Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MENEJA
wa Timu ya Taifa ya England, maarufu `Simba Watatu`, Roy Hodgson
amepumua kidogo katika harakati zake za kuwania kucheza fainali za kombe
la Dunia mwakani nchini Brazi baada ya kutoka suluhu dhidi ya Ukraine
jana usiku.
England
iliingia uwanjani kupambana kwa nguvu bila ya nyota wake Wayne Mark
Rooney, Dany Welbeck na Daniel Sturrage kutokana na sababu tofauti.
Sturrage na Rooney ni majeruhi, wakati Welbeck alikuwa anatumikia kadi aliyopewa mechi ya nyuma.
Juni
19, 2012, ilikuwa mara ya mwisho kwa England kushinda mechi ya
ushindani, lakini si dhidi ya Moldova au San Marino bali Upinzani wa
siku hiyo ulikuwa dhidi ya Ukraine, na toka hapo, England imeshakutana
mara mbili na wakali hao na kushindwa kuibuka na ushindi.
England
wamebakiwa na mechi dhidi ya Montenegro pamoja na Poland mwezi ujao na
wanatakiwa kupata ushindi ili kukata tiketi ya kcuheza fainali za kombe
la Dunia mwakani nchini Brazil.
Na mechi hizo watacheza katika dimba lao la Taifa la Wembley, hivyo kujipa matumaini ya kufanya vizuri.
Kikosi cha Ukraine: Pyatov, Fedetskiy, Khacheridi, Kucher, Shevchuk, Stepanenko, Edmar, Gusev (Bezus 68), Yarmolenko (Khomchenovskiy 90), Konoplianka, Zozulya (Seleznyov 90). Subs: Koval, Dedechko, Tymoschuk, Mandzyuk, Grechyshkin, Morozyuk, Rakitskiy, Devic,
Khudzamov.
Khudzamov.
Kikosi cha England: Hart, Walker, Cahill, Jagielka, Cole, Lampard, Gerrard, Wilshere (Young 68), Walcott (Cleverley 89), Lambert, Milner. Subs: Ruddy, Smalling, Baines, Caulker, Carrick, Barkley, Defoe, Sterling, Townsend, Forster.
0 comments:
Post a Comment