This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, February 27, 2013

KOCHA WA AZAM FC APIGWA ADHABU

Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall (pichani) amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

  Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.
Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.
Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.
Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.
Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.
Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.
Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.
Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.
Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.
Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.
Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

WAFANYA BIASHARA WAVUNA MAHELA VODACOM


 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingw(kulia) akiongea na Mshindi kwenye simu ya mezani wakati wa Droo  ya  kuwapata washindi wa shilingi Milioni 5 na Milioni moja  katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.wanaoshuhudia kushoto kulia ni Matina Nkurlu Meneja Uhusiano,Benjamin Michael Maneja wa Huduma za Ziada na Afisa Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Salehe,Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.



  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu (kulia)akionesha moja ya namba ya simu ya mshindi wa Promosheni ya"MAHELA"aliejishindia kitita cha shilingi Milioni 5 ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 kila mmoja katika promosheni hiyo inayoendelea kuchezeshwa na Vodacom Tanzania,katikati ni Maneja wa Huduma za ziada wa Vodacom Bw.Benjamin Michael,anaefatia ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bi.Chiku Salehe. Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.

msd yawalipua wanaolinda wabadhirifu

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi.
Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la
kujadili tafiti z\ilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha
zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri

BODI YA UTALII YASAINI MKATABA NA WAANDAAJI WA ONESHO LA UTALII LA INDABA AFRIKA KUSINI, KUANZISHA ONESHO LA SWAHILI TOURISM FAIR NCHINI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga katikati wa tatu kutoka kulia, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki kushoto na Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd wakisaini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha onesha la Utalii litakalojulikana kwa jina la Swahili Tourism Fair kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika nchini Tanzania kwenye ukumbi huohuo wa Mlimani City Dar es salaam kuanzia Oktoba 2-5 mwaka huu, Wanaoshuhudia tendo hilo la kusainiwa kwa mkataba huo nyuma ni Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na kulia ni Ian Kaduma Mwanasheria wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Kampuni ya Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd Pia ndiyo inayoandaa maonyesho makubwa ya utalii nchini Afrika Kusini yanayojulikana kama Indaba 
 Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd akisaini mkataba huo huku Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akishuhudia tukio hilo kushoto ni Ian Kaduma Mwanasheria wa TTB

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea leo February 27, 2013.