wa Makuyuni atakuwa amenichoma kisu mimi, naomba msiwape kura hata moja, naomba muwafundishe adabu,” alisema Lowassa.

Akikishambulia chama hicho kwa kutumia helikopta katika Kata hiyo, alisema siku zote vita vya kiafrika vinapiganwa kwa kutumia askari wa miguu na si helikopita.

Alisema CCM inatumia askari wa miguu kuhakikisha inashinda vita vyake, hivyo haitatishika na helikopita hiyo.

Alikirushia kombora chama hicho kwa kukitaka kisimame hadharani na kujipapanua kama hakihusiki na vurugu zinazoendelea nchini.

Alisema kama kweli hakihusiki na vurugu zilizopo nchini basi viongozi hao wanapaswa kujihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki.

“Nawaomba hawa CHADEMA wajihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki na vurugu hizi, je wanaifanyia nchi yetu mema au mabaya,” alihoji Lowassa.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI ADDIS ABABA, ETHIOPIA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani Mh…
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani Mh Liberata Mulamula walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibe walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibe na ujumbe wake walipokutana pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibe pamoja na Mratibu wa Masuala ya Ukimwi wa Marekani Balozi Eric Goosby walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Waziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulishaWaziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller kwa Mhe Gideon Moi, Seneta wa Kaunti ya Baringo nchini kenya na ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha KANU cha nchi hiyo walipokutana pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Mohamed Morsi walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika Mkutano wa kawaida wa 21 wa Umoja wa Afrika katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa taaisi ya kimataifa inayoshughulikia mapambano dhidi ya Ukimwei, Kifua Kikuu na Malaria ya The Global Fund Dkt Mark Dybil na afisa wa taasisi hiyo Bi Shu-shu Tekle-Haimanot walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) professor Ntumba Luaba na ujumbe wake walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
(PICHA ZOTE NA IKULU)

AIRTEL YAZINDUA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS 2013‏

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa progamu ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo, wengine ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo (katikati) na Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu. Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo akikazia jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye halfa ya uzinduzi wa programu ya Airtel 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo kushoto ni…
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa progamu ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo, wengine ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo (katikati) na Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu. Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo akikazia jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye halfa ya uzinduzi wa programu ya Airtel 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni.
Baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012 wakisalimiana na Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa progamu ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo.
Wakizindua programu ya Airtel Rising Stars 2013 Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni na mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Dar es Saalam Almasi Kasongo wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars 2013.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012.
---
AIRTEL YAZINDUA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS 2013‏
Dar es Salaam, Jumanne 28 Mei 2013… Airtel Tanzania leo imezindua michuano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Airtel imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kudhamini mashindano hayo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) pamoja na serikali kukuza vipaji vya soka nchini Tanzania.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo tangu kampuni ya airtel ianze kudhamini mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo huanzia ngazi ya mkoa hadi Taifa. Fainali za Airtel Rising Stars Taifa hufatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa kwa wachezaji nyota chini ya ukufunzi wa makocha mahili wa vijana kutoka klabu ya Manchester United.

“Nafurahi kwamba tumepiga hatua na leo tunazindua msimu wa tatu wa Airtel Rising Stars ambao bila shaka utakuwa wa ushindani na wa kusisimua”, alisema Beatrice Singano, Mkuu wa Idara ya mawasiliano ya Airtel Tanzania. Uzindinduzi huo ulifanyika katika ofisi za TFF.

Singano alisema: “Airtel imevutiwa na mwitikio wa vijana wengi waliojitokeza kujiandisha na kushiriki katika mashindano ya Airtel Rising Stars katika miaka iliyopita. Ni matumaini yetu kwamba vijana wengi zaidi watajitokeza kushiriki mwaka huu”.

Singano alisema mpango huu kabambe unawalenga wasichana na wavulana nchi nzima ili kuwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao kwa mawakala wa soka, makocha na mamlaka nyingine zinazohusika na programu za kuendeleza vipaji vya soka. Mwaka huu Airtel Rising Stars itajumuisha jumla ya timu 24 za wasichana na wavulana kutoka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Morogoro, Ilala, Kinondoni Temeke, Kigoma, Tanga na Ruvuma ambao baadhi yao watateuliwa kuunda timu za mikoa yao katika fainali za Taifa. Vile vile mashindano ya Taifa yatatumika kuteua timu itakayoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa (inter-country tournament)
Akizunguma katika hafla hiyo, mgeni rasmi Mkurugezi wa Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na Airtel kuwekeza kwenye programu ya soka ya vijana ambao ndiyo nguzo mhimu kwa maendeleo ya mchezo wa soka nchini. Kauli yake iliungwa mkono na Makamu wa Pili wa Rais wa TFF Bw Basibu Ramadhani ambaye alisema program za soka za vijana ndio njia pekee ya kuinua kiwango cha soka nchini.

“Tumeshudia vipaji vingi katika mashindano yaliyopita na bila shaka michuano ya mwaka huu yataendelea kutoa vipaji vingine vingi. Natowa wito kwa timu kubwa hapa nchini kutumia fursa hii kupata wachezaji chipukizi kwa ajili kuimarisha timu zao. Nawatakia washiriki wote mashindano mema na wazingatie nidhamu na taratibu ya mchezo wa soka.” alisema Thadeo.

Programu hii ya Afrika inaungwa mkono na klabu kubwa ya Manchester United kwa lengo la kubaini vipaji vya soka na kuviendeleza ili kuweza kuonekana kwa mawakala, makocha na kupata nafasi ya kutambulika kitaifa na kimataifa.

Ushirikiano wa Airtel na Manchester United katika kuendeleza soka ya vijana ni utekelizaji wa makubaliano yaliyotiwa saini kati ya pande hizo mbili mwezi Disemba 2010 ambayo yanaiwezesha Airtel kutumia hazina ya ufundi wa soka kutoka klabu hiyo kubwa duniani kuendeleza vijana chipukizi barani Afrika.

Vijana wanaoshiriki Airtel Rising Stars mwaka huu hapa nchini wanatajiwa kuanza kujiandikisha mwezi ujao na jumla ya timu 24 kutoka mikoa 9 zitashiriki.

Airtel ni kampuni ya simu za mikononi inayofanya biashara barani Afrika katika nchi za Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Democratic Republic of Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Tanzania, Uganda, na Zambia.