This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, February 25, 2014

MAJAMBAZI WAUWAWA ARUSHA

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Watu wanne ambao bado hawajafahamika wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa baada ya kupigwa risasi na askari Polisi. Tukio hilo lilitokea jana tarehe 21.02.2014 muda wa saa 1:00 jioni katika bar moja iitwayo Pama iliyopo maeneo ya Makao Mapya jijini hapa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, tukio hilo lilitokea mara baada ya jeshi la polisi Mkoani hapa kupata taarifa toka kwa raia wema kwamba watu hao walikuwa wanapanga kwenda kufanya tukio la uhalifu katika kituo kimojawapo cha kuuzia mafuta kilichopo jijini hapa ambapo ufuatiliaji wa taarifa hiyo ulianza.

Ilipofika muda huo askari hao walikwenda katika bar hiyo na mara baada ya majambazi hao kuwaona askari hao walihisi wanafuatiliwa ndipo mmojawao ghafla alitoa bastola  na kufyatua risasi tatu ambapo moja ilimparaza askari mmoja aitwaye F. 1416 D/Ssgt Richard katika mkono wake wa kushoto

 “Kufuatia hali hiyo askari nao waliamua kujibu mapigo kwa kupiga risasi ambapo wanne kati ya watano walijeruhiwa na mmojawao alifanikiwa kukimbia akiwa na silaha inayosadikiwa kuwa ni SMG”. Alisema Kamanda Sabas.

Kamanda Sabas alisema kwamba, majambazi hao walifariki dunia wakiwa njiani kuelekea hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu na miili yao imehifadhiwa hospitalini hapo kwa ajili ya utambuzi toka kwa ndugu na jamaa wa karibu.

Aidha Kamanda Sabas alisema, katika eneo la tukio askari hao walipata bastola moja aina ya Star yenye namba 42640 FNH PISTOLE MODEL KAL 7.65 ikiwa na risasi tatu katika magazine, maganda matatu ya risasi pamoja na begi moja dogo la mgongoni lenye rangi nyekundu likiwa na risasi nne hivyo kufanya jumla ya risasi saba kupatikana.

Bado Jeshi la Polisi Mkoani hapa linaendelea na upelelezi kuhusiana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumtafuta mtuhumiwa mmoja aliyekimbia.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Sabas aliendelea kuwashukuru wananchi wa Arusha kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoutoa kwa jeshi la Polisi Mkoani hapa na kuwasihi waendelee kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu hali itakayosaidia kukomesha matukio ya uhalifu mkoani hapa.

MREMBO AFARIKI GHAFLA GUEST ARUSHA

MREMBO mmoja ambaye alihu-dumu kwenye nyumba ya kulala wageni na baa (jina tunalo) iliyopo Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Blandina Michael (33) amekutwa amekufa kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo huku chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na vitendo vya ushirikiana.
Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye pia anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa kafara mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa, kila mwaka mtu mmoja katika biashara zake hupoteza maisha ghafla. 
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alipoongea na Uwazi juzikati alikanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni muumini mzuri wa imani yake. 
‘’Hao watu wanapotosha sana, unajua kuna mwaka mwanaume mmoja alikufa ghafla kwenye nyumba yangu ya kulala wageni, alikuja na mpenzi wake ila alimeza Viagra ambazo hata polisi walizikuta mezani. 
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema. 
Kifo cha Blandina kilitokea ndani ya chumba huku mtu mmoja anayedaiwa kuwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Timo, mkazi wa eneo hilo akihojiwa na polisi. 
Marehemu Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga, anaelezwa na bosi wake huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa familia yake kwa vile alimwamini sana. Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa na tatilo la kiafya. Bosi huyo alisema mwili wa marehemu uligundulika baada ya mfanyakazi mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2 asubuhi ambapo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa ndipo alipoamua kwenda kumgongea katika chumba hicho. Alisema baada ya kufika alishangaa kukuta mlango wa chumba chake uko wazi na alipochungulia alibaini kwamba Blandina alikuwa amefariki dunia. Hata hivyo, polisi baada ya kufika na kuufanyia uchunguzi wa awali mwili huo hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote linaloashiria kuuawa, ingawa mwili huo ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

TASWIRA MBALIMBALI TOKA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA




ameir
Wajumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Ismail Aden Rage na Kheri Ameir wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuaharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma hadi Ijumaa.
 dovutwa
Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama (UPDP), Fahmi Dovutwa  na Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema wakibadlishana…
ameir
Wajumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Ismail Aden Rage na Kheri Ameir wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuaharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma hadi Ijumaa.
 dovutwa
Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama (UPDP), Fahmi Dovutwa  na Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma. fedh
Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Ismail Aden Rage (kulia) na Mjumbe mwezie na Naibu Waziri wa Fedha Mwingulu Nchemba (kushoto) wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma.
hamis
Wajumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Dkt Khamis Kigwangalla (kulia) akisalimiana na Mjumbe mwezie ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta (kushoto)  nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma. 
Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba(kulia) alisamiana na mwandishi na Mpiga picha wa Kampuni ya Mwananchi Emmanuel Helman jana mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kikao cha Bunge.
jenista
Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni NaibuWaziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Jenista Mhagama (kushoto) na Mjumbe mwezie Lediana Mung’ong’o wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma. kissu
Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Shaban Kissu (koshoto) na Naibu Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Juma Mkamia (kulia) wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma. mapalala
Mjumbe wa Mkutano wa Bunge la Katiba  ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta (kushoto)  akisalimiana na Mjumbe mwezie James Mapalala nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma. nagu
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji ) Dkt Mary Nagu (kushoto) akibadilishana mawazo na Mjumbe mwenzie Paul Kimiti  jana mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kikao cha Bunge hilo.
Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Fedha  Mwingulu Nchemba akiteta jambo na Mjume wa Bunge hilo Philemon Ndesamburo jana mjini Dodoama mara baada ya kuharishwa kikao cha Bunge. simba
Wajumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ambao pia ni wapenzi na wananchama wa Timu ya Simba wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Juma Mkamia, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta (katikati)  na Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage. oWajumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma.

NI AIBU ILIOJE BUNGE LA KATIBA!

NYALANDU APANGUA WAKURUGENZI MALIASILI


nyalandupx_745e8.jpg
Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewaondoa katika nyadhifa zao, Wakurugenzi mbalimbali kwa sababu zilizoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.
Hatua ya Nyalandu imekuja ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Bunge la Desemba 22, 2013 lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.
Nyalandu alisema: "Namwondoa Prof Alexander Songorwa (Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori) na kumteua Paul Sarakikya kukaimu nafasi hiyo."

Alisema pia kuwa amemwondoa Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Profesa Jafari Kidegesho kwenye nafasi hiyo na Dk Charles Mulokozi ameteuliwa kushika wadhifa huo.
Mwingine aliyeteuliwa ni Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji-Ujangili, nafasi iliyoachwa wazi na Sarakikya wakati Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, Nebbo Mwina anabaki kwenye nafasi yake.
Nyalandu alisema Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori na kwamba waliotangazwa kuondolewa kwenye nyadhifa, kazi zao mbadala zitatangazwa baadaye.
Waziri Nyarandu alitoa siku 30 kwa Wakurugenzi Wakuu wa kila Idara, Shirika na Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, kutengeneza viashiria vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) na kuvikabidhi kwake.
Alisema hatua hiyo itafanikisha kufikiwa malengo ya wizara hiyo, kwani uwajibikaji na ufanisi wa kazi za kila siku utapimwa katika hali ya uwazi ili mikakati ya wizara itekelezwe katika mifumo inayopimika na hatimaye kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Waziri huyo aliagiza kila mtumishi akiwamo yeye mwenyewe, kutekeleza majukumu yaliyopangwa kwa kuzingatia kanuni za mwenendo (code of conduct), zitakazopendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo.

HATIMAYE MTOTO MWENYE UVIMBE WA AJABU AKATWA MGUU NCHINI INDIA


Mtoto mwenye uvimbe wa ajabu, Hamis Liyuga akiwa anaandaliwa kupelekwa katika chumba cha upasuaji.
 
 Hamis Liyuga akipelekwa katika chumba cha upasuaji.…
 
Mtoto mwenye uvimbe wa ajabu, Hamis Liyuga akiwa anaandaliwa kupelekwa katika chumba cha upasuaji.
 

...Akiwa ndani ya chumba cha upasuaji.
...Akiwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Mwandishi wa Global Publishers, Imelda Mtema (kushoto) aliyeambatana na mtoto Hamis Liyuga nchini India.