Friday, February 28, 2014

WANACHAMA WA SACCOS YA WALIMU KILOLO WATAKIWA KUREJESHA MADENI


Afisa  ushirika mkoa  wa Iringa John Kiteve  akifungua mkutano huo
 
Mwakilishi wa CRDB Iringa akifuatilia matukio  katika mtandao huu 

Mwakilishi wa benk ya CRDB Iringa Bw Bruno  akiwahamasisha  kujiunga na bima mbalimbali  


Afisa ushirika mkoa wa Iringa John Kiteve akifungua mkutano mkuu wa Saccos ya  Walimu Kilolo leo
Na  Francis Godwin Blog
WANACHAMA wa  chama cha   kuweka na kukopa  cha  Kilolo Teacher’s  Saccos wilayani  Kilolo  mkoani  Iringa  wametakiwa  kujenga  uaminifu  katika  kulipa madeni ya  mikopo  ambayo  wamekopeshwa badala ya  kugeuza ni  sadaka  kwao.
Wito  huo  umetolewa na afisa  ushirika  wa  mkoa wa Iringa  John  Kiteve  wakati  akifungua  mkutano mkuu  wa mwaka  leo  mjini  Kilolo.
Kiteve  alisema  kuwa  wapo  baadhi ya  wanachama  wasio  waaminifu ambao  wamekuwa  wakiomba mikopo na mara  baada ya  kupewa  mikopo  hiyo wamekuwa  wakishindwa  kurejesha  mikopo   hiyo  jambo  ambalo  linachangia  vyama  vingi  vya  ushiriki na mikopo  kuyumba hapa nchini.
“ wapo  baadhi  ya  wanachama  ambao  si  waaminifu  wamekuwa  wakichukua  mikopo  na wakati  wakihama  wamekuwa  wakihama na madeni  ya  saccos  bila kufika  ofisini  za  Saccos na kueleza  jinsi ambavyo atarejesha  mikopo  hiyo.
Hivyo  aliwataka  wanachama hao  kujenga utamaduni  wa  kurejesha  mikopo kwa  wakati  ikiwa ni  pamoja na  kutumia  mikopo  hiyo  kwa maendeleo  badala ya  kutumia  mikopo kwa anasa  ambazo  zitakwamisha  urejeshaji wa madeni ya mikopo  yao.
Pia  Kiteve  alisema  kuwa  Saccos  hiyo  ya walimu  wilaya ya  kilolo ni moja kati ya  Saccos  ambazo  zimekuwa  zikifanya  vema na kuwa  tofauti na  saccos  nyingine za  walimu  nchini  kutokana na utaratibu mzuri  wa Saccos  hiyo kuwaunganisha  walimu wa  shule za msingi na  sekondari.
Hata  hivyo  alisema ili kuondoa matabaka katika Saccos  hiyo ni  vema  wanachama  wote  kuwa  kitu kimoja  badala ya  kuwepo kwa matabaka  kati ya  walimu wa  shule za msingi na Sekondari jambo ambalo litaua nguvu ya  Saccos  hiyo.
  katibu  wa  chama  hicho  Fabian  Chavala alisema  kuwa  chama   hicho  kilianzishwa  mwaka 2007 na  kupata  usajili wake  IR 465 kikiwa na  wanachama  60 wakiwemo  wanaume 36 na  wanawake 24 ila  kwa  sasa  kina  wanachama 516  kati yao ni  walimu wa   shule za msingi ni 416 na  wengine  waliobaki ni  kutoka  shule za sekondari.
Hata  hivyo  alisema  kumekuwepo  na mafanikio makubwa katika  chama hicho  kwa chama  kuongeza wanachama kwa kasi na kuwa na jengo lake pamoja na  kuwa na mahusiano mazuri na taasisi za kifedha  hasa benk ya CRDB
Mwenyekiti  huyo  alisema kuwa wanachama  wa chama  hicho  wameendelea  kunufaika na mikopo  na kuwa hadi sasa  wanachama 35  wamekopeshwa  mikopo ya ununuzi wa vyombo  vya usafiri yakiwemo  magari  manne na pikipiki 31,wanachama 343 wamepewa  mikopo ya ujenzi wa nyumba za kisasa ,wanachama 156 wamekopeshwa mikopo ya masomo ya  watoto  wao na wanachama 28  wamepewa  mikopo ya biashara na  kilimo .(P.T)

0 comments: