RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AZURU WILAYA YA SEGEREMA
PICHA NA JOHN LUKUWI
DIWANI WA TLP :SIASA SI UADUI, AMFAGILIA KINANA KWA BUSARA ZAKE
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLoKBfZOSl6UotMt_1M7KgeFw2NQo5ssk9TzdVi2TQz6fWB2EmwREkHqC28O0U_r7OMbNkvCFRCxhdrYAMkOnavrRXULmsu3QeYJM8wo3A8xe-GsEUPNd9hM4jJQeFhpfC19XCKBifAhT0/s1600/TLP.jpg)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na diwani wa TLP
Ntabo Majabi kata ya MwendaKulima wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo
cha afya kilichodhaminiwa na mgodi wa Buzwagi kulia ni Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
……………….
Na Adam Mzee
DIWANI
wa Kata Mwendakulima Ntabo Majabi kupitiaTanzania Labour Party (TLP),
amesema Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhaman Kinana ni kiongozi mwenye busara
na hekima kubwa na ndio maana Rais Jakaya Kikwete amemua kumpa nafasi
hiyo kwa kuwa atakuwa anamjua vizuri.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kituo cha afya katika eneo hilo, alisema
amefurahishwa na aina ya siasa ambazo zinafanywa na Kinana na yeye
binafsi ametambua kuwa Katibu Mkuu huyo wa CCM anaouwezo mkubwa wa
kufanya kazi zake.
“Kinana
wewe ni jembe, wakati unazungumza nilikuwa nimekaa mbali na kusikiliza
lakini maelezo yako yamenifurahisha na ndio maana nimeamua kuja kukupa
mkono.Kama nchi hii ingekuwa na makatibu wakuu wengi wa aina yako,
tungepiga hatua hasa katika siasa za nchi hii.
“Pia
niwaambie wananchi siasa si ugomvi, Kinana ameeleza vizuri, tunatakiwa
kushirikiana ili kufanikisha malengo ya kuwatumikia wananchi.Nakupongeza
mzee Kinana kwa maelezo yako yamenipa faraja licha ya kwamba mimi ni
diwani kupitia TLP,”alisema.
Ndugu
Kinana alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa CCM ndio yenye
Serikali na diwani huyo licha ya kuwa TLP bado anatekeleza ilani ya CCM ,
hivyo wananchi nao wanatakiwa kutambua hakuna sababu ya kulumbana
kwasababu tu ya mambo ya siasa.
0 comments:
Post a Comment