This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, September 11, 2013

SIRI NJE

USIRI ulikuwa umetawala kuhusu mmiliki wa meli ya Kitanzania iliyonaswa juzi nchini Italia, ikiwa na tani 30 za madawa ya kulevya aina ya bangi lakini sasa kila kitu kinaweza kuwekwa nje bin hadharani kutokana na taarifa mpya ambazo gazeti hili limezipata.

Mv Gold Star ikiungua.
Uwazi linazo ‘data’ kuwa mmoja wa wamiliki wa meli hiyo ni mfanyabiashara wa Kitanzania mwenye asili ya Bara la Asia ambaye alipata kuwa memba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu…
Stori: Mwandishi Wetu
USIRI ulikuwa umetawala kuhusu mmiliki wa meli ya Kitanzania iliyonaswa juzi nchini Italia, ikiwa na tani 30 za madawa ya kulevya aina ya bangi lakini sasa kila kitu kinaweza kuwekwa nje bin hadharani kutokana na taarifa mpya ambazo gazeti hili limezipata.
Mv Gold Star ikiungua.
Uwazi linazo ‘data’ kuwa mmoja wa wamiliki wa meli hiyo ni mfanyabiashara wa Kitanzania mwenye asili ya Bara la Asia ambaye alipata kuwa memba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu zilizopita.
Jina la mfanyabiashara huyo linabaki kwenye kapu letu mpaka baadaye tutakapokuwa kwenye mazingira sahihi ya kumtaja, kwani kufanya hivyo kwa sasa ni kuingilia mamlaka za kisheria ambazo zipo kwenye uchunguzi makini.
Habari zinafafanua kuwa mbunge huyo, hamiliki meli hiyo peke yake, bali kuna watu wengine ambao ni raia wa Visiwa vya Marshall, barani Australia.
Magunia ya bangi japo siyo yaliyokuwa katika MV Gold Star.
Inaelezwa zaidi kwamba watu hao kutoka Marshall ni mabilionea wakubwa ambao wanamiliki visiwa vitatu kwenye Bahari ya Pacific ambavyo ni Ujae Atoll, Ujelang Atoll na Lib.
Mabilionea hao ndiyo wenye Kampuni ya Gold Star Shipping ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma za usafiri wa majini hususan kwa njia ya meli.
Gold Star Shipping ni kampuni iliyosajiliwa Visiwa vya Marshall lakini kwa ushirikiano na mbunge huyo wa zamani, waliileta nchini meli yao ya mizigo ya MV Gold Star, ikasajiliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

MAGUMASHI YALIPOANZA
MV Gold Star ilisajiliwa Zanzibar ili tu ipate kibali cha kutumia Bendera ya Taifa la Tanzania, kwani baada ya hapo, imekuwa ikipuyanga kwenye mataifa mengine, ikitoa huduma za usafiri pasipo kurudi kwenye nchi iliyosajiliwa.
Taarifa za hivi karibuni, zinaonesha kuwa imeshakwenda na kurudi Misri mara mbili, Algeria mara mbili na Uturuki, huku Bandari ya Zanzibar ambayo inaitambulisha kama ndiyo nyumbani kwao, haijapata kutia nanga hata mara moja.
Julai 29, 2013, saa 2:04 asubuhi, ilitia nanga Bandari ya Said, Misri. Juni 18, 2013, saa 1:05 jioni, iliwasili Bandari ya Mostaganem, Algeria. Mei 31, 2013, saa 9:04 usiku, ilifika Bandari ya Iskenderun, Uturuki. Mei 24, 2013, saa 1:04 asubuhi, iliingia Bandari ya Said, Misri na Aprili 14, 2013, saa 2:02 asubuhi, ilipiga king’ora Bandari ya Mostaganem, Algeria.

WASIFU WA MELI
Bandari ya nyumbani ni Zanzibar, imetengenezwa mwaka 1975, watengenezaji ni Kampuni ya Astilleros De Mallorca, iliyopo Palma De Mallorca, Hispania, mmiliki ni Gold Star Shipping kutoka Visiwa vya Marshall, meneja ni Gold Star Shipping, ipo katika jamii ya Hellenic Shipping Register.

WAMILIKI WA ZAMANI
Ilimilikiwa na Ibrahim Junior mpaka Februari 2011, Breogan I (aliiuza Novemba 2006), Breogan (Machi 2002), Estela De Mar (Desemba 1996), Inezgane (1996), Puerto Suances (1988) na Suecia (1985).

NI MADAWA YENYE THAMANI KUBWA
Kwa mujibu wa ripoti za mitandao ya Waitaliano na Waingereza, MV Gold Star, ilipakia mzigo wa madawa ya kulevya nchini Uturuki na walikuwa wanafanya jaribio la kuingiza mzigo huo wenye tani 30 nchini Italia.
Walinzi wa ufukweni kwenye Bahari ya Mediterranean, waliishtukia meli hiyo na kuizingira, watu waliokuwemo baada ya kuona hali ni mbaya, waliwasha moto kuiteketeza MV Gold Star kisha kufanya jaribio la kutaka kutoroka kupitia boti ndogo.
Askari hao wa ufukweni, walishirikiana na maofisa uhamiaji wa Italia kuwakamata watu tisa ambao walikuwemo kwenye meli hiyo na baada ya kuwahoji, ilibainika wote wanatokea nchi za Misri na Syria.
Taarifa kutoka kwa maofisa uhamiaji wa Italia zinasema kwamba baada ya kuwahoji watuhumiwa, ilibainika waliamua kuiteketeza meli hiyo kwa moto ili kuondoa ushahidi wa tani 30 za madawa ya kulevya zilizokuwemo.
Ilibainishwa pia kuwa thamani ya madawa hayo ya kulevya yaliyokamatwa ni pauni milioni 50 ambazo kwa chenji ya Tanzania ni shilingi bilioni 126.5.

FEDHA HIZO ZINAWEZA KUENDESHA WIZARA TATU
Kama mzigo huo ungevuka salama na kuuzwa, fedha hizo zinatosha kuendesha wizara tatu katika Serikali ya JK, hii ni kwa mujibu wa makadirio na mapato ya matumizi (bajeti), mwaka wa fedha 2013-2014.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto bajeti yake ni shilingi bilioni 23, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo shilingi bilioni 30 na Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo shilingi bilioni 67, jumla shilingi bilioni 120.
Hii inamaanisha kuwa fedha hizo za wauza unga, zinaweza kuendesha wizara hizo na chenji itabaki shilingi bilioni 6.5 ambazo zinaweza kujenga shule na mabweni mengi tu. Uchambuzi huo ni kuonesha namna ambavyo wauza unga walivyo watu hatari, kwani wana pesa nyingi.

ITALIA KAZI WANAYO
Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao, vikosi vya uokoaji nchini humo, kuanzia vya majini, anga na nchi kavu, viliizingira meli hiyo kuzima moto uliokuwa unaiteketeza.
Mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni, taarifa zilieleza kwamba bado shughuli ya kuzima moto ilikuwa inaendelea.

TANZANIA HAKUNA ANAYEJUA
Uwazi lilifanya jitihada za kuwatafuta watu mbalimbali wanaohusika na udhibiti wa madawa ya kulevya nchini lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa na taarifa.
Hata Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, aliliambia Uwazi akiwa nchini Ethiopia kuwa hajui chochote kuhusu meli hiyo kukamatwa lakini aliahidi kufuatilia.

NI SKENDO NZITO KWA NCHI
Kukamatwa kwa meli hiyo kunazidi kuipaka matope Tanzania, kwani hivi karibuni raia wake wamekuwa wakikamatwa katika mataifa mengine, wakiwa wanasafirisha madawa ya kulevya. Vilevile, kuna ile skendo ya meli ya Wairan yenye Bendera ya Tanzania ambayo iliibua gumzo mwaka huu lakini suluhisho halijapatikana.

NJEMBA YAMKUTA MAZITO

NJEMBA moja iliyojulikana kwa jina la Haji Bakari maarufu kama Mchome limekamatwa baada ya kudaiwa kutapeli kiasi cha shilingi 570,000 kwa njia ya simu za mkononi.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, njemba hilo lilifanikisha utapeli huo kwa kutumia majina ya watu wanaofahamiana na washirika kibiashara.

Kijana huyo aliomba pesa hizo kwa madai kuwa gari lake limemharibikia maeneo ya Chalinze mkoani Pwani hivyo alihitaji kiasi hicho ili aweze kulitengeneza. Bila hiyana, aliyeombwa alitoa fedha hizo kwa moyo mmoja ingawa kwa awamu mbili.

Akizungumza na gazeti hili, mtu aliyetapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la Godilizen Moshi alisema baada ya kumkamata mtu huyo, alijihami na kusema kuwa aliyefanya mchezo huo ni pacha wake.

Akisimulia mkasa huo, Moshi alidai: “Kijana huyu ni mzoefu na alikuwa…

Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'
NJEMBA moja iliyojulikana kwa jina la Haji Bakari maarufu kama Mchome limekamatwa baada ya kudaiwa kutapeli kiasi cha shilingi 570,000 kwa njia ya simu za mkononi.
Haji Bakari akipandishwa kwenye difenda.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, njemba hilo lilifanikisha utapeli huo kwa kutumia majina ya watu wanaofahamiana na washirika kibiashara.
Kijana huyo aliomba pesa hizo kwa madai kuwa gari lake limemharibikia maeneo ya Chalinze mkoani Pwani hivyo alihitaji kiasi hicho ili aweze kulitengeneza. Bila hiyana, aliyeombwa alitoa fedha hizo kwa moyo mmoja ingawa kwa awamu mbili.
...Akiwa ndani ya difenda.
Akizungumza na gazeti hili, mtu aliyetapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la Godilizen Moshi alisema baada ya kumkamata mtu huyo, alijihami na kusema kuwa aliyefanya mchezo huo ni pacha wake.
Akisimulia mkasa huo, Moshi alidai: “Kijana huyu ni mzoefu na alikuwa akitumia simu nambari 0655 301646, nilimuamini baada ya kunitajia jina la mtu ambaye nafahamiana na tunashirikiana kibiashara.”
Alisema baada ya kukamilisha kumpatia kiasi hicho cha fedha alizoomba alimpigia simu ili kuhakiki kama amezipata lakini ilipopokelewa, mpokeaji alisema alikuwa mazishini mkoani Kilimanjaro, kitu ambacho kilimshtua na kuhisi kutapeliwa.
Baada ya hapo, Moshi aliwataarifu ndugu zake na mara moja msako mkali dhidi ya tapeli huyo ukaanza.
“Nilipagawa baada ya kujibiwa kuwa niliyemtumia fedha yuko Kilimanjaro, jibu hilo lilinichanganya sana,” alisema Moshi.
Kwa mujibu wa Moshi, alitafuta watu wa kumsaidia kumkamata mtu huyo na hatua yao ya kwanza ilikuwa ni kwenda ofisi za mtandao wa Tigo zilizopo Mlimani City jijini Dar ili kujua sehemu halisi alipo tapeli huyo.
Baada ya kueleza tatizo lao, mfanyakazi wa kampuni hiyo aliwaeleza kuwa mtu mwenye namba hiyo anapatikana eneo la Ubungo Kibangu, jijini Dar es Salaam.
“Na kweli tulipoenda Kibangu tukiwa na wenyeji wa huko tulifanikiwa kumpata kirahisi sana na kumchukua, kutokana na kibano alichopewa alisema sio yeye aliyetapeli bali ni pacha wake,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa amekamatwa. “Tunamchunguza kabla ya kumfikisha kortini,” alisema.

DENTI ALIYEDAI KUZAA NA DIAMOND... AUMBUKA, ATISHIA KUJIUA


Video: Sasha siku alipokuwa akiongea na GPL kuhusu madai ya kuzaa na Diamond.
MREMBO Sasha Juma, 20, kwa sasa anapitia kipindi cha majuto, analipia gharama ya kujivalisha ubandidu na kujisingizia kupewa mimba na supastaa, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
 Sasha Juma akiongea na…

Video: Sasha siku alipokuwa akiongea na GPL kuhusu madai ya kuzaa na Diamond.
MREMBO Sasha Juma, 20, kwa sasa anapitia kipindi cha majuto, analipia gharama ya kujivalisha ubandidu na kujisingizia kupewa mimba na supastaa, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Sasha Juma akiongea na GPL..
Sasha, akiwa na macho makavu, alitamka mbele ya waandishi wetu kuwa mimba hiyo aliyopewa na Diamond, ilimgharimu kufukuzwa shule akiwa kidato cha nne mwaka jana.
Unadhani Sasha analo tena? Ameshaumbuka na baada ya simulizi yake ya kutunga kushtukiwa, hivi sasa mrembo huyo anatishia kujiua.
Mr. Juma ambaye ni baba mzazi wa Sasha, aliliambia Risasi Mchanganyiko: “Huyu mtoto ametishia kujiua, anajua makosa aliyoyafanya. Anataka kutuvuruga vichwa, ukweli ni kwamba kila alichokisema kuhusu Diamond ni uongo mtupu.
“Nahisi kuna mtu yupo nyuma yake, sasa anataka kumtumia ili kumchafua Diamond, upande mwingine akili yangu inaniambia yule mtoto anataka umaarufu, maana najua yule ni mwigizaji, sasa pengine anataka kutoka.”
Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
UONGO WA SASHA
Risasi, lilipata taarifa kuhusu malalamiko ya Sasha ambaye alikuwa akidai kupotezewa dira ya maisha na Diamond kwa sababu alimpa mimba na kumtelekeza na mtoto mwenye umri wa miezi minne.
Baada ya kupata ‘tipu’ hiyo, mwandishi wetu alimsaka kwa udi na uvumba mpaka Septemba 4, mwaka huu (Jumatano ya wiki iliyopita) ambapo mrembo huyo alitia maguu kwenye mjengo mkubwa wa magazeti pendwa nchini Tanzania, Global Publishers Ltd.
Baada ya kuwasili makao makuu ya Global Publishers, Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, Sasha aliingizwa kwenye chumba maalum chenye mitambo ya kurekodi sauti na picha kisha akaanza kumwaga simulizi yake.
Alidai kuwa alikutana na Diamond, Mlimani City, mwaka jana, wakapeana namba za simu kabla ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi ambao uliwafikisha kwenye ‘kategori’ ya kuparamia kitandani na kutenda mchezo wa baba na mama pasipo kutumia na kinga.
“Nilipopata mimba Diamond alinishawishi nisitoe, akaniahidi atanisomesha hata kama nitafukuzwa shule. Baadaye nilifukuzwa shule, akazidi kunipa moyo kwamba atanilinda. Mimba ilipokuwa kubwa akapotea, nilipozaa hakujitokeza.
“Diamond akawa siyo yule ambaye alikuwa ananipa moyo. Alibadilika, hali hiyo ikanifanya nione mwanangu hana baba, hata cheti za kuzaliwa, sijamwandika Diamond, mtoto wangu nimempa ubini wa baba yangu, yaani ya Juma.”
Sasha akiwa na mtoto aliyedai ni wa Diamond.
NI UONGO MTAKATIFU
Ili kukamilisha habari hiyo ambayo ilitoka kwenye gazeti hili, toleo la Jumamosi iliyopita, mwandishi wetu aliwasiliana na baba mzazi wa Sasha (Mr. Juma) ambaye alipoambiwa kuhusu mwanaye kuzaa na Diamond, alishtuka kisha akasema:
“Unajua yule mtoto sikai naye, anaishi na mama yake. Mimi sijui chochote ila nashangaa, inawezekanaje apate mimba mpaka azae mimi baba yake sijui? Ngoja niongee na mama yake.”
Mr. Juma alipiga simu kuzungumza na mama yake Sasha mbele ya mwandishi wetu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;
MR. JUMA: Habari yako.
MAMA SASHA: Salama tu, za kwako?
MR. JUMA: Namshukuru Mungu, ebwana mbona Sasha kaongea na mwandishi wa habari anasema kapewa mimba na Diamond na amezaa?
MAMA SASHA: Wewe si unajua haya mambo ya vijana?
MR. JUMA: Mambo ya vijana kivipi? Ina maana mtoto anapata ujauzito mpaka anazaa wewe na baba yake hamjui?
MAMA SASHA: Baba nani, si wewe?
MR. JUMA: Mimi baba yake sijui, ndiyo maana nakuuliza wewe, maana nimesikia umekuwa unawasiliana na Diamond kuhusu hili.
MAMA SASHA: Nani kakwambia? Nimeshasema hayo ni mambo ya watoto, naomba umuulize mwanao vizuri, kama hauna namba yake nikutumie.
Katika mazungumzo hayo, Mama Sasha, hakumpa majibu ya moja kwa moja mzazi mwenzake, kuhusu binti huyo kupata mimba, kuzaa na Diamond kuwa mhusika.

RIPOTI YA WIKI HII
Mr. Juma alifika ofisi za Global Publishers na kueleza: “Jana (Jumapili iliyopita), nilimchukua Sasha na kuzungumza naye kwa kirefu, kwa kifupi alikiri kuwa hajawahi kupata mimba na yule mtoto si wa kwake.
“Mtoto imebainika ni wa dada yake, yaani mtoto mkubwa wa Mama Sasha ambaye anaitwa Khadija. Kuna kitu cha kujifunza hapa kuwa Sasha aliwadanganya mpaka watu ambao niliwakabidhi ili wamsaidie kisanii.
“Kabla sijaongea kwa kirefu na Sasha, nilizungumza na Thabit Abdul (mwanamuziki wa Five Stars) ambaye nilimkabidhi kwake kumsimamia kisanii, nikamuuliza inakuwaje mtoto anapata mimba? Akanijibu hata yeye anashangaa. Kwani hata yeye alishangaa kumuona Sasha akiwa na picha nyingi amebeba mtoto kwenye simu yake.
“Akamuuliza umezaa akajibu ndiyo. Hisia zangu zinazunguka katika mambo mawili, ama aliamua kutunga ili kupata umaarufu kupitia jina la Diamond au alitumwa na mtu. Jana wakati nazungumza na Sasha, nilikasirika sana, nikaona hatutafika pazuri.
“Ikabidi nimpigie simu rafiki yangu mmoja ili amwite azungumze naye. Kweli alimwita wakazungumza, baadaye yule rafiki yangu akaniambia Sasha kasema anaona mambo yanazidi kuwa makubwa, kwa hiyo anataka kunywa sumu afe. Namshangaa sana huyu mtoto, sijui ana kichaa gani?”

UKWELI NI HUU
Kwa mujibu uchunguzi wetu usio na shaka, mtoto aliyepigwa picha akiwa amebebwa na Sasha, mama yake halisi ni dada wa mrembo huyo ambaye ni Khadija.
Sasha na Khadija wanaunganishwa na mama yao lakini kila mmoja ana baba yake.
Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa kwa sasa Khadija anaishi na mwanaye mkoani Tanga, huku Sasha akiendelea kupuyanga ndani ya Jiji la Dar, akiwa hajui tamu wala chungu ya kunyonyesha, vilevile hajawahi kusikia uchungu wa uzazi wala hatambui sura ya ‘leba’ ilivyo.
Khadija akizungumza kupitia simu ya Mr. Juma, huku mwandishi wetu akifuatilia mazungumzo, alisema: “Nikija Dar nitafika Global, mimi ndiyo mama wa yule mtoto na zile picha Sasha alipiga na mtoto siku ya arobaini yake.
“Sasha anataka kunisababishia matatizo na baba mzazi wa mtoto. Mimi kama mama mzazi wa mtoto, simjui Diamond, kwa hiyo hahusiki chochote na mtoto wangu.”
Aidha, Mr. Juma alisema kuwa alimpigia simu Diamond na kumuweka sawa kuhusiana na tuhuma ambazo binti yake alimsakizia.
“Diamond anajua kila kitu, nimeshaongea naye na nimejaribu kumtaka atulize munkari, maana ni wazi zile taarifa zimemchukiza sana. Kweli zimemchukiza.”

DIAMOND ANASEMAJE?
Gazeti hili lilipozungumza na Diamond, alisema: “Nilishasema simjui huyo Sasha, ahadi yangu ipo palepale, nitampeleka mahakamani. Amenichafua sana.
“Masharti yangu ni haya, kama anataka nimsamehe aende kweye redio na televisheni akatangaze kwamba sijampa mimba.”

ONYO
Aibu ambayo Sasha anakutana nayo sasa na tishio la kuburuzwa mahakamani ambalo analikabili kutoka kwa Diamond ni onyo kwa watu wengine ambao wamekuwa na tabia za kuwasingizia wenzao ili kujipatia umaarufu.
Risasi linazo taarifa kwamba tangu alipoumbuka, Sasha amekuwa mtu wa kujificha, akikwepa kukutana na watu ambao wanajua mkanda mzima wa simulizi yake ya kutunga.

Rais Kikwete azindua miradi ya maji na umeme Sengerema

0L7C0442Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Katika kijiji cha Katunguru/Nyamtelela wilayani Sengerema,Mkoani Mwanza leo.Kulia ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe. 0L7C0638Mwakilishi wa Serikali ya watu wa Marekani Bwana Karl Fickenscher akitoa hati ya kukabidhi mradi wa MCC I kwa waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati wa  hafla ya ufunguzi wa njia mpya za umeme kwenye mifumo ya kusambaza umeme mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika katika kijiji cha Bukokwa wilayani Sengerema,Mkoani Mwanza leo.Katikati akishuhudia ni Afisa mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge Account-(MCC)Tanzania Bwana Bernard Mchomvu. 0L7C0665Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utekelezaji wa mradi wa umeme wa MCC unaotekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Geita wakati wa  hafla ya ufunguzi wa njia mpya za umeme kwenye mifumo ya kusambaza umeme mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika katika kijiji cha Bukokwa wilyani Sengerema,Mkoani Mwanza leo.Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo. 0L7C0717Mwakilishi wa Millenium Challenge Account nchini Tanzania Bwana Karl Fickenscher akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua mradi wa njia mpya za umeme kwenye mifumo ya kusambazia umeme mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika katika kijiji cha Bukokwa,Wilayani Sengerema leo. Kushoto ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kulia ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo(picha na Freddy Maro)

