Video: Sasha siku alipokuwa akiongea na GPL kuhusu madai ya kuzaa na Diamond.
MREMBO Sasha Juma, 20, kwa sasa anapitia kipindi cha majuto,
analipia gharama ya kujivalisha ubandidu na kujisingizia kupewa mimba na
supastaa, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Sasha Juma akiongea na…
Video: Sasha siku alipokuwa akiongea na GPL kuhusu madai ya kuzaa na Diamond.
MREMBO Sasha Juma, 20, kwa sasa anapitia kipindi cha majuto,
analipia gharama ya kujivalisha ubandidu na kujisingizia kupewa mimba na
supastaa, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Sasha Juma akiongea na GPL..
Sasha, akiwa na macho makavu, alitamka
mbele ya waandishi wetu kuwa mimba hiyo aliyopewa na Diamond,
ilimgharimu kufukuzwa shule akiwa kidato cha nne mwaka jana.
Unadhani Sasha analo tena? Ameshaumbuka na baada ya simulizi yake ya
kutunga kushtukiwa, hivi sasa mrembo huyo anatishia kujiua.
Mr. Juma
ambaye ni baba mzazi wa Sasha, aliliambia Risasi Mchanganyiko: “Huyu
mtoto ametishia kujiua, anajua makosa aliyoyafanya. Anataka kutuvuruga
vichwa, ukweli ni kwamba kila alichokisema kuhusu Diamond ni uongo
mtupu.
“Nahisi kuna mtu yupo nyuma yake, sasa anataka kumtumia ili
kumchafua Diamond, upande mwingine akili yangu inaniambia yule mtoto
anataka umaarufu, maana najua yule ni mwigizaji, sasa pengine anataka
kutoka.”
Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
UONGO WA SASHA
Risasi, lilipata taarifa kuhusu malalamiko ya
Sasha ambaye alikuwa akidai kupotezewa dira ya maisha na Diamond kwa
sababu alimpa mimba na kumtelekeza na mtoto mwenye umri wa miezi minne.
Baada ya kupata ‘tipu’ hiyo, mwandishi wetu alimsaka kwa udi na uvumba
mpaka Septemba 4, mwaka huu (Jumatano ya wiki iliyopita) ambapo mrembo
huyo alitia maguu kwenye mjengo mkubwa wa magazeti pendwa nchini
Tanzania, Global Publishers Ltd.
Baada ya kuwasili makao makuu ya
Global Publishers, Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, Sasha aliingizwa
kwenye chumba maalum chenye mitambo ya kurekodi sauti na picha kisha
akaanza kumwaga simulizi yake.
Alidai kuwa alikutana na Diamond,
Mlimani City, mwaka jana, wakapeana namba za simu kabla ya kuanzisha
uhusiano wa kimapenzi ambao uliwafikisha kwenye ‘kategori’ ya kuparamia
kitandani na kutenda mchezo wa baba na mama pasipo kutumia na kinga.
“Nilipopata mimba Diamond alinishawishi nisitoe, akaniahidi
atanisomesha hata kama nitafukuzwa shule. Baadaye nilifukuzwa shule,
akazidi kunipa moyo kwamba atanilinda. Mimba ilipokuwa kubwa akapotea,
nilipozaa hakujitokeza.
“Diamond akawa siyo yule ambaye alikuwa
ananipa moyo. Alibadilika, hali hiyo ikanifanya nione mwanangu hana
baba, hata cheti za kuzaliwa, sijamwandika Diamond, mtoto wangu nimempa
ubini wa baba yangu, yaani ya Juma.”
Sasha akiwa na mtoto aliyedai ni wa Diamond.
NI UONGO MTAKATIFU
Ili kukamilisha habari hiyo ambayo ilitoka
kwenye gazeti hili, toleo la Jumamosi iliyopita, mwandishi wetu
aliwasiliana na baba mzazi wa Sasha (Mr. Juma) ambaye alipoambiwa kuhusu
mwanaye kuzaa na Diamond, alishtuka kisha akasema:
“Unajua yule
mtoto sikai naye, anaishi na mama yake. Mimi sijui chochote ila
nashangaa, inawezekanaje apate mimba mpaka azae mimi baba yake sijui?
Ngoja niongee na mama yake.”
Mr. Juma alipiga simu kuzungumza na mama yake Sasha mbele ya mwandishi wetu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;
MR. JUMA: Habari yako.
MAMA SASHA: Salama tu, za kwako?
MR. JUMA: Namshukuru Mungu, ebwana mbona Sasha kaongea na mwandishi wa habari anasema kapewa mimba na Diamond na amezaa?
MAMA SASHA: Wewe si unajua haya mambo ya vijana?

MR. JUMA: Mambo ya vijana kivipi? Ina maana mtoto anapata ujauzito mpaka anazaa wewe na baba yake hamjui?
MAMA SASHA: Baba nani, si wewe?
MR. JUMA: Mimi baba yake sijui, ndiyo maana nakuuliza wewe, maana nimesikia umekuwa unawasiliana na Diamond kuhusu hili.
MAMA SASHA: Nani kakwambia? Nimeshasema hayo ni mambo ya watoto, naomba
umuulize mwanao vizuri, kama hauna namba yake nikutumie.
Katika
mazungumzo hayo, Mama Sasha, hakumpa majibu ya moja kwa moja mzazi
mwenzake, kuhusu binti huyo kupata mimba, kuzaa na Diamond kuwa mhusika.
RIPOTI YA WIKI HII
Mr. Juma alifika ofisi za Global Publishers na kueleza: “Jana (Jumapili
iliyopita), nilimchukua Sasha na kuzungumza naye kwa kirefu, kwa kifupi
alikiri kuwa hajawahi kupata mimba na yule mtoto si wa kwake.
“Mtoto imebainika ni wa dada yake, yaani mtoto mkubwa wa Mama Sasha
ambaye anaitwa Khadija. Kuna kitu cha kujifunza hapa kuwa Sasha
aliwadanganya mpaka watu ambao niliwakabidhi ili wamsaidie kisanii.
“Kabla sijaongea kwa kirefu na Sasha, nilizungumza na Thabit Abdul
(mwanamuziki wa Five Stars) ambaye nilimkabidhi kwake kumsimamia
kisanii, nikamuuliza inakuwaje mtoto anapata mimba? Akanijibu hata yeye
anashangaa. Kwani hata yeye alishangaa kumuona Sasha akiwa na picha
nyingi amebeba mtoto kwenye simu yake.
“Akamuuliza umezaa akajibu
ndiyo. Hisia zangu zinazunguka katika mambo mawili, ama aliamua kutunga
ili kupata umaarufu kupitia jina la Diamond au alitumwa na mtu. Jana
wakati nazungumza na Sasha, nilikasirika sana, nikaona hatutafika
pazuri.
“Ikabidi nimpigie simu rafiki yangu mmoja ili amwite
azungumze naye. Kweli alimwita wakazungumza, baadaye yule rafiki yangu
akaniambia Sasha kasema anaona mambo yanazidi kuwa makubwa, kwa hiyo
anataka kunywa sumu afe. Namshangaa sana huyu mtoto, sijui ana kichaa
gani?”
UKWELI NI HUU
Kwa mujibu uchunguzi wetu usio na
shaka, mtoto aliyepigwa picha akiwa amebebwa na Sasha, mama yake halisi
ni dada wa mrembo huyo ambaye ni Khadija.
Sasha na Khadija wanaunganishwa na mama yao lakini kila mmoja ana baba yake.
Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa kwa sasa Khadija anaishi na mwanaye
mkoani Tanga, huku Sasha akiendelea kupuyanga ndani ya Jiji la Dar,
akiwa hajui tamu wala chungu ya kunyonyesha, vilevile hajawahi kusikia
uchungu wa uzazi wala hatambui sura ya ‘leba’ ilivyo.
Khadija
akizungumza kupitia simu ya Mr. Juma, huku mwandishi wetu akifuatilia
mazungumzo, alisema: “Nikija Dar nitafika Global, mimi ndiyo mama wa
yule mtoto na zile picha Sasha alipiga na mtoto siku ya arobaini yake.
“Sasha anataka kunisababishia matatizo na baba mzazi wa mtoto. Mimi
kama mama mzazi wa mtoto, simjui Diamond, kwa hiyo hahusiki chochote na
mtoto wangu.”
Aidha, Mr. Juma alisema kuwa alimpigia simu Diamond na kumuweka sawa kuhusiana na tuhuma ambazo binti yake alimsakizia.
“Diamond anajua kila kitu, nimeshaongea naye na nimejaribu kumtaka
atulize munkari, maana ni wazi zile taarifa zimemchukiza sana. Kweli
zimemchukiza.”
DIAMOND ANASEMAJE?
Gazeti hili
lilipozungumza na Diamond, alisema: “Nilishasema simjui huyo Sasha,
ahadi yangu ipo palepale, nitampeleka mahakamani. Amenichafua sana.
“Masharti yangu ni haya, kama anataka nimsamehe aende kweye redio na televisheni akatangaze kwamba sijampa mimba.”
ONYO
Aibu ambayo Sasha anakutana nayo sasa na tishio la kuburuzwa mahakamani
ambalo analikabili kutoka kwa Diamond ni onyo kwa watu wengine ambao
wamekuwa na tabia za kuwasingizia wenzao ili kujipatia umaarufu.
Risasi linazo taarifa kwamba tangu alipoumbuka, Sasha amekuwa mtu wa
kujificha, akikwepa kukutana na watu ambao wanajua mkanda mzima wa
simulizi yake ya kutunga.