Wednesday, February 26, 2014

Al Ahly watua Dar na vyakula, maji




WAPINZANI wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri wameonyesha wamepania kuhakikisha hawapotezi mchezo wa Jumamosi baada ya kutua nchini na maji na baadhi ya vyakula ambavyo watapikiwa wachezaji wao.
Habari za uhakika kutoka Cairo, zimeeleza Ahly wamebeba chupa za maji, baadhi ya vyakula na kazi hiyo itafanywa na mpishi wao maalum raia wa…

WAPINZANI wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri wameonyesha wamepania kuhakikisha hawapotezi mchezo wa Jumamosi baada ya kutua nchini na maji na baadhi ya vyakula ambavyo watapikiwa wachezaji wao.
Habari za uhakika kutoka Cairo, zimeeleza Ahly wamebeba chupa za maji, baadhi ya vyakula na kazi hiyo itafanywa na mpishi wao maalum raia wa Ujerumani ambaye amekuwa akisafiri na timu hiyo kwa misimu miwili sasa, kila inapotoka nje ya Misri.
Mmoja wa Watanzania wanaoishi jijini Cairo, amesema waliondoka na vifaa hivyo jana usiku na wanatarajia kuwasili Dar leo alfajiri na ndege ya Egypt Air.

“Wamebeba kila kitu, wakati wanapita hapa airport, baadhi ya vitu vyao vilishapita. Kwa kuwa sisi tuko hapa kazini, tulisikia wakisema kuwa ni maji na vyakula kwa ajili ya wachezaji wa Ahly.
“Wachezaji walifuatia baadaye sana, hapa walikuja na basi maalum na baadaye wakaingia ndani ya uwanja wa ndege. Wanaonekana wako fiti na walikuwa wakitumia muda mwingi kutaniana na walionekana kuwa na furaha tu,” alisema mpashaji huyo ambaye ameishi nchini humo kwa zaidi ya miaka 10 na anazungumza lugha ya Kiarabu kwa ufasaha.
Timu hiyo imekuwa ikibeba maji na vyakula ikiwa ni sehemu ya kujiwekea tahadhari ya kuhujumiwa au kuhofia ubora wa maji katika nchi husika wanayokwenda kucheza mechi yoyote ya kimataifa. Mfumo huo hutumiwa pia na timu ya taifa ya Misri.
Hii si mara ya kwanza kwa timu za Kiarabu kufanya hivyo, Ahly iliwahi kufanya hivyo ilipocheza na Yanga na kuifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, mwaka 2008, pia Zamalek nayo ilifanya hivyo lakini ikapigwa bao 1-0 na Simba, mwaka 2003.

0 comments: