This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, July 17, 2013

Airtel na UNESCO kuzindua radio jamii Karagwe Bukoba

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO wanatarajia kuzindua radio jamii katika wilaya ya Karagwe mkoani Bukoba mwishoni mwa wiki hii
 
 
 
 
Uzinduzi huo unafatia ushirikiano kati ya Airtel na UNESCO katika mradi wa kusadia jamii na kufikisha mawasiliano ya radio sehemu ambazo zina changamoto za huduma za mawasiliano ya radio
 
Akiongea kuhusu uzinduzi huo ya Airtel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema  “ Mradi huu wa radio za jamii tunaufanya kwa kushirikiana na UNESCO kwa lengo la kuendeleza na kuboresha huduma za mawasiliano na kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani wa maeneo ya vijijini.
 
Tumejipanga kufanya uzinduzi wa ushirikiano wetu na UNESCO na Radio ya FADECO Karagwe utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 19 julai 2013
 
Mgeni rasmi atakuwa ni mkuu wa mkoa wa Bukoba LutenFabian Masawe , pamoja na yeye tutakuwa na viongozi mbalimbali wa serikali watakaohuduria sherehe za uzinduzi huo
 
Tunaamii kwa kupitia radio hizi jamii itabadilika na kupata elimu zitakazosaidia kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wananchi wengi wana pata habari mbalimbali zikiwemo za kibiashara, uchumi, kijamii na kisiasa.
 
Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin alisema “tunayo miradi mingi ya kusaidia jamii kujikwamua na hali ngumu za uchumi, kupata elimu bora, uongozi bora , kuachana na mila potofu na mengine mengi.  kwa kupitia mradi huu wa Radio tunaoshirikiana na wenzetu wa Airtel tumeshaona matunda na mafanikio mengi mpaka sasa, lengo letu ni kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo za kuwapata wananchi habari za ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha na sehemu nyingine za nchi na Dunia.
 
Akiongea kuhusu uzinduzi wa Radio jamii Karagwe Mkurugenzi wa Radio ya FADECO Bw Joseph Sekiku alisema “Mpaka sasa vifaa na mitambo ya mawasiliano ya kisasa imeshafungwa na tuko katika hatua ya majaribio ambapo tumeshuhudia ufanisi mkubwa zaidi kulinganisha na awali kwani tumeweza kutanua wigo na kufikia vijiji vingi zaidi”.
 
nawashukuru sana Airtel na UNESCO kwa kutufikia na kuwawezesha kuendesha radio yetu kwa ufanisi zaidi. Radio ya FADECO ilizinduliwa toka mwaka 2007  na kuanza  kurusha matangazo yetu rasmi kwa vijiji vya karibu, changamoto tuliyokuwa nayo ni pamoja na kurusha matangazo yetu katika vijiji vilivyo mbali zaidi kutoka hapa radioni. Kwa kupitia mradi huu tumeweaza kuona mfanikio makubwa tayari, 
 
“Tunagemea kuzindua rasmi ushirikiano wetu na UNESCO pamoja na Airtel siku Ijumaa hapa Karagwe. Nachukua fulsa kuwaalika wananchi wadau wa sekta za mawasiliano, viongozi mbalimbali kuhudhuria halfa hii ya uzinduzi na kusherehekea pamoja nasi mafanikio haya” aliongeza Sekiku
 
Mradi wa radio jamii umeanzishwa mwaka jana 2012 radio zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi zitafaidika na mradi huu kama ilivyo katika Radio hii ya FADECO iliyopo wilaya ya Karagwe Bukoba

