Thursday, July 11, 2013

MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI

Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
 
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
  
Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela  
 
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
Na  Mbeya yetu

Related Posts:

  • Nini hatma ya kesi ya Kenyatta ICC? Pande zinazohusika katika kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC Mjini The Hague zimekuwa na kikao cha kujadili mstakabali wa kesi hiyo. Kiongozi wa mashtaka wa I… Read More
  • Utata kesi ya Mtanzania Afrika Kusini Kesi ya Mtanzania Stephen Ongolo anayeshikiliwa na polisi Afrika Kusini akituhumiwa kutishia kutoa siri za mke wa pili wa Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli Zuma (MaNtuli), im… Read More
  • Tanzania yakamata dawa za kulevya Polisi nchini Tanzania wamekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo 201 katika eneo la bahari kati ya Dar es Salaam na Zanzibar nchini humo. Kamanda wa kikosi maalum cha kuzuia… Read More
  • FAMILIA KUMINA TANO HAZINA MAHALA PAKUISHI GEREZA PAWAGA  Ofisi za Gereza Pawaga zilizo ezuliwa na upepo mkali ulio ambatana na mvua juzi jioni.  Sehemu ya masalia ya bati na matandiko yalio haribiwa na mvua  SACAP Deusdedit Kamugisha Afisa wa … Read More
  • MSAMBINUNGWA” by TUNDA MAN feat ALLY KIBA MSAMBINUNGWA” by TUNDA MAN feat ALLY KIBA (Photo’s) The Making of music Video “MSAMBINUNGWA” by TUNDA MAN feat ALLY KIBA - See more at: http://onelovetz.blogspot.com/2014/01/photos-making-of-music-video.html#sthash.txPg… Read More

0 comments: