This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, April 18, 2013

SEKESEKE! MH! MKE AMSHUSHIA KIPIGO MUMEWE BAR

Stori:Mwandishi Wetu
Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni alizua sekeseke la aina yake baada ya kumvaa mwanaume anayedaiwa ni mume wake na kumshushia kichapo.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Baa ya Corner iliyopo Afrikasana, Sinza jijini Dar ambapo inadaiwa chanzo cha vurumai hilo ni mwanaume huyo kutoonekana nyumbani.
Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio hilo kilitutonya kuwa, awali mwanamke huyo alitinga katika kiwanja hicho cha kujidai asubuhi na mapema huku akionekana kuangazaangaza huku na kule kabla ya kukutana na…

Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio hilo kilitutonya kuwa, awali mwanamke huyo alitinga katika kiwanja hicho cha kujidai asubuhi na mapema huku akionekana kuangazaangaza huku na kule kabla ya kukutana na bwana wake huyo na kuanza kuzozana.
“Yule mwanamke alipofika hapa alionekana alikuja kishari na hata alivyokuwa akiongea na yule bwana wake tulibashiri kutokea kwa ugomvi.
“Kweli… haukupita muda mrefu tukaona wakianza kukunjana, mara mwanamke akapandwa na hasira na ndipo sekeseke la aina yake likatokea,” kilidai chanzo hicho.
Ikaelezwa kuwa kutokana na jinsi walivyokuwa wakitifuana, wasamaria wema waliingilia kati na kuwataka wayamalize badala ya kuwapa faida watu.
Kufuatia ushauri huo, wawili hao waliachiana na mwanamke akaanza kulia kisha akamlalia mwanaume huyo kifuani, wakabembelezana na kuondoka eneo hilo. 

PONGEZI: H. BABA AINGIZA SOKONI PIPI ZENYE JINA LAKE

H. Baba akionesha pipi zake.

Katika kuonesha kwamba bado ana kiu ya kuona sanaa yake inapanuka  na kuvuma mbali huku akiboresha maisha yake, kukuza kipato na kuongeza ufanisi , msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini H. Baba ameamua kujikita katika biashara kwa style ya kipekee  kwa kuingiza sokoni bidhaa aina ya pipi zenye jina, picha na chata zake, pipi zinazojulikana kwa jina la "H. BABA & FLORA MAPENZI KWA WATOTO".



 Pipi hizo zilizopambwa kwa picha ya H. Baba katika karatasi ya kuishika pipi, zikipambwa na mfuko wa nylon wenye uzito wa gram 250 uliona picha ya mwanamuziki H. Baba na mwigizaji wa Bongo movie Flora Mvungi  na  zinazo tengenezwa na kampuni ya TANFRIK LIMITED ya Nairobi nchini Kenya, tayari zimeanza kuuzwa kwenye baadhi ya maduka na vibanda mbalimbali vya biashara kanda ya ziwa.
Muonekano wa mbele.
Muonekano wa nyuma.

HUKUMU YA SHEIKH PONDA YAKUMBWA NA MIZENGWE LEO

HUKUMU ya Kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya maandamano haramu imeahirishwa mpaka tarehe 9 mei mwaka huu.
Kesi hiyo imeharishwa baada ya Hakimu  Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa ,kutokuwepo Mahakamani hapo.
Awali hakimu huyo alitarajiwa kuketi katika kiti cha enzi na kutoa hukumu ya kesi hiyo Na.245/2012 inayomkabili Ponda na wenzake. 
Aprili 3 mwaka huu:Mawakili wa upande wa Jamhuri ,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi Juma Nassor na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa njia ya maandishi ambapo mawakili wa upande wa jamhuri waliiomba mahakama iwaone washitakiwa wote wana hatia na wapewe adhabu kwa mujibu wa sheria.
Wakati mawakili wa utetezi waliiomba mahakama iwaone washitakiwa hawana hatia na iwaachilie huru kwa sababu hawakutenda makosa yanayowakabili na kwamba upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yao.

