Friday, February 28, 2014

BANZA: NILIANZA SIGARA, BANGI, UNGA ILA SASA…

MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefunguka mazito juu ya matumizi mabaya ya bangi na madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na jinsi alivyokuwa akiyatumia.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Global TV Online mwanzoni mwa wiki hii, Banza alikiri kutumia madawa ya kulevya na kusema; “Nilianza kuvuta sigara ya kawaida, nikaja bangi na baadaye madawa ya kulevya aina ya Heroin ambapo alikuwa akiyatumia kwa…
MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefunguka mazito juu ya matumizi mabaya ya bangi na madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na jinsi alivyokuwa akiyatumia.
Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ kabla ya kufanya mahojiano na Global TV Online.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Global TV Online mwanzoni mwa wiki hii, Banza alikiri kutumia madawa ya kulevya na kusema; “Nilianza kuvuta sigara ya kawaida, nikaja bangi na baadaye madawa ya kulevya aina ya Heroin ambapo alikuwa akiyatumia kwa kuchanganya na sigara au bangi.
“Ujana ulisababisha nikajiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya ila sasa nimeacha kabisa na nawashauri vijana wenzangu kuwa mbali na kilevi hicho kwani kama huna kipato cha kutosha unaweza kugeuka kibaka maana mwili ukizoea ni vigumu kuacha.”

0 comments: