This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, February 26, 2014

Al Ahly watua Dar na vyakula, maji




WAPINZANI wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri wameonyesha wamepania kuhakikisha hawapotezi mchezo wa Jumamosi baada ya kutua nchini na maji na baadhi ya vyakula ambavyo watapikiwa wachezaji wao.
Habari za uhakika kutoka Cairo, zimeeleza Ahly wamebeba chupa za maji, baadhi ya vyakula na kazi hiyo itafanywa na mpishi wao maalum raia wa…

WAPINZANI wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri wameonyesha wamepania kuhakikisha hawapotezi mchezo wa Jumamosi baada ya kutua nchini na maji na baadhi ya vyakula ambavyo watapikiwa wachezaji wao.
Habari za uhakika kutoka Cairo, zimeeleza Ahly wamebeba chupa za maji, baadhi ya vyakula na kazi hiyo itafanywa na mpishi wao maalum raia wa Ujerumani ambaye amekuwa akisafiri na timu hiyo kwa misimu miwili sasa, kila inapotoka nje ya Misri.
Mmoja wa Watanzania wanaoishi jijini Cairo, amesema waliondoka na vifaa hivyo jana usiku na wanatarajia kuwasili Dar leo alfajiri na ndege ya Egypt Air.

“Wamebeba kila kitu, wakati wanapita hapa airport, baadhi ya vitu vyao vilishapita. Kwa kuwa sisi tuko hapa kazini, tulisikia wakisema kuwa ni maji na vyakula kwa ajili ya wachezaji wa Ahly.
“Wachezaji walifuatia baadaye sana, hapa walikuja na basi maalum na baadaye wakaingia ndani ya uwanja wa ndege. Wanaonekana wako fiti na walikuwa wakitumia muda mwingi kutaniana na walionekana kuwa na furaha tu,” alisema mpashaji huyo ambaye ameishi nchini humo kwa zaidi ya miaka 10 na anazungumza lugha ya Kiarabu kwa ufasaha.
Timu hiyo imekuwa ikibeba maji na vyakula ikiwa ni sehemu ya kujiwekea tahadhari ya kuhujumiwa au kuhofia ubora wa maji katika nchi husika wanayokwenda kucheza mechi yoyote ya kimataifa. Mfumo huo hutumiwa pia na timu ya taifa ya Misri.
Hii si mara ya kwanza kwa timu za Kiarabu kufanya hivyo, Ahly iliwahi kufanya hivyo ilipocheza na Yanga na kuifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, mwaka 2008, pia Zamalek nayo ilifanya hivyo lakini ikapigwa bao 1-0 na Simba, mwaka 2003.

Alphonce Mawazo Meneja Kampeni wa Mgombea wa Chadema Kalenga, Achukua Nafasi ya Lema



Alphonce Mawazo, Kamanda wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Picha na Arusha Times)
Arusha255 inaweza kuthibitisha uteuzi mpya wa Ndugu Alphonce Mawazo kama meneja kampeni za kumnadi mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bi Grace Tengega Mvanga katika uchaguzi mdogo wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Machi 16, 2014 katika Jimbo la Kelenga Mkoani Iringa kwa lengo la kumpata mbunge atakayewakilisha wana Kalenga baada ya kufariki kwa aliyekuwa M<bunge wa Jimbo hilo Marehemu Profesa Mgimwa, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha.
Awali alikuwa ameteuliwa Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema kuwa meneja kampeni, lakini kutokana na majukumu ya Bunge la Katiba imeonekana hatakuwa na muda wa kutosha kufanya kazi hiyo.
Mawazo na lemaAlphonce Mawazo (kushoto) na Gobless Lema latika moja ta tukio la kisiasa.  Hapa chini ni maelezo binafsi ya Mawazo kufuatia uteuzi huo kama alivyoandika kwenye ukufasa wake wa Facebook
“Nakishukuru chama changu cha chadema kwa kuniamini na kunipa heshima kuu ya kuwa kampeni meneja wa hapa Kalenga panapofanyika uchaguzi mdogo wa ubunge baada kifo cha aliyekuwa Mbunge Wa jimbo hili Dr. Mugimwa.
Mikoba hii nimeirithi kutoka kwa Mh: Lema Mbunge wa Arusha Mjini kutokana na wabunge kushiriki moja kwa moja kwenye Bunge la Katiba hivyo kuwa na muda mfinyu sana aa kufanya shughuli zingine nje ya Bunge.
Natambua sio kazi ndogo na wala sio mteremko.  Ninchoweza kuwaahidi ni mapambano yasiyo na simile. Dhamira yangu ni dhabiti mno, utayari wangu kutimiza adhima ya mioyo ya watanzania na ile ya chama changu haipimiki. Hakuna gharama itakayo kuwa ngumu kwangu kuilipa kwa ajili ya ukombozi wa taifa langu, nina maanisha HAKUNA. Nitajie gharama yoyote nitakuambia am ready to pay ili mradi niwe na uhakika ya kwamba kama ni damu yangu inatakiwa haimwagiki bure kwa faida ya wachache.
Namwamini Benson Kigaila ambaye ni operation kamanda, Mimi humwita General wa vita. Namwamini Dr:slaa kipenzi cha watanzania na MTU shupavu sana. Namwamini Mbowe Mwenyekiti ambaye ni chachu kubwa ya mabadiliko Tanzania na inspirational kwa vijana. Naiamini Kamati Kuu ya Chadema.
Nilipokea kwa mshituko kidogo taarifa za wasaliti wawili kule Shinyaga lakini baada ya kusikia majina yao nikapumua maana nawafahamu fika na kwa wakati mmoja nilishawahi kuwaonya kuwa chama kingewashinda. Yametimia, sina sikitiko hata chembe waacheni waondoke lilikuwa bomu hatari sana. Nimemwambia Dr Slaa asipoteze muda kuwafikiri. Kkwa mila za kiafrika hatuombolezei mimba iliyo haribika.
Mwisho naomba mtuombee sisi tulioko vitani Kalenga, vijana wenu wengi wamejitoa na wako huku, wengi wao wamekuja kwa kusukumwa na matamanio ya mabadiliko na hawajui watakula au kunywa nini. Kama una chochote waweza kutuma kupitia namba yangu 0756039703 au kama unamjua yoyote aliyeko field huku tafadhali msaidie. ALUTA CONTINUA.”

SLAA AWANG'AKIA VIONGOZI WA SERIKALI!!


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amesema tatizo la umaskini linalowakabili Watanzania, linatokana na viongozi walioko madaraka kutokuwa waadilifu.
Alisema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa vyema taifa haliwezi kuwa na watu maskini kama ilivyo hivi sasa.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika katika Vijiji vya Igula katika Kata ya Luwota na Magulilwa mkoani Iringa.
“Nchi hii siyo maskini, imejaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa ipaswavyo, taifa lisingekuwa na umaskini kama ilivyo sasa,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Leo hii viongozi wa CCM wamekosa uadilifu ndiyo maana magogo kutoka katika misitu yetu yanaibiwa na kupelekwa nje ya nchi.
Dk Slaa alisema hayo yanatokana taifa kuongozwa na watu wasio waadilifu, huku Amiri Jeshi Mkuu ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete akishindwa kukabiliana na hali hiyo. Katika mikutano hiyo, Dk Slaa aliwataka wakazi wa Kalenga kumchagua mbunge wao ili kuongeza idadi ya wabunge wake