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AZURU WILAYA YA SEGEREMA

IMG_1853Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu kutoka kwa chipukizi mara tu baada ya kuingia wilayani Sengerema kwa ziara ya siku moja tarehe 10.9.2013. IMG_1893Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Katunguru kilichoko wilayani Sengerema alipokwenda kijijini hapo kwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Katunguru/ Nyamtelela tarehe 10.9.2013. IMG_1930Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Katungulu/Nyamtelela utakaogharimu shs milioni 734 na utawanufaisha zaidi ya watu elfu kumi. IMG_1981Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Luchili akiwa njiani kwenda katika kijiji cha Bukokwa kuzindua rasmi mradi wa umeme tarehe 10.9.2013. IMG_2008Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini sherehe za uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliofanywa na Rais Kikwete huko Bukokwa wilayani Sengerema tarehe 10.9.2013. IMG_2032 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokea hati ya makabidhiano ya mradi wa umeme wa Bukokwa uliofadhiliwa na Millenium Challenge Co-operation ya Marekani. IMG_2082Rais Jakaya Kikwete akiangalia michoro inayoonyesha usambazaji wa umeme katika mkoa wa Mwanza. IMG_2090Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizindua rasmi mradi wa umeme wa Bukokwa tarehe 10.9.2013
PICHA NA JOHN LUKUWI

DIWANI WA TLP :SIASA SI UADUI, AMFAGILIA KINANA KWA BUSARA ZAKE

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na diwani wa TLP Ntabo Majabi kata ya MwendaKulima wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha afya kilichodhaminiwa na mgodi wa Buzwagi kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
……………….
Na Adam Mzee
DIWANI wa Kata Mwendakulima Ntabo Majabi kupitiaTanzania Labour Party (TLP), amesema Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhaman Kinana ni kiongozi mwenye busara na hekima kubwa na ndio maana Rais Jakaya Kikwete amemua kumpa nafasi hiyo kwa kuwa atakuwa anamjua vizuri.
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha afya katika eneo hilo, alisema amefurahishwa na aina ya siasa ambazo zinafanywa na Kinana na yeye binafsi ametambua kuwa Katibu Mkuu huyo wa CCM anaouwezo mkubwa wa kufanya kazi zake.
“Kinana wewe ni jembe, wakati unazungumza nilikuwa nimekaa mbali na kusikiliza lakini maelezo yako yamenifurahisha na ndio maana nimeamua kuja kukupa mkono.Kama nchi hii ingekuwa na makatibu wakuu wengi wa aina yako, tungepiga hatua hasa katika siasa za nchi hii.
“Pia niwaambie wananchi siasa si ugomvi, Kinana ameeleza vizuri, tunatakiwa kushirikiana ili kufanikisha malengo ya kuwatumikia wananchi.Nakupongeza mzee Kinana kwa maelezo yako yamenipa faraja licha ya kwamba mimi ni diwani kupitia TLP,”alisema.
Ndugu Kinana alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa CCM ndio yenye Serikali na diwani huyo licha ya kuwa TLP bado anatekeleza ilani ya CCM , hivyo wananchi nao wanatakiwa kutambua hakuna sababu ya kulumbana kwasababu tu ya mambo ya siasa.

HODGSON APUMUA INGAWA KAZI IPO, ATOKA 0-0 NA UKRAINE, MECHI DHIDI YA MONTENEGRO NA POLAND NDIO MAHAKAMA YAKE!!

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MENEJA wa Timu ya Taifa ya England, maarufu `Simba Watatu`, Roy Hodgson amepumua kidogo katika harakati zake za kuwania kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani nchini Brazi baada ya kutoka suluhu dhidi ya Ukraine jana usiku.
England iliingia uwanjani kupambana kwa nguvu bila ya nyota wake Wayne Mark Rooney, Dany Welbeck na Daniel Sturrage kutokana na sababu tofauti.
Sturrage na Rooney ni majeruhi, wakati Welbeck alikuwa anatumikia kadi aliyopewa mechi ya nyuma.
Juni 19, 2012, ilikuwa mara ya mwisho kwa England kushinda mechi ya ushindani, lakini si dhidi ya Moldova au San Marino bali Upinzani wa siku hiyo ulikuwa dhidi ya Ukraine, na toka hapo, England imeshakutana mara mbili na wakali hao na kushindwa kuibuka na ushindi.
England wamebakiwa na mechi dhidi ya Montenegro pamoja na Poland mwezi ujao na wanatakiwa kupata ushindi ili kukata tiketi ya  kcuheza fainali za kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Na mechi hizo watacheza katika dimba lao la Taifa la Wembley, hivyo kujipa matumaini ya kufanya vizuri.
Late drama: Frank Lampard heads one just past the post in second half stoppage timeDuuh!: Frank Lampard akipiga kichwa na kugonga mwamba dakika za majeruhi kipindi cha pili
Right place right time: Steven Gerrard nips in to stop Yarmolenko as Joe Hart gets ready to make a saveSehemu  na muda sahihi: Steven Gerrard akimdhibiti Yarmolenko huku Joe Hart akiwa tayari kuokoa
Centurion: Frank Lampard (left) gets a header on goal during his 100th capKapiga mechi ya 100: Frank Lampard (kushoto)  akipiga kichwa golini katika mechi yake ya 100
Deep in thought: Roy Hodgson looks to have a lot on his mind on the touchlineDimbwi la mawazo: Roy Hodgson akionekana kutoamini kinachoendeleaDesperate dive: Joe Hart flings himself across goal as Yevhen Konoplyanka's free kick is deflected wideKazi ya nguvu: Joe Hart akijaribu kuokoa mpira wa adhabu uliochongwa na Yevhen Konoplyanka
Kikosi cha Ukraine: Pyatov, Fedetskiy, Khacheridi, Kucher, Shevchuk, Stepanenko, Edmar, Gusev (Bezus 68), Yarmolenko (Khomchenovskiy 90), Konoplianka, Zozulya (Seleznyov 90). Subs: Koval, Dedechko, Tymoschuk, Mandzyuk, Grechyshkin, Morozyuk, Rakitskiy, Devic,
Khudzamov.
Kikosi cha England: Hart, Walker, Cahill, Jagielka, Cole, Lampard, Gerrard, Wilshere (Young 68), Walcott (Cleverley 89), Lambert, Milner. Subs: Ruddy, Smalling, Baines, Caulker, Carrick, Barkley, Defoe, Sterling, Townsend, Forster.

SADC yamuonya Kagame kuhusu mipango yake ya kuivamia Tanzania baada ya kuomba msaada wa kijeshi toka Kenya na Uganda

MZOZO wa kidiplomasia alioibua Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa Rais Jakaya Kikwete, sasa unaonekana kuchukua mwelekeo mpya, baada ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kumuonya kiongozi huyo kuacha mara moja fikra zozote mbaya dhidi ya Tanzania, MTANZANIA Jumatano limedokezwa. 



Habari za uhakika na za kuaminika kutoka miongoni mwa viongozi wa juu wa SADC na maofisa wa Serikali, waliokuwa katika ujumbe wa Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa akihudhuria Mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu huko Uganda hivi karibuni, zinaeleza kuwa tayari Jumuiya hiyo imekwisha mpatia ujumbe huo mmoja wa mawaziri aliyekuwa ameandamana na Kagame muda mfupi baada ya kikao chake na Kikwete.

Taarifa ambazo MTANZANIA Jumatano imezinasa, zinaeleza kuwa, kiongozi mmoja wa juu wa Msumbiji ambaye alikuwa pia Uganda, alikaririwa akimueleza Waziri huyo wa Kagame kuacha kabisa fikra za kuishambulia Tanzania, kwa sababu ya uamuzi wake wa kupeleka vikosi vyake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

“Uamuzi wa Tanzania na Afrika Kusini kupeleka majeshi DRC, ni msimamo wa pamoja wa SADC. Vitisho vyovyote dhidi ya Tanzania au uvamizi wa kijeshi, utachukuliwa ni uvamizi dhidi ya SADC, hivyo tutakuwa tayari kuingia vitani kupigana upande wa Tanzania,” alikaririwa akisema ofisa huyo wa juu wa Msumbiji.

Inaelezwa kuwa, SADC imetoa msimamo huo baada ya kubaini kuwa hasira ya sasa ya Kagame dhidi ya Rais Kikwete, msingi wake unatokana na hatua ya Tanzania kupeleka vikosi vyake nchini Kongo kwenda kupambana na vikundi vya waasi vikiwemo vile vinavyodaiwa kuwa na ushirika na majeshi ya Rwanda.

Taarifa hizi zinathibitishwa na habari ambazo gazeti hili ilizinasa jana kupitia gazeti la The Namibian la nchini Namibia, ambalo liliandika kuwa Jeshi la nchi hiyo (NDF), ambalo linaunda kikosi maalumu cha SADC, lilikuwa limeanza kushiriki mazoezi huko Jangwani karibu na Walvis Bay. Mazoezi hayo yatadumu hadi Oktoba 15 mwaka huu.

