TIMU ya Yanga jana ilizidi kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania
Bara baada ya kuilaza JKT Oljoro mabao 3-0 kwenye mchezo uliopigwa
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo, Yanga
imefikisha jumla ya pointi 52 baada ya kucheza mechi 22. Mabao ya Yanga
yaliwekwa kimiani na Nadir Haroub 'Cannavaro', Simon Msuva na Hamis
Kiiza 'Diego'.
0 comments:
Post a Comment