Stori:Mwandishi Wetu
Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi
karibuni alizua sekeseke la aina yake baada ya kumvaa mwanaume
anayedaiwa ni mume wake na kumshushia kichapo.
Tukio hilo la
aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Baa ya Corner
iliyopo Afrikasana, Sinza jijini Dar ambapo inadaiwa chanzo cha vurumai
hilo ni mwanaume huyo kutoonekana nyumbani.
Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio hilo kilitutonya kuwa, awali
mwanamke huyo alitinga katika kiwanja hicho cha kujidai asubuhi na
mapema huku akionekana kuangazaangaza huku na kule kabla ya kukutana na…
Chanzo
chetu kilichokuwa eneo la tukio hilo kilitutonya kuwa, awali mwanamke
huyo alitinga katika kiwanja hicho cha kujidai asubuhi na mapema huku
akionekana kuangazaangaza huku na kule kabla ya kukutana na bwana wake
huyo na kuanza kuzozana.
“Yule mwanamke alipofika hapa alionekana
alikuja kishari na hata alivyokuwa akiongea na yule bwana wake
tulibashiri kutokea kwa ugomvi.
“Kweli…
haukupita muda mrefu tukaona wakianza kukunjana, mara mwanamke
akapandwa na hasira na ndipo sekeseke la aina yake likatokea,” kilidai
chanzo hicho.
Ikaelezwa
kuwa kutokana na jinsi walivyokuwa wakitifuana, wasamaria wema
waliingilia kati na kuwataka wayamalize badala ya kuwapa faida watu.
Kufuatia ushauri huo, wawili hao waliachiana na mwanamke akaanza kulia
kisha akamlalia mwanaume huyo kifuani, wakabembelezana na kuondoka eneo
hilo.
Thursday, April 18, 2013
Home »
» SEKESEKE! MH! MKE AMSHUSHIA KIPIGO MUMEWE BAR
0 comments:
Post a Comment