Wednesday, September 11, 2013

NJEMBA YAMKUTA MAZITO

NJEMBA moja iliyojulikana kwa jina la Haji Bakari maarufu kama Mchome limekamatwa baada ya kudaiwa kutapeli kiasi cha shilingi 570,000 kwa njia ya simu za mkononi.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, njemba hilo lilifanikisha utapeli huo kwa kutumia majina ya watu wanaofahamiana na washirika kibiashara.

Kijana huyo aliomba pesa hizo kwa madai kuwa gari lake limemharibikia maeneo ya Chalinze mkoani Pwani hivyo alihitaji kiasi hicho ili aweze kulitengeneza. Bila hiyana, aliyeombwa alitoa fedha hizo kwa moyo mmoja ingawa kwa awamu mbili.

Akizungumza na gazeti hili, mtu aliyetapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la Godilizen Moshi alisema baada ya kumkamata mtu huyo, alijihami na kusema kuwa aliyefanya mchezo huo ni pacha wake.

Akisimulia mkasa huo, Moshi alidai: “Kijana huyu ni mzoefu na alikuwa…

Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'
NJEMBA moja iliyojulikana kwa jina la Haji Bakari maarufu kama Mchome limekamatwa baada ya kudaiwa kutapeli kiasi cha shilingi 570,000 kwa njia ya simu za mkononi.
Haji Bakari akipandishwa kwenye difenda.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, njemba hilo lilifanikisha utapeli huo kwa kutumia majina ya watu wanaofahamiana na washirika kibiashara.
Kijana huyo aliomba pesa hizo kwa madai kuwa gari lake limemharibikia maeneo ya Chalinze mkoani Pwani hivyo alihitaji kiasi hicho ili aweze kulitengeneza. Bila hiyana, aliyeombwa alitoa fedha hizo kwa moyo mmoja ingawa kwa awamu mbili.
...Akiwa ndani ya difenda.
Akizungumza na gazeti hili, mtu aliyetapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la Godilizen Moshi alisema baada ya kumkamata mtu huyo, alijihami na kusema kuwa aliyefanya mchezo huo ni pacha wake.
Akisimulia mkasa huo, Moshi alidai: “Kijana huyu ni mzoefu na alikuwa akitumia simu nambari 0655 301646, nilimuamini baada ya kunitajia jina la mtu ambaye nafahamiana na tunashirikiana kibiashara.”
Alisema baada ya kukamilisha kumpatia kiasi hicho cha fedha alizoomba alimpigia simu ili kuhakiki kama amezipata lakini ilipopokelewa, mpokeaji alisema alikuwa mazishini mkoani Kilimanjaro, kitu ambacho kilimshtua na kuhisi kutapeliwa.
Baada ya hapo, Moshi aliwataarifu ndugu zake na mara moja msako mkali dhidi ya tapeli huyo ukaanza.
“Nilipagawa baada ya kujibiwa kuwa niliyemtumia fedha yuko Kilimanjaro, jibu hilo lilinichanganya sana,” alisema Moshi.
Kwa mujibu wa Moshi, alitafuta watu wa kumsaidia kumkamata mtu huyo na hatua yao ya kwanza ilikuwa ni kwenda ofisi za mtandao wa Tigo zilizopo Mlimani City jijini Dar ili kujua sehemu halisi alipo tapeli huyo.
Baada ya kueleza tatizo lao, mfanyakazi wa kampuni hiyo aliwaeleza kuwa mtu mwenye namba hiyo anapatikana eneo la Ubungo Kibangu, jijini Dar es Salaam.
“Na kweli tulipoenda Kibangu tukiwa na wenyeji wa huko tulifanikiwa kumpata kirahisi sana na kumchukua, kutokana na kibano alichopewa alisema sio yeye aliyetapeli bali ni pacha wake,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa amekamatwa. “Tunamchunguza kabla ya kumfikisha kortini,” alisema.

0 comments: