Wednesday, March 20, 2013

RC KANALI MSTAAFU ISSA MACHIBYA AYATAKA MAKAMPUNI YA SIMU KUDHIBITI VITENDO VYA UHALIFU KUIPITIA SIMU ZA MKONONI

kikwete 1316Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akifungua mkutano wa wadau wa Mawasiliano ulioandaliwa na TCRA mkoani humo kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazokabili sekta hiyo jana kikwete 1319
                         Wadau  mbalimbali Mawasiliano wakiwa katika mkutano huo
Na Mwandishi wetu,Kigoma
Mkuu wa mkoa kigoma Issa Machibya amezitaka kampuni za simu za mkononi kuweka udhibiti wa kutosha kwa mitandao yao ya simu ili kuzuia vitendo vya utapeli na uhalifu ambavyo vimechangiwa na simu hizo. Akifungua kikao cha
siku moja cha wadau wa mawasiliano leo kilichoitishwa na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) Machibya alisema kuwa mitandao ya simu imekuwa ikitumika sana kwa sasa katika kufanyia utapeli lakini juhudi za kuwakamata wahusika hazizai matunda.
 Alisema kuwa moja ya sababu za kushindwa kukamatwa kwa wahalifu hao ni pamoja na kusajili kwa kutumia majina bandia jambo ambalo amesema linaviwia vigumu vyombo vya usalama kuwamakata wahusika waliojiandikisha kwa majina bandia.
 Ili kufanikisha kuhakikisha mwenye simu ndiye mwenye jina halisi amezitaka kampuni za simu kuhakikisha kwamba mawakala wao wanaohuza laini za simu wanapata vitambulisho sahihi vya wahusika na kutokubali kusajili namba ya simu kam muhusika hana kitambulisho.
 Akizungumzia kuhusu kuanza kwa matumizi ya teknolojia ya digitali kutoka analojia Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wananchi wanapaswa kukubaliana na mabadiliko ya teknolojia kwani jambo hilo si la Tanzania peke yake bali ni suala la kidunia.
 Alisema kuwa jambo kubwa ambalo linapaswa klufanywa kwa sasa ni kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa mfumo huo na kuona namna gani serikali na wadau mbalimbali wanashirikiana kuhakikisha wananchi wanatumia teknolojia hiyo kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake Meneja mipango na utafiti wa mamlaka ya mwasiliano nchini (TCRA), Ally Simba alisema kuwa moja ya kazi za mamlaka ni kuhakikisha teknolojia mbalimbali zilizochini ya mamlaka hizo zinatumika bila kuleta athari kwa jamii na kwamba kutokana na hilo wanatarajia kukaa tena na wadau mbalimbali katika kuangalia suala la udhibiti wa simu za mkononi zisitumike vibaya.

0 comments: