This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, December 28, 2013

MKE AKATWA MAPANGA, HAWARA ATAJWA


Stori: Timoth Itembe, TARIME

MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya Nyamisangura, wilayani hapa, Eliza Marwa,28, hivi karibuni amenusurika kuuawa na mumewe, baada ya majirani kufika kumuokoa kutokana na kukatwakatwa mapanga.

Mariamu akiugulia maumivu.
Mama huyo aliliambia gazeti hili akiwa katika Hospitali ya Wilaya Bomani, Tarime kuwa mume wake Marwa Ogora alimkatakata mapanga baada ya kumtuhumu kuwa akikwenda kwa hawara yake badala ya kwenda kwenye mazishi ya mjomba wake…

TARIME
MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya Nyamisangura, wilayani hapa, Eliza Marwa,28, hivi karibuni amenusurika kuuawa na mumewe, baada ya majirani kufika kumuokoa kutokana na kukatwakatwa mapanga.

Mariamu akiugulia maumivu.
Mama huyo aliliambia gazeti hili akiwa katika Hospitali ya Wilaya Bomani, Tarime kuwa mume wake Marwa Ogora alimkatakata mapanga baada ya kumtuhumu kuwa akikwenda kwa hawara yake badala ya kwenda kwenye mazishi ya mjomba wake huko Bunchari.
Akifafanua zaidi, Eliza alikuwa na haya ya kusema: ‘’Mjomba alifariki na mazishi yake yalifanyika Desemba, kumi na sita mwaka huu ambapo nilihudhuria baada ya kumwarifu mume wangu kuwa nitahudhuria lakini alinijibu kuwa hakuwa na fedha za kunipa ili niende kwenye mazishi.
“Nilichukua jukumu la kwenda kwa kutumia nauli yangu kwa kuwa muda huo mume wangu alikuwa kazini na baada ya mazishi kesho yake asubuhi Desemba kumi na saba mwaka huu nilirudi nyumbani na kumkuta mume wangu ambaye alianza kunipiga kwa mpini wa jembe kisha panga akidai kuwa sikuwa nimeenda kwenye mazishi badala yake nilikuwa nimeenda kwa mpenzi wangu.
“Alinishambulia sehemu mbalimbali za mwili hususani kichwani, kidogo anitoe ubongo, wasingekuwa majirani kuniokoa baada ya kupiga yowe naamini angeniua kwani hivi sasa siwezi hata kuamka na masikio yameziba, miguu ina ganzi, siwezi kutembea.
“Mume wangu Ogora amekuwa akinipiga mara kwa mara lakini kutokana na watoto tuliozaa naye nimekuwa nikivumilia mateso, naogopa kuondoka na kuacha watoto walelewa na mama wa kambo,”alidai mama huyo.
Ogora hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani anasakwa na dola na afisa mmoja wa polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema  wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa. Naye daktari wa hospitali aliyolazwa mama huyo, Nega Malico alikiri kumpokea mgonjwa huyo.

Saturday, December 7, 2013

UPEPO MKALI WAEZUA PAA LA SHULE YA MSINGI LUGANGA

1 892ea
Wanafunzi wa shule ya msingi Luganga kata ya Ilolompya Tarafa ya Pawaga Mkoa wa Iringa, wakiangalia sehemu ya paa la chumba cha darasa lililo ezuliwa na upepo mkali hivi karibuni.
2 e40f4
Nyumba ya Mwalimu
4 10483
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Luganga wakicheza nje ya Darasa lililo ezuliwa
5 ff967
Wanafunzi Shule ya msingi Luganga wakiendelea na Masomo ndani ya Darasa lililo ezuliwa na Upepo mkali hivi karibuni,Picha na Said Ng'amilo.(HD)

 Raia wa Afrika Kusini wako kwenye maombolezo kwa siku ya pili hii leo wakiwa kwenye mkesha kwa usiku nzima kwa ajili ya kuomboleza mpendwa wao Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela, aliyeaga dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Watu wamekuwa wakikumbuka mema yake , wakicheza na kuimba Mbele ya makazi yake ya zamani mjini Soweto.
Katika mkutano na Waandishi wa habari , Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliainisha matukio ya juma zima kwa ajili ya maombolezo ambapo ametangaza kuwa siku ya jumapili siku maalum ya maombi na ibada maalum.
Siku ya Jumanne, itakuwa ni siku ya shughuli maalum za maombolezo ya kitaifa ambapo shughuli hizo zitafanyika katika uwanja wenye uwezo wa kukusanya watu 95,000 ulio nje kidogo ya mji wa Johannesburg.
Raia wa Afrika kusini wakiwa kwenye maombolezo
Mwili wa Mandela utalala Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria kuanzia siku ya jumatano mpaka siku ya ijumaa.
Mazishi ya Mandela yatafayika jumapili ijayo tarehe 15 kijijini kwake alikokulia,Qunu.
Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 kabla ya kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.
Serikali yake iliondoa utawala wa kibaguzi wa watu weupe ambao ulikuwa na sera za kuwagawa watu wenye asili ya weupe na weusi.
Raia wa Afrika Kusini nchi nzima wamekuwa wakisali, wakiimba nyimbo za kupinga ubaguzi wa rangi na kuwasha mishumaa, wakikumbuka maisha ya Kiongozi wao na namna alivyo wavuta kwa mtindo wa maisha yake.