MILIONI 2 (2 000,000) ZATOLEWA NA SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA BI KIDUDE

Mhe. rais wa zanzibar Dr Shein na viongozi wengine wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya marehemu Bi Kidue kabla ya kuhifadhiwa kwenye jeneza.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika dua ya pamoja kumuombea Gwiji la sanaa Zanzibar Bi. Fatma Binti Baraka (Bi. Kidude) nyumbani kwake Rahaelo nyuma ya Studio ya ZBC Redio.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na baadhi ya Familia ya Bi. Kidude wakati alipofika kutoa mkono wa pole kwa ndugu na jamaa wa msanii huyo. Kushoto kwa Balozi  ni Ndg. Haji Ramadhani Suwed na kulia ni Bw. Abdullrahman Saleh.
Umati mkubwa wa Wananchi walioshiriki mazishi ya Msanii Gwiji wa sanaa kanda ya Afrika Mashariki na Mipaka yake  Bi. Fatma Binti Baraka (Bi Kidude) nyumbani kwake Rahaleo nyuma ya Studio ya ZBC Redio.
 Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakiendelea na dua ya kumuombea msanii Gwiji wa Taarab Bi. Fatma Binti Baraka ( Bi Kidude) nyumbani kwake Rahaleo.
------------
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kugharamia mazishi ya Gwigi la Sanaa ndani ya ukanda wa Afrika ya Mashariki na mipaka yake Anti Fatma Binti Baraka (Maarufu Bi. Kidule) aliyefariki dunia jana mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu.
 
Hatua hiyo imekuja kufuatia  mchango wake katika kuitangaza sanaa ya Zanzibar nje ya mipaka ya Tanzania hasa kwenye  fani ya muziki wa Taarabu asilia na ile ngoma maarufu ya Unyago inayotumika katika sherehe za harusi.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akiifariji familia ya Marehemu Bi. Kidude wakati wa matayarisho ya mazishi yake eneo la Rahaleo nyuma ya Kituo cha ZBC Redio Rahaleo Mjini Zanzibar.
 
Balozi Seif akitoa ubani wa shilingi Milioni (2,000,000/- )kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa familia ya marehemu amesema jamii na waswahili wote katika mwambao wa Afrika Mashariki wanafahamu mchango mkubwa wa Msanii Bi. Kidude  katika fani ya muziki wa taarabu.
 
Amesema Zanzibar imepata sifa kubwa katika Nyanja za Kimataifa kutokana na mchango wa wasanii kwa kueneza sanaa ya Taarabu iliyotoa  fursa kwa baadhi ya watalii na wataalamu kuvitembelea Visiwa vya Zanzibar.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameitaka Familia ya Msanii Bi. Kidude kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha msiba na kuwaeleza kwamba msiba huo sio wao peke yao.
 
Balozi Seif amesema kwa kweli sisi sote tulimpenda sana Bi. Fatma Binti Baraka (Kidude) lakini tuelewe kwamba Mwenyezi Mungu amempenda zaidi na ndio maana akamuhitaji.
 
Naye Mmoja wa wana Familia hiyo Bw. Haji Ramadhan Suwed Buda kwa niaba ya Familia ya Marehemu Bi. Kidude ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango wake wa kuungana nao katika msiba huo.
 
Bw. Haji amesema hatua hiyo ya Serikali imeleta faraja kwao na kupunguza machungu ya msiba huo.
 
Msanii Gwiji wa sanaa ya Taarab asilia na ngoma ya Unyago Marehemu Bi. Kidude aliyekadiriwa kufikia umri wa zaidi ya miaka 98 hakuwahi kuolewa wala kupata Mtoto.
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Bi. Kidude mahali pema peponi – Amin.

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MAZISHI YA BI KIDUDE LEO MCHANA....




Picha za mazishi ya Bi. Kidude. Viongozi wa serikali kama rais Jakaya Kikwete, rais wa Zanzibar Ali sheni, makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar maalim Seif Sharif Hamad, na wasanii kama Mzee Yusuf, Diamond Platnumz, nk walikua miongoni mwa wahudhuriaji katika kumsindikiza gwiji huyo wa Taarabu katika safari yake ya mwisho.