This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, February 28, 2014

Benki ya Dunia yaisimamishia Uganda msaada

Benki ya dunia imesitisha mkopo wa dola milioni 90 kwa Uganda wa kuimarisha sekta ya afya kufuatia kupitishwa kwa sheria inayoharamisha ushoga na kutoa adhabu kali kwa watakaopatikana na hatia Hatua hiyo ya benki ya dunia haikutarajiwa na wengi kwani taasisi hiyo mara nyingi hujiepusha kuingilia masuala ya ndani ya kisiasa ya nchi wanachama au kuhusiana na masuala kama haki za mashoga, kuepuka kuzishurutisha...

BANZA: NILIANZA SIGARA, BANGI, UNGA ILA SASA…

MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefunguka mazito juu ya matumizi mabaya ya bangi na madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na jinsi alivyokuwa akiyatumia. Akizungumza kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Global TV Online mwanzoni mwa wiki hii, Banza alikiri kutumia madawa ya kulevya na kusema; “Nilianza kuvuta sigara ya...

Real Madrid yaisulubu Schalke 04

Na Fadhy Mtanga REAL Madrid imejihakikishia kucheza robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Schalke 04 ya Ujerumani mabao 6-1. Mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo, mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili ulimwenguni Gareth Bale pamoja na mchezaji mahiri Karim Benzema walihakikisha kila mmoja wao anatupia nyavuni magoli mawili ili kuifanya Real Madrid, vinara wa ligi kuu nchini Hispania,...

STEVE NYERERE AMWAGIA SIFA LULU

Stori: Mayasa Mariwata RAIS wa Bongo Movie Unit, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amemmwagia sifa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuwa ni binti mdogo lakini sasa anajitambua tofauti na wasanii wengine wakubwa. Elizabeth Michael ‘Lulu’. Akipiga stori na Ijumaa Steve alisema kuwa, mbali na umakini katika kazi zake za kisanii, sasa hivi yuko makini...

RED HANDED! NJEMBA AUVAA MTEGO AKIWA NA MKE WA RAFIKI YAKE GESTI

  MAANDIKO yanasema ‘usitamani mali ya mtu mwigine’! Ni kweli kabisa, onyo hilo lilichukua fursa yake kufuatia njemba mmoja aliyejulikana kwa jina la Anton John Mwaweje kunaswa laivu gesti na mke wa rafiki yake aliyefahamika kwa jina moja la Chalz. Mke wa mtu sumu: Anton John Mwaweje baada ya kunaswa akiwa na mke wa rafiki yake gesti. Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii kwenye gesti moja...

WASANII WAZINDUA KAMPEINI KUHAKIKISHA MAPENDEKEZO YAO KIKATIBA YANASIKILIZWA

Wasanii mbalimbali wakifuatilia kuhusiana na katiba iliyokataliwa kusikilizwa. Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la sanaa (BASATA), Godfrey Lebejo Mngereza akihutubia wasanii.… Wasanii mbalimbali wakifuatilia kuhusiana na katiba iliyokataliwa kusikilizwa. Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la sanaa (BASATA), Godfrey Lebejo Mngereza akihutubia wasanii. Wana Hip hop kutoka kushoto, Danny Msimamo, Quick Racka, Profesa Jay, Nikki wa Pili na Kala...

WANACHAMA WA SACCOS YA WALIMU KILOLO WATAKIWA KUREJESHA MADENI

Afisa  ushirika mkoa  wa Iringa John Kiteve  akifungua mkutano huo   Mwakilishi wa CRDB Iringa akifuatilia matukio  katika mtandao huu  Mwakilishi wa benk ya CRDB Iringa Bw Bruