This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Tuesday, May 14, 2013
GODBLESS LEMA ASAKWA NA POLISI WA U.K KWA KOSA LA KUMBAKA FLORA BAHATI LYMO
MWIZI KWA KUTUMIA BODABODA AUAWA!
KIJANA mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayedaiwa ni mzoefu wa wizi kwa kutumia usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’, ameuawa baada ya kumliza mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jusmini.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar, saa tatu usiku ambapo inadaiwa mwanamke huyo alikuwa akikatiza mitaa hiyo huku akiwa ameweka mkoba wake kwapani.
Ikadaiwa mwanamke huyo akiwa eneo hilo huku akiamini yuko salama, ilitokea bodaboda kwa nyuma ikiwa imebeba abiria na ghafla alishangaa anakwapuliwa mkoba wake.
“Unajua yule mama alikuwa akitembea kwa kujiamini lakini inavyoonekana wale jamaa ambao ndiyo zao kuwaibia watu walikuwa wamemlia ‘timing’ tangu aliposhuka kwenye daladala.
“Tuliposikia makelele ya mwizi, tulimfuata mama huyo na tulipomuuliza akatuambia ameibiwa mkoba wake huku akituonesha vijana hao ambao muda huo walikuwa wakikimbia,” kilieleza chanzo hicho kilichoshuhudia tukio zima.
Ikaelezwa kuwa, kufuatia maelezo ya mwanamke huyo, baadhi ya watu wenye hasira kali wengine wakiwa kwenye pikipiki waliamua kuwakimbiza wezi hao ambapo mmoja alishuka na kukimbia kivyake huku mwenye bodaboda akizuiwa kwenye geti kuu ya kutokea magari.
“Alipozuiwa akaona imeshakua soo, akashuka na kuitelekeza pikipiki yake kisha akataka kudandia gari nyingine lakini watu wakafanikiwa kumkamata kwenye mataa ya Mwenge ambapo magari yalisimama, jamaa alishushiwa kichapo hadi akauawa,” kiliendelea kupasha chanzo hicho.
Baada ya kijana huyo kuuawa, polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wake. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela (pichani)alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema taarifa za kifo cha kijana huyo hazijafika mezani kwake lakini akasema anaendelea kufuatilia.
KASHIFA YA NGONO YALITAFUNA BUNGE LETU....WABUNGE WADAIWA KUBEBANA NA KUPEANA MIMBA
SKENDO nzito inalitafuna Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikitawala madai kwamba kuna wabunge wawili wanawake, wamejazwa mimba na waheshimiwa wenzao wanaume.
Awali, ulitawala uvumi kuwa mmoja wa wabunge wa upinzani (viti maalum), akitokea Kanda ya Kaskazini, amepewa ujauzito na mheshimiwa mwingine ambaye ni kiongozi anayeshika nafasi za juu kwenye moja ya vyama vikuu vya upinzani nchini (wote majina yao tunayahifadhi kwa sasa).
Kashfa hiyo ya mtunga sheria huyo kupewa mimba na mheshimiwa mwenzake ambaye ni mume wa mtu, ilipata mbeleko na kuifanya ivume zaidi, baada ya Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde, kulipuka bungeni: “Humuhumu ndani kuna wabunge wanawake wenye mimba zisizotarajiwa.”
Lusinde, alitamka hayo Aprili, mwaka huu, wakati akichangia hotuba ya bajeti, Ofisi ya Waziri Mkuu, kipindi ambacho bunge lilikuwa limechafuka kutokana na wabunge kurushiana ‘mipasho’ wao kwa wao.
Kauli ya Lusinde, pamoja na kupokelewa tofauti na wabunge wengi wanawake, wakidai mheshimiwa mwenzao amewadhalilisha, upande mwingine, katika ‘vikao vya kwenye korido’, matukio ya vicheko na kugonga mikono yalitawala na kunena kwa msisitizo “message delivered”, yaani ujumbe umefika.
Katika kufanyia kazi kila kinachozungumzwa, mwandishi wetu alizungumza na baadhi ya wabunge ambapo Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, alisema: Unajua madai ya mimba yanawahusu wanawake, kwa hiyo waulizwe wenyewe.
“Kama umenitafuta mimi kwa kigezo kwamba ni mbunge kijana, basi waulize wabunge vijana wanawake,” alisema Mnyika.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, alikiri kufahamu kuwepo kwa tuhuma kwamba wapo wabunge wamepeana mimba lakini hawezi kuwa na uhakika kwa sababu uhusiano wa kimapenzi ni jambo la faragha.
“Hayo madai yapo, yanazungumzwa. Wapo wanaotajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, hayo ni mambo ya faragha. Sijui pengine walioanzisha haya madai wana vipimo vyao,” alisema Kafulila.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Morogoro, Sara Msafiri, alisema kuwa haiwezekani wabunge kupata mimba zisizotarajiwa kwa sababu ni watu wazima.
“Wabunge tunapata mafunzo ya uzazi, kwa hiyo kama ni mimba basi mtu anakuwa amepanga kuipata. Hakuna kitu kama hicho. Hata hilo la kutoa mimba halipo kabisa, sijawahi kusikia mtu amefanya hivyo bungeni,” alisema Sara.
Mbunge mwingine wa Viti Maalum (Chadema), Chiku Abwao, alisema: “Hakuna mbunge anayepata mimba isiyotarajiwa, kwanza nilimshangaa mbunge kutamka mambo kama hayo, alistahili kuwaambia watoto, lengo lake lilikuwa kudhalilisha wanawake.”
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Munde Tambwe, alisema: “Ile kauli ya Lusinde kwamba kuna wabunge wanapata mimba zisizotarajiwa, nadhani kuna mtu alikuwa anamlenga, kwa hiyo mimi siwezi kulizungumzia.”
PICHA 5 ZA WANAFUNZI WA MANZESE WALIOVAMIWA NA MASHETANI LEO ASUBUHI
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda maeneo hayo.
Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.
Saturday, May 11, 2013
MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR

Clouds Media Group yazindua msimu wake mpya kwa kishindo
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa Muziki hapa chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini hiyo iliyohusu na harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa Dodoma.…
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa Muziki hapa chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini hiyo iliyohusu na harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa Dodoma.kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa. Aidha pia mchana huu kutakuwepo na burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania katika uwanja wa jamhuri .
fursa hizi kwa umoja na maendeleo ambapo TWENZETU, inakuwa neno rasmi la
mawasiliano.Kama vile haitoshi kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia
wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali
zitahusishwa ikiwemo semina ya fursa kwa
watanzania,burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula
na bidhaa mbalimbali za kitanzania zitapatikana uwanja wa jamhuri mapema leo mchana.










































