This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, July 7, 2013

BONGO FLEVA WAICHAPA BONGO MUVI KWA PENALTI 2-1



Nahodha wa Bongo Fleva, Hamis Baba 'H Baba' akipokea kombe kutoka kwa Mhe. William Ngeleja.
Bongo Fleva wakisherehekea ushindi wao.
Bongo Muvi…
Nahodha wa Bongo Fleva, Hamis Baba 'H Baba' akipokea kombe kutoka kwa Mhe. William Ngeleja.
Bongo Fleva wakisherehekea ushindi wao.
Bongo Muvi baada ya kichapo.
Timu ya Bongo Fleva imeibuka kidedea kwa kuichapa Bongo Muvi mabao 3-2 katika mchezo wao wa leo kwenye Tamasha la Matumaini 2013. Mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa mabao yalikuwa 1-1 ndipo zikaamriwa penalti na Bongo Fleva kuibuka kifua mbele kwa penalti 2-1.

ANGA WAILAZA SIMBA KWA PENATI 4-3, WATWAA KOMBE

Wachezaji wa Yanga (wabunge) wakishangilia na kombe lao.
Wachezaji wa Yanga (wabunge) wakishangilia baada ya kuwalaza watani wao Simba (Wabunge) kwa penati…
Wachezaji wa Yanga (wabunge) wakishangilia na kombe lao.
Wachezaji wa Yanga (wabunge) wakishangilia baada ya kuwalaza watani wao

LOWASSA APONGEZWA NA BAKWATA KWA KUVISHWA JOHO MAALUMU.....MILIONI 590 ZACHANGISHWA KATIKA HARAMBEE



Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akipongezwa na kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawi kwa kumvika joho la kilemba  baada ya kufanikisha harambee kwa ajili ya Kituo cha Redio Ikra kinachomilikiwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza. 


Anayeshuhudia ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Salum Hassan Fereji. 


Katika harambee hiyo zaidi ya sh. mil. 590 zilipatikana na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. mil 500. 




WAZIRI Mkuu mstaafu  Mhe.Edward Lowassa ijumaa usiku aliongoza harambee kubwa  na ya kihistoria ya kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.



Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na marafiki zake, wafanyabiashara, taasisi na  makampuni mbalimbali, watu binafisi na viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma wawakilishi wao hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 590 zikiwemo ahadi.
















UMATI WA WATU WALIOJITOKEZA KATIKA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI


 
 

MWANACHUO WA MWAKA WA KWANZA ALAANI KITENDO CHA KUPIGWA "EXILE" NA MADENTI WENZIE


Vitendo  vya  wanafunzi  kupigana  exile( kumpisha room ili angonoke na mpenzi wake)   vimekuwa  vikishika  kasi  ya  ajabu  katika  hosteli  za  wanafunzi  wa  vyuo  vikuu  mbalimbali ambao  kwao  limekuwa  ni  jambo  la  kawaida...!!

Hali  imekuwa  ni tofauti  kidogo  kwa  mwanafunzi  wa  chuo kimoja  hapa  nchini  ambaye  yuko  mwaka  wa  kwanza na anategemea kuingia mwaka wa pili.


Akiongea  na  mtandao  huu  kwa  sharti  la  kutotajwa  jina , mwanafunzi  huyo  amefunguka  na kudai  kuwa  Exile  imemuathiri  sana  kisaikolojia.Imemfanya  aishi  kama  mtumwa  huku  taaluma  yake  ikiyumba  kwa  kasi.

Hili  ni   simulizi  la  mwanafunzi  huyo:
 
"Maisha ya shule yana changamoto  nyingi sana.Kwa  mtu  yeyote  ambaye  ni  mcha  mungu  ni  lazima  itamuwia  vigumu  sana  kukabiliana  na  hali hii.

"Nasema  hivi  kwa  sababu  ndani  ya  hosteli  huwa  tunaishi  watu   tofauti  wenye malezi  tofauti.Kasheshe  ni  kwetu  sisi  first  year...

"Mazingira  kwetu  ni  mageni  na  ndani  ya  hosteli  tunaishi  na  mabraza  wa  miaka  ya  juu  wenye  wapenzi  wao  hapo hapo chuoni ambao  huwaleta  vyumbani   na  wakati mwngine  hulala  nao.

"Wanapokuja  na  wapenzi  wao  vyumbani  ni  lazima  uwapishe  wafanye  mambo  yao.Na  ukiwapisha  maana  yake  utoke  kwa  zaidi  ya  masaa  matatu  mpaka   matano

"Ndani  ya  chumba  changu  tulikuwa  tunaishi  watatu, mmoja  mwaka  wa  pili, mwingine  wa  tatu  na  mimi  mwaka wa kwanza.Wote  hao  walikuwa  na  wapenzi  wao  hapo hapo  chuoni.

"Siku  zote  za  wikiendi  walikuwa  wamezigawana.Mmmoja  ilikuwa  ni  jumamosi  na  mwingine  jumapili.Yaani  kwa  kifupi  ni  kwamba  sikuwa  na  uhuru wa  kukaa  chumbani   siku za wikiendi  na  wakati  mwingine  hata  siku  za  wiki.

"Nimeamua  niwe  muwazi  maana hali  hii  imekuwa  ni  kero  kwangu   na  imekuwa  ikiniathiri  sana  kisaikilojia  na  kusababisha  taaluma  yangu  iyumbe  nikilinganisha  na  nilipokuwa  naanza.

"Naomba  nitoe  ombi  kwa  wanafunzi wenzangu.Sote  tuko  vyuoni  kutafuta  maisha  na  zile  hosteli  tunazilipia  kwa  gharama  sawa.Kwa  nini  umsumbue  mwenzako  wakati  gesti  zipo?..Yangu  ni  hayo  tu"

LEO NDIO LE


JACOB STEVEN (JB).
HALIMA MDEE.
PATRICK AMOTE (KENYA).…JACOB STEVEN (JB).
HALIMA MDEE.
PATRICK AMOTE (KENYA).
ESTER BULAYA.
VINCENT KIGOSI 'RAY'.
SHADRACK MUCHANJE (KENYA).
THOMAS MASHALI.
AUNT EZEKIEL.
IDD AZZAN.
FRANCIS MIYEYUSHO.
JACQUELINE WOLER.
ZITTO KABWE.
PICHANI JUU NI TASWIRA ZA WATAKAOPANDA ULINGONI KUZIPIGA KATIKA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI 2013 LITAKALOFANYIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO JUMAPILI. USIKOSE!

BASI LA SUMMRY LAUA WATU 9 NA KUJERUHI 53



Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni na kuua watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu.


Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi


Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.
 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa  jina la Ntungu


Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko,  dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana ...

 
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.