KINANA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI PORINI, AOMBOLEZA KIFO CHA NELSON MANDELA


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusimama njiani akitokea wilayani Makete akielekea wilayani Wanging"ombe, katika ziara yake maalum ya Mkoa wa Njombe kuhusu Chama cha Mapinduzi kilivyopokea kifo cha mpigania uhuru wa Afrika Kusini na mtu aliyeheshimiwa sana duniani Mzee Nelson Mandela kama alivyojulikana kama "Madiba" aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo ijumaa tarehe 6, Kinana amesema CCM inatambua jinsi Nelson Mandela alivyoipigania nchi yake na Afrika kwa ujumla, kuikomboa mikononi mwa ubaguzi wa rangi na kuiweka huru,…

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusimama njiani akitokea wilayani Makete akielekea wilayani Wanging"ombe, katika ziara yake maalum ya Mkoa wa Njombe kuhusu Chama cha Mapinduzi kilivyopokea kifo cha mpigania uhuru wa Afrika Kusini na mtu aliyeheshimiwa sana duniani Mzee Nelson Mandela kama alivyojulikana kama "Madiba" aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo ijumaa tarehe 6, Kinana amesema CCM inatambua jinsi Nelson Mandela alivyoipigania nchi yake na Afrika kwa ujumla, kuikomboa mikononi mwa ubaguzi wa rangi na kuiweka huru, Ameongeza kwamba CCM na wanachama wake pamoja na watanzania wote watakumbuka mambo mema yote aliyoifanyia nchi yake na Afrika kwa ujumla na kuyaenzi kwa vitendo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Cchama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akizungumza nao alipozungumzia kifo cha ayati Nelson Mandela huko Wanging"ombe mkoani Njombe leo.
Katibu Mkuu wa Cchama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kukagua shule ya sekondari ya Makete Girls iliyopo katika kijiji cha Mtweve wilayani Makete leo akiwa njiani kwenda Wilayani Wanging"ombe, kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kukagua sekondari ya Makete Girls katika kijiji cha Mtweve akiwa njiani kwenda Wanging"ombe mkoani Njombe, Kutoka kulia ni Toto Timoth ambaye ametoa tani tano ya mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo,Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akiongozana Hosea Mpagike Katibu wa CCM mkoa wa Njombe mara baada ya magari kukwama njiani kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Hosea Mpagike Katibu wa CCM mkoa wa Njombe wakisubiri magari yaliyokuwa yamenasa kwenye tope wakati msafara ukielekea wilayani Wanging'ombe leo.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kutoka kulia na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wa pili pamoja na waandishi wahabari wakitembea kwa miguu huku magari yakiwafuata mara baada ya kuyanasua kwenye tope.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili wilayani Wanging'ombe leo, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi.
"Kweli Bini ana Huruma" Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Bibi Geremana Mrwiro mwanakijiji ambaye alileta jembe ili litumike kwa kusaidia kunasua magari yaliyokuwa yamekwama kwenye tope.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kijiji cha Usuka kilipo kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima wilayani Wanging'ombe ambapo Katibu mkuu wa CCM alitembelea vijana walioamua kujiunga pamoja na kuendesha kilimo
Baadhi ya vijana hao wakinyanyua kadi zao juu ili kula kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa na Ndugu Abdulrahman Kinana leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi kijana Said Mkweta.
Utulivu wa kula kiapo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi kuhuso moja ya Power Tiller itakayotumiwa na vijana hao kulimia shamba lao ili kuwahi mvua zinazonyesha.
Gari lililokuwa likitumiwa na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa likinasuliwa kwenye tope mara baada ya kuteleza na kuingia kandokando ya mtari
Juhudi za kunasua zikiendelea.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata kulia Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakitoka nje mara baada ya katibu mkuu huyo kuzindua jengo la kitegauchumi la CCM mkoa wa Njombe leo ambalo limepangishwa na Wizara ya Fedha.

AIRTEL BINGWA KUFUNGUKIA MBAGALA ZAKHIEM LEO

Young killer
Haya sasa mabingwa wote wa Airtel bingwa  kula bata pamoja wikiendi hii Mbagala. Kama wewe ni bingwa wa kusakata kabumbu na kuonyesha umahili wa kumiliki mpira njoo leo tuonyeshe jumamosi hii MBAGALA ZAKHIEM kuanzia saa sita mchana mpaka saa 12 na nusu zawadi kibao kutolewa jezi, tisheti.Wasanii watakaopanda stajini ni Ney wa Mitego, Young killer  na Vinoko shackers ,Pia wadada…
Huku tukishuhudia draw ya Mimi Bingwa watu wanavyojishindia mamilioni na ticket ya kwenda Old Trafford kuangalia live mechi za  Man United  bure. Kama haitoishi sasa screen kubwa ya ukubwa zaidi ya mita  4 itaonyesha live mchezo wa Man United na Newcastle United.
Kiingilio ni BURE.