| Mwenyekiti wa MANET Bw Zuberi Mwachura kulia akieleza mkakati wa kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya taifa ya Ruaha leo |
| Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akifafanua jambo |
MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema), Mchungaji Peter Msigwa amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa mkakati wake wa kunusuru vitendo vya ujangili katika hifadhi za Taifa.
Kuhusu watu maarufu mkoani Iringa wanaojihusisha na biashar a ya pembe za ndovu na hata kutumia magari ya umma kama Ambulence kusafirisha pembe hizo za ndovu alisema kuwa ana idadi yao ndevu zaidi na kuwa katika kikao cha bunge kijacho ataweka hadharani majina yao.
Kiongozi wa wanaharakati wa mtandao wa kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Fundi Mihayo alisema kuwa mbinu mbali mbali zinatumika katika kusafirisha pembe za ndovu ikiwa ni pamoja na usafiri wa boda boda kutumika sasa kuendeshea vitendo vya ujangili .
Alisema usafiri huo umekuwa ukitumika kuvushia pembe za ndovu katika maeneo ya vizuizi na hivyo kutaka ulinzi na upekuzi mkubwa unahitajika katika kukomesha vitendo hivyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa MANET Zuberi Mwachura alisema kuwa lengo la mtandao huo ni kuendelea kupambana na vitendo vya ujangili katika maeneo ya hifadhi nchini .
Kwani alisema kuwa usalama wa wanyama pori na mazingira yao ni walazima kwa maendeleo yetu hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kujua na kufahamu eneo ambalo wanatoka au wanaishi watu wanao fanya au kushiriki au kujihusisha na vitendo vya ujangili ni jukumu letu kuhamasisha jamii ya wananchi wote wajione wana wajibu wa kushiliki katika vita dhidi ya ujangili.
“..lazima tukubali kwamba ujangili upo, Pamoja na changamoto zake, lakini hatuwezi kukaa kimya tukiacha majangili waendelee kuteketeza tembo wetu. …. Mwanzo wa mafanikio katika jambo lolote ni dhamila na nidhamu, ya kupanga na kutekeleza. ….. Kwa kukubaliana katika nia hii ya kupambana na ujangili ni vizuri tuwe na tamko la dhamira yetu ya kujinasua katika Lindi Kubwa la ujangili wa Tembo”

































