This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, April 16, 2013

MHESHIMIWA AUMBUKA!

Bumbuwazi: Meneja Everson Makowa-Mwale (49), akiwa ameduwaa baada ya kunaswa akijivinjari na mke wa mfanyakazi wake.
NI aibu kubwa kuliko maelezo! Meneja wa kampuni ya kusafirisha mizigo ya Malawi Cargo, tawi la mkoani hapa, Everson Makowa-Mwale (49), raia wa nchi jirani ya Malawi amenaswa chumbani na mke wa mfanyakazi wake (jina tunalo).
Tukio hilo lililojaa fedheha lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya saa 11:25 jioni baada ya askari wa jeshi la polisi, ndugu na jamaa kufika eneo la hoteli moja maarufu jijini hapa (jina limehifadhiwa) na kumkuta chumbani akiwa mtupu akijiandaa kufanya ngono na mke huyo wa mtu.
Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo, kabla ya kuumbuka, alikuwa ameandaa mazingira yote kwa ajili ya kuvunja amri ya sita na mke huyo wa mfanyakazi wake.
Mtego wa kumnasa ulifanikiwa baada ya mtuhumiwa kutinga hotelini hapo akiwa na gari la kampuni aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 821 ASY na kunyooka moja kwa moja chumbani alikokuwa akisubiriwa na mwanamke huyo.
WASIFU WA MENEJA
Habari za uhakika zilieleza kuwa bosi huyo ni mbunge mstaafu aliyewahi kuwa Mheshimiwa wa Jimbo la Nkotakota South East nchini Malawi kwa kipindi cha miaka kadhaa.
Jamaa huyo aliangushwa na Agness Chatipwa Mandebvu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2009 nchini humo ndipo akatinga jijini hapa na kupata kazi ya umeneja wa kampuni hiyo ya usafirishaji.
MADAI MAZITO
Ilidaiwa kuwa meneja huyo ndiyo mchezo wake kwa sababu amekuwa akiwafanyia hivyo mabinti wanaofika ofisini kwake kwa ajili ya kuomba kazi ambapo huwakubalia kuwapa kazi endapo watakubali kushiriki naye dhambi ya uzinzi.
Uchunguzi ndani ya kampuni hiyo ulidaka madai kuwa tangu awe meneja, mabinti zaidi ya watano waliacha au kufukuzwa kazi walipokataa kufanya naye ngono.
Ilidaiwa kuwa wanaokubaliana na hali hiyo kutokana na ugumu wa maisha humkubalia na kupandishwa vyeo kiholela.
Sakata la tabia hiyo chafu kwa raia wa Kitanzania, lilifikia kikomo baada ya mfanyakazi mmoja (jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani wa meneja huyo kusimamishwa kazi kwa madai kuwa alichelewa kuripoti kazini.
MCHEZO WA NIPE NIKUPE
Mfanyakazi huyo ambaye alikuwa akiishi na mkewe nyumbani kwa bosi wake, alisimamishwa kazi ambapo bosi huyo alitumia mwanya huo kuanza kumchombeza mke wa jamaa huyo kwa kumwambia amkubalie ili amrudishe mumewe kazini.
Baada ya kupata usumbufu huo kwa kipindi kirefu ndipo jamaa huyo pamoja na wafanyakazi wenzake ambao walikuwa hawaipendi tabia ya bosi wao wakaandaa mtego uliomnasa kama panya bila kujinasua na kuishia mikononi mwa polisi.
WAFANYAKAZI
Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo ambao majina yake hawakutaka yaandikwe gazetini, walisema tabia ya bosi wao imekithiri na kwamba amekuwa akitumia wadhifa wake kuwalaghai watoto wa kike ili kufanya nao mapenzi.
Wafanyakazi hao walidai ni bora Idara ya Uhamiaji mkoani hapa iingilie kati suala hilo ili kuwanusuru Watanzania dhidi ya watumishi wa kigeni wanaokuwa na tabia zinazolenga kuwaondolea utu wao.
TURUDI KWENYE TUKIO
Baada ya kufumaniwa akiwa mtupu kutokana na mke wa mtu huyo kutoa ishara kwa walioweka mtego, aliomba radhi kwa mume wa mwanamke huyo ambaye ni mwajiriwa wa kampuni anayefanya kazi ya kutengeneza bustani.
Hata hivyo, msamaha wake ulikataliwa na soo likatinga polisi na sasa anasubiriwa kupelekwa mbele ya mkono wa sheria...