Inaelezwa kuwa wakati mazoezi hayo yakiendelea, Mkuu wa majeshi ya Namibia (NDF), Luteni Jenerali, Epafras Ndaitwah aliwakumbusha washiriki hao kuwa kwa sasa wanachama wenzao kama Wanajeshi wa Tanzania na Namibia, wanapambana na maadui wa amani Kongo na kwamba lazima wajiandae kwa hali yoyote ambayo haitabiriki.

Hatua hiyo ya sasa ya SADC, na sifa ambazo imepata kummwagia Rais Kikwete kwa namna alivyosimamia mizozo wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi, inaonyesha wazi jinsi Jumuiya hiyo ilivyotayari kuwa upande wa kiongozi huyo.

Kutokana na hilo, baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo wanasema kuwa si ajabu basi Kagame na Serikali yake wakawa wanafahamu msimamo huo wa SADC, ambao haujawekwa hadharani hasa kwa kuzingatia uamuzi wake wa kuungana na Uganda na Kenya katika usharika wao wa hivi karibuni.

Pia hatua ya nchi yake kusaini mkataba wa kiusalama na nchi nyingine tano wa kusaidiana kijeshi endapo mmoja wao atavamiwa na nchi nyingine, imeelezwa kuwa na mwelekeo huo huo wa Kagame kuanza kujihami.

Nchi ambazo zimeingia mkataba huo na Rwanda ni pamoja na Ethiopia, Kenya, Uganda na Sudan Kusini.

Hata hivyo wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo, wamekosoa muungano huo wa kusaidiana kijeshi na Rwanda, wakidai kuwa ni wa mashaka ukilinganisha na ule unaounda SADC ambao unajengwa na matendo ya kihistoria.

Wameitolea mfano Ethiopia, kwamba ni rahisi kuasi kutokana na mfumo wake wa kijeshi unaoongozwa kwa mkono wa chuma, huku wanajeshi wake wakiwa katika hali mbaya ya kiuchumi.

Wameulinganisha mfano huo na nchi moja tu ya Zimbambwe ambayo inaunda SADC kwamba, pamoja na matatizo yote ya migogoro ya kisiasa na kidiplomasia inayoyakabili, lakini jeshi lake lipo imara na linatunzwa vizuri.

Wakati wadadisi na wachambuzi wa mambo wakiwa na mtizamo huo, hatua ya sasa ya SADC imekuja wakati ambapo tayari Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma aliwahi kuionya Rwanda akisema kuwa endapo nchi hiyo itajaribu kuigusa Tanzania, atakuwa tayari hata peke yake kupeleka jeshi lake kupambana nchini humo.

Nje ya SADC, nchi zinazounda Jumuiya hiyo kama Afrika Kusini, Msumbiji, Zimbabwe, Namibia na Angola zinaguswa moja kwa moja na hisia za Tanzania, kutokana na historia yake ya kushiriki kwenye ukombozi na uhuru wa nchi hizo.

Kutokana na hilo, wachambuzi hao wanasema kuwa si rahisi kwa wao kukaa kando pale watakapoona maslahi ya Tanzania yanachezewa, hasa linapokuja suala la kuichokoza.

Taarifa hizo za SADC zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Marekani, Barack Obama, kuinyooshea kidole cha lawama Rwanda, kitendo hicho kinaonekana kuungwa mkono kwa kasi na makundi mengine ya kimataifa.

Kagame ambaye kwa miaka mingi amekuwa kiongozi kipenzi cha mataifa mengi tangu alipofanikiwa kumaliza mapigano yaliyosababisha mauaji ya halaiki nchini kwake mwaka 1994, katika siku za hivi karibuni taswira yake inaonekana kubadilika na kuchukua mwelekeo wa uadui zaidi kuliko urafiki.

Hilo linatokana na kile kinachodaiwa kuwa Serikali yake imekuwa ikihusika kuwasaidia waasi wa kundi la M23, wanaoendesha mapambano dhidi ya majeshi ya Serikali ya Kongo, jambo linalopingwa na Jumuiya ya Kimataifa pia wanatuhumiwa kwa ubakaji na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Tuhuma hizo ndizo ambazo zinamuweka Rais Kagame katika hatari na wingu la mashaka kwa sasa, hasa baada ya uhusiano wake na Tanzania kupita katika wakati mgumu kutokana na kuingia kwenye mgogoro na Rais Kikwete ambaye alimshauri kukaa meza moja ya mazungumzo na waasi wa FDLR.