WANAJESHI 7 WALIOUAWA DARFUR FULL STORY

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA imeingia kwenye majonzi mazito baada ya wanajeshi wake 7 kuuawa na waasi wa Jimbo la Darfur nchini Sudan inayoongozwa na Rais Omary Bashir walipokuwa katika kazi ya ulinzi wa amani nchini humo.
Imam akiongoza sala ya kuaga miili ya wanajeshi waliouawa Darfur nchini Sudan.
Pamoja na tukio hilo la kusikitisha, Risasi Mchanganyiko limechimba kwa undani na kuibuka na ‘full story’ ya kilichotokea siku ya tukio na kusababisha…
Na Mwandishi Wetu
TANZANIA imeingia kwenye majonzi mazito baada ya wanajeshi wake 7 kuuawa na waasi wa Jimbo la Darfur nchini Sudan inayoongozwa na Rais Omary Bashir walipokuwa katika kazi ya ulinzi wa amani nchini humo.
Imam akiongoza sala ya kuaga miili ya wanajeshi waliouawa Darfur nchini Sudan.
Pamoja na tukio hilo la kusikitisha, Risasi Mchanganyiko limechimba kwa undani na kuibuka na ‘full story’ ya kilichotokea siku ya tukio na kusababisha wanajeshi hao kuuawa.
Kiongozi wa Kanisa naye akiongoza sala ya kuaga miili ya wanajeshi hao.
HABARI KAMILI
Habari za uhakika kutoka kwa chanzo cha kuaminika, wanajeshi wa Tanzania walikuwa wakiusindikiza msafara wa amani wa Umoja wa Mataifa (UN) uliokuwa ukitokea eneo la Khor Abeche kwenda Nyara Darfur na kushambuliwa na waasi hao.
Msemaji wa Jeshi la Tanzania, Kapambala Mgawe.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kabla ya shambulio hilo, lililowaondoa duniani wanajeshi hao, inadaiwa kwamba mmoja wa wanajeshi wa Tanzania alitekwa na waasi hao ambao walikuwa na nia ya kutaka kumshikilia na kutoa vitisho kwa dunia kuondoa majeshi yanayolinda amani nchini humo.
Inadaiwa kuwa wanajeshi wa Tanzania walihamaki na kujaribu kutoa msaada wa kumuokoa mwenzao ndipo lilipotokea shambulio hilo ambalo pia limesababisha wanajeshi wengine 14 kupatwa na majeraha.
Rais Jakaya Kikwete.
KUMBE WANGEFANYA HIVI…
Wanajeshi hao wa Tanzania wameuawa wakiwa wanapigania amani na kutii kifungu cha 6 cha sheria cha majeshi ya kulinda amani duniani ambacho kinapiga marufuku wanajeshi kujibishana kwa silaha na waasi.
Wanachotakiwa kufanya ni kukimbia au kujilinda kwa kujihami bila ya kuleta madhara kwa upande wa pili vinginevyo wasingekufa kama wasingeitii sheria hiyo.

TANZANIA YALIA NA KIFUNGU NA.6
Akizungumza na waandishi wa habari nchini mwishoni mwa wiki iliyopita, Msemaji wa Jeshi la Tanzania, Kapambala Mgawe alisema Tanzania inatarajia kufanya mazungumzo na Umoja wa Mataifa (UN) ili kuomba kifungu hicho namba 6 kinachowakataza wanajeshi wanaolinda amani kujibu mapigo kiondolewe.
Rais wa Sudan Omar Hassan Ahmad Al-Bashir.
VILIO KILA KONA
Pamoja na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuwalilia wanajeshi hao, vilio vimetawala kila kona ya nchi.

HEBU ONA
Kutokana na asili ya majina ya wanajeshi hao, kila pembe ya nchi inaweza kuguswa kwa njia moja ama nyingine na vifo hivyo;
Sajenti Shaibu Othuman na Koplo Mohammed Juma, hawa wanawakilisha vilio upande wa Pwani ya Tanzania kuanzia Zanzibar hadi Kusini mwa Tanzania kwenye Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Wengine ni Koplo Oswald Chaula na Pte. (Private) Rodney Ndunguru, hawa wanawakilisha Nyanda za Juu Kusini  katika Mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma.
Wakati marehemu Pte. Peter Werema anawakilisha Kanda ya Ziwa hususan katika Mkoa wa Mara ambao sambamba na mikoa mingine ya jirani nao wameguswa na msiba huo.
Kilio hicho kimesambaa hadi katika mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania ikiwemo Arusha na Kilimanjaro kutokana na kifo cha Pte. Fortunatus Msofe .
Aidha, mwanajeshi mwingine Koplo Mohammed Chikilizo naye amesababisha vilio katika mikoa ya Pwani.

FRANK ATISHIWA KUUAWA

Na Mwaija Salum

MSANII wa Filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi ‘Frank’ amedai kutishiwa kuuawa baada ya kupokea ujumbe mfupi wa meneno ‘sms’ kutoka kwa mtu anayekulikana kwa majina ya Jonathan Lyradu.
 Mohammed Mwikongi ‘Frank’.
Frank amesema alianza kupokea meseji hizo tangu mwezi uliopita ambapo Lyradu amekuwa akimtishia kusitisha pumzi yake hapa duniani.

“Mara ya kwanza nilijua amekosea namba, nikamuuliza anamuhitaji nani, lakini akanitumia meseji nyingine na kunitaja jina langu huku akiendelea kunitisha na…
Na Mwaija Salum
MSANII wa Filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi ‘Frank’ amedai kutishiwa kuuawa baada ya kupokea ujumbe mfupi wa meneno ‘sms’ kutoka kwa mtu anayekulikana kwa majina ya Jonathan Lyradu.
Mohammed Mwikongi ‘Frank’.
Frank amesema alianza kupokea meseji hizo tangu mwezi uliopita ambapo Lyradu amekuwa akimtishia kusitisha pumzi yake hapa duniani.
“Mara ya kwanza nilijua amekosea namba, nikamuuliza anamuhitaji nani, lakini akanitumia meseji nyingine na kunitaja jina langu huku akiendelea kunitisha na kunimwagia mvua ya matusi kwa kweli nilimshangaa kwani simjui mtu huyo,” alisema Frank.
Msanii huyo alisema ametoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi Tabata na kufungua jalada TBK/RB/2750/13 TAARIFA.
Katika utafiti wa awali uliofanywa na polisi wakati wa kumsaka mtu huyo anayemtishia maisha Frank anaonekana katika mitandao kuwa ni mkazi wa maeneo ya Magomeni, Sinza na Bamaga, Mwenge jijini Dar.

DIAMOND AFUTURU NA KIMADA!

Na Musa Mateja

HIVI karibuni mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa akifuturu na hawara yake, Penniel Mungilwa ‘Penny’, kitendo ambacho kimewashangaza wengi na baadhi kufikia hatua ya kumponda kuwa anakwenda kinyume na Uislam.
 Tukio hilo lilijiri nyumbani kwa Diamond maeneo ya Sinza- Mori jijini Dar ambapo mbali na mastaa hao, pia walikuwepo waumini wengine wa dini hiyo walioalikwa katika chakula hicho kitakatifu.…

Na Musa Mateja
HIVI karibuni mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa akifuturu na hawara yake, Penniel Mungilwa ‘Penny’, kitendo ambacho kimewashangaza wengi na baadhi kufikia hatua ya kumponda kuwa anakwenda kinyume na Uislam.
Tukio hilo lilijiri nyumbani kwa Diamond maeneo ya Sinza- Mori jijini Dar ambapo mbali na mastaa hao, pia walikuwepo waumini wengine wa dini hiyo walioalikwa katika chakula hicho kitakatifu.
Waumini wamponda
Wakizungumza na gazeti hili mara baada ya kumuona Penny ambaye ni demu wa Diamond akiwa eneo hilo, baadhi ya waumini walisema walishangazwa na uwepo wake kwani sheria ya dini ya Kiislam hairuhusu kuwa karibu na kimada hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Walisema, Diamond hatakiwi kuwa karibu na Penny si kwa kipindi hiki tu bali hata baada, mpaka pale ambapo atatoa mahari na kuozeshwa kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislam.

“Huyu kijana kafanya jambo zuri la kuwafuturisha wenzake ila amekosea kumualika yule mwanamke wake, yule kwake ni kimada na kwa sheria za dini yetu huruhusiwi kabisa kumkaribia, sasa ona wanafuturu pamoja na wanashikanashikana, ile siyo sawa,” alisema muumini mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Muft Simba
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Swaleh alisema: “Diamond anatakiwa aambiwe kuwa anafanya makosa sana kuwa karibu na yule Penny.
“Kihalali kwanza anatakiwa amsilimishe kisha amlipie mahari ndipo amuoe lakini kinyume na hapo atakuwa anaishi na hawara na kuwa naye karibu ni kujichumia dhambi anazoweza kuziepuka.”
Maalim Hussein
Mashehe nao wacharuka
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya mashehe wenye heshima kubwa Tanzania nao walionesha kukerwa na kitendo alichokifanya Diamond na kusema kinakiuka maadili ya dini yao.
Walisema, mwanamke ambaye hajaolewa anayeishi au kuwa karibu na mwanaume na wakati mwingine kuzini, huyo ni kimada na hana nafasi kwenye Uislam.
Shekh Alhadi Mussa
Shehe Khamisi Mataka
Huyu ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mashehe na Wanazuoni Tanzania anasema: “Lengo la swaumu ni kumfanya mtu kuwa Mchamungu na Mchamungu ni yule anayefanya yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha aliyokatazwa.
“Katika Uislam kuwa na hawara inakatazwa, si kwa kipindi hiki tu cha Mwezi Mtukufu bali hata baada. Kwa hiyo kufuturu na hawara ni kinyume na Uislam na unapata dhambi.”
Shekh Mataka
Maalim Hassan Yahya
Ni Mnajimu maarufu nchini. Yeye anasema kuwa, hawara hakubaliki kidini hivyo hatakiwi kupika futari wala kuwa naye karibu kwa namna yoyote, kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za funga na maadili ya Uislam.

Shekh Alhad Musa Salum
Huyu ni Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kuhusiana na hili la Diamond la kufuturu na Penny anasema kuwa, uhawara hauruhusiwi katika Uislam na wanaoendekeza hilo waache mara moja ili waweze kupata radhi za Mwenyezi Mungu.
Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban Simba hivi karibuni aliwasihi Waislam kutimiza nguzo hiyo muhimu ya Uislam na kuwataka wahakikishe wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa ili waweze kufikia lengo la kufunga.

WANAJESHI 7 WALIOUAWA DARFUR FULL STORY

DROO YA KWANZA YA AIRTEL YATOSHA YAFANYIKA

Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw. Jackson Mmbando akionyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) jinsi droo ya Airtel Yatosha inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw. Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi. Aneth Muga wa kwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya washindi 7ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.…

Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw. Jackson Mmbando akionyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) jinsi droo ya Airtel Yatosha inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw. Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi. Aneth Muga wa kwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya washindi 7ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.
Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw. Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wa promosheni ya Airtel yatosha mara baada ya kuibuka mshindi katika droo ya wiki ya kwanza inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw. Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi. Aneth Muga wa kwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya washindi 7 ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.