Airtel na Nokia wazindua Offer Kabambe ya Nokia Lumia 620

Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 BatuliChombo mwandishi wa habari wa Sikuba kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa  Simu hiyo kwa ushirikiano katiya Airtel na Nokia  utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju…
Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa  simu Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu
* Wateja kupata muda wa maongezi wa dakika 275 bure
* Offa itajumuisha SMS bila kikomo na kifurushi cha internet ya 3.75G cha 3GB
Monday 15 Aprili 2013, Airtel Tanzania imeungana kwa pamoja na kampuni ya Nokia na  kuzindua simu ya Nokia Lumia 620 itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kuunganishwa na huduma ya technologia ya juu kwa
kupitia simu za kisasa na kupata ofa kabambe za bure za muda wa mongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet kwa muda wa mienzi mitatu Nokia Lumia 620 pamoja na simkadi ya Airtel itatoa uwezo tofauti ikiwemo kuunganishwa na internet na mtandao na kuangalia mitandao mbalimbali yakijamii pamoja na tovuti mbalimbali.
Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Jimy Tara mwandishi wa habari wa ITV kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa  Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia  utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju
Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju kwa pamoja wakionyesha kipeperushi cha Nokia Lumia 620 wakati wa wakati wa uzinduzi wa  Nokia Lumia 620 kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia  utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
Nokia Lumia inamuonekano mzuri na wa  kisasa wenye rangi za kipekee ambapo kutokana na ubunifu `wetu wa kutengeneza simu zenye rangi tofauti mteja ataweza
kujichagulia simu yenye mvuto na rangi aitakayo Vitu vingine vilivyopo kwenye simu hii ya Nokia Lumia ni pamoja na kamera yenye lensi ya kisasa, ya mega pixel 5, pamoja na kamera ya mbele, kutokana na kuwa na Lensi bora hii itamuwezesha mteja kupata video au picha yenye muonekano mzuri zaidi Ndani ya Nokia Lumia 620 unaweza kupata vitu muhimu sana ikiwemo ramani ya Dunia pamoja na maelekezo maalum wa vitu au sehemu maalum mbalimbali.
Akiongea wakati wa uzinduzi Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema" tumeshirikiana na Nokia katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora na nafuu kwa kupitia vifaa vya Nokia vinavyokuhakikishia kiwango cha juu huku tukiwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu.Kwa kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G tunayoitoa nchi nzima wateja wetu wana hakikishiwa huduma za uhakika wakati wote.Nokia Lumia itaunganishwa na ofa ya kifurushi cha muda wa maongezi cha dakika 275, sms bila kikomo na intenet ya kifurushi cha 3GB kitakachopatika kwa wiki moja kila mwenzi kwa muda wa mienzi mitatu "Kupata offa hii wateja wetu watatakiwa kuweka muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi 1000 mara wanaponunua simu ya Nokia Lumia 620. Na katika kuthibitisha thamira yetu ya kutoa huduma zinazoendana nathamani ya pesa ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu.Airtel itaendelea kushirikiana na makampuni mbalimbali katika kutoa huduma bora na bei nafuu kwa kupitia mtandao wake mpana wenye huduma muhimu za Airtel Money na huduma yetu kabambe ya Airtel yatosha Aliongeza Mmbando.Kwa upande wake Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, alisema kampuni ya Nokia inaendelea kuonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kutoa bidhaa za simu bora zitakazowapatia wateja kile wanachokihitaji.
Tunafurahia kuleta bidhaa bora na za bei nafuu zenye uwezo tofauti, simu ya Nokia Lumia 620katika soko la Tanzania. Tunaamini  muundo mzuri wa simu hii, rangi nzuri na uzoefu tofauti pamoja na huduma za Airtel zitawapatia wateja wetu sababu ya kujipatia simu hii ya Nokia Lumia" "Nokia Lumia 620 zinapatikana kwa gharama ya shilingi 450,000/= tu.Simu inapatikana katika maduka yote ya Airtel, midcom na wakala wa Nokia wa premium. kwa sasa, kinachotakiwa kufanya ni wewe mtanzania kutembelea moja kati ya haya maduka na kujipatia simu hii orijino kutoka Nokia.Kutokana na ubora wa simu hizi za Nokia Lumia 620 mteja ataweza kufurahia zaidi huduma zote za kimtandao za Airtel zikiwemo zile za kutuma na kupokea pesa, Airtel Yatosha, Jirushe, kutuma na kupokea
SMS, huduma bora ya Intaneti ya 3.75G na nyingi nyinginezo.

Monday, April 15, 2013

EXTRA BONGO WAFANYA MAKAMUZI MEEDA CLUB - Hello:

EXTRA BONGO WAFANYA MAKAMUZI MEEDA CLUB - Hello:www.facebook.com

DKT. SHEIN AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA WIZARA YA MIUNDOMBINU na MAWASILIANO IKULU ZANZIBAR LEO


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,( kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi,pia Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati)akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo…

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,( kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi,pia Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati)akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi, (wa tatu kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamadi.

Sunday, April 14, 2013

HII NDO LAANA INAYOTENDEKA MOMBASA......NASIKIA HUKO HADI WANAUME HUJIUZA


The 21st century generation seems to have thrown all caution and the respectable ways that the forefathers fought so hard to see their children grow up with are no longer there.

In Mombasa at some night clubs this is what goes down.

YANGA YAZIDI KUJIKITA KILELENI

Timu za Yanga na JKT Oljoro zikiingia uwanjani.
Yanga wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Simon Msuva.…
Timu za Yanga na JKT Oljoro zikiingia uwanjani.
Yanga wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Simon Msuva.
Hekaheka langoni mwa JKT Oljoro.
Haruna Niyonzima akijaribu kuipita ngome ya JKT Oljoro.
Hamis Kiiza akiifungia Yanga bao la tatu.
Mshikemshike langoni mwa Yanga.
Wanausalama wakifuatilia soka.
Mpaka mwisho wa mchezo score board ilisomeka hivi.
Raha ya mechi ushindi.
TIMU ya Yanga jana ilizidi kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuilaza JKT Oljoro mabao 3-0 kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa,  jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo, Yanga imefikisha jumla ya pointi 52 baada ya kucheza mechi 22. Mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na Nadir Haroub 'Cannavaro', Simon Msuva na Hamis Kiiza 'Diego'.