Mwenyekiti wa MANET Bw Zuberi Mwachura kulia akieleza mkakati wa kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya taifa ya Ruaha leo |
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akifafanua jambo |
……………….
Na Francis Godwin Blog, Iringa
MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema), Mchungaji Peter Msigwa amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa mkakati wake wa kunusuru vitendo vya ujangili katika hifadhi za Taifa.
MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema), Mchungaji Peter Msigwa amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa mkakati wake wa kunusuru vitendo vya ujangili katika hifadhi za Taifa.
Huku mbunge huyo akidai kuwa anawajua viongozi mbali mbali na watu
maarufu ambao wanaendelea kuendesha vitendo vya ujangili katika
hifadhi ya Ruaha Iringa ikiwa ni pamoja na kulitumia gari la
wagonjwa (Ambulence) kusafirisha meno ya tembo na atawataja wahusika
bungeni.
Msigwa ambae ni waziri
kivuli wa wizara ya maliasili na utalii alitoa pongezi hizo leo
mjini Iringa wakati wakati akifungua kikao cha kujadili vitendo vya
ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa iliyoandaliwa na
taasisi isiyo ya kiserikali ya Mazingira Netwark Tanzania (MANET).
“Awali ya yote napenda
kumshukuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa kuja na mikakati ya kweli ya
kupambana na vitendo vya ujangili nchini kwa kutumia askari wa jeshi
la lawanchi Tanzania (JWTZ)…huu ni mkakati mzuri ambao binafsi
nimempongeza sana kwa hatua hiyo” alisema Msigwa .
Kuwa ni mara kadhaa
watanzania wamepata kusikia viongozi wa Serikali wenye dhamana
wakisema kuwa mtandao wa majangili na wafanyabiashara haramu wa
wanyamapori ni mpana na mgumu kuumaliza
Pia
ni mara kadhaa pia Serikali imeendelea kukiri kuwa mtandao huu
unawahusisha Wafanyabiashara wakubwa, Wanausalama, Wabunge, Wanasiasa na
watu wenye dhamana ya uongozi katika taifa letu umekuwa ni kikwazo
kikubwa katika vita dhidi ya ujangili.
“….Serikali
imeendelea kutoa matamko kuwa itawataja wahusika wa biashara haramu
dhidi ya wanyamapori na kuwachukulia hatua lakini cha kushangaza, mara
zote hakuna hatua yoyote inayochukuliwa..ni jambo moja la msingi ambalo
ningependa kulizungumza na kusisitiza hapa leo ni juu ya wajibu wa kila
Mtanzania katika kuhakikisha kuwa tunaungana kwa pamoja katika vita
dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori”
Hivyo
alisema hatua ya Rais Kikwete kuweka mkakati huo wa kutumia
askari wa JWTZ katika kulinda hifadhi na kupambana na majangili ni
jambo la kumpongeza.
Kwani
alisema baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika tamko
lake maarufu mwaka 1961 lijulikanalo kama Arusha Manifesto alisema
yafuatayo
“Uhai
wa wanyamapori ni jambo muhimu na linalotuhusu sana sisi sote barani
Afrika. Viumbe hawa wa porini, wakiwa katika mapori wanamoishi,sio
muhimu tu kwa ajili ya kuajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu
ya maliasili yetu na pia ndio mustakabali wa maisha yetu ya baadaye”.
Alisema
kuwa mwalimu Nyerere alitambua umuhimu wa kutunza wanyamapori kwa
wakati huo tukiwa na hazina kubwa ya wanyama, lakini leo viongozi wa
Serikali wameshikwa na kigugumizi katika kuhakikisha dira na jitihada za
baba wa taifa letu ,vinatimizwa.
Hivyo
alisema kama kiongozi ambaye wananchi wamenipa dhamana ya
kuwawakilisha, nawiwa kutumia nafasi hiyo, kuendeleza juhudi zangu na
kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakua mdau
nambari moja wa kupinga biashara haramu ya wanyamapori kwani si tu kuwa
inalitia hasara taifa letu bali pia inaweka hatarini maisha ya
wanyamapori kwa vizazi vijavyo.
“Nachukua
nafasi hii kuikumbusha na kuitaka Serikali kutimiza wajibu wake kwa
kuwafikisha majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori katika
vyombo vya dola na watendewe ipasavyo kwa mujibu wa Sheria”Kuhusu watu maarufu mkoani Iringa wanaojihusisha na biashar a ya pembe za ndovu na hata kutumia magari ya umma kama Ambulence kusafirisha pembe hizo za ndovu alisema kuwa ana idadi yao ndevu zaidi na kuwa katika kikao cha bunge kijacho ataweka hadharani majina yao.
Kiongozi wa wanaharakati wa mtandao wa kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Fundi Mihayo alisema kuwa mbinu mbali mbali zinatumika katika kusafirisha pembe za ndovu ikiwa ni pamoja na usafiri wa boda boda kutumika sasa kuendeshea vitendo vya ujangili .
Alisema usafiri huo umekuwa ukitumika kuvushia pembe za ndovu katika maeneo ya vizuizi na hivyo kutaka ulinzi na upekuzi mkubwa unahitajika katika kukomesha vitendo hivyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa MANET Zuberi Mwachura alisema kuwa lengo la mtandao huo ni kuendelea kupambana na vitendo vya ujangili katika maeneo ya hifadhi nchini .
Kwani alisema kuwa usalama wa wanyama pori na mazingira yao ni walazima kwa maendeleo yetu hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kujua na kufahamu eneo ambalo wanatoka au wanaishi watu wanao fanya au kushiriki au kujihusisha na vitendo vya ujangili ni jukumu letu kuhamasisha jamii ya wananchi wote wajione wana wajibu wa kushiliki katika vita dhidi ya ujangili.
“..lazima tukubali kwamba ujangili upo, Pamoja na changamoto zake, lakini hatuwezi kukaa kimya tukiacha majangili waendelee kuteketeza tembo wetu. …. Mwanzo wa mafanikio katika jambo lolote ni dhamila na nidhamu, ya kupanga na kutekeleza. ….. Kwa kukubaliana katika nia hii ya kupambana na ujangili ni vizuri tuwe na tamko la dhamira yetu ya kujinasua katika Lindi Kubwa la ujangili wa Tembo”
0 comments:
Post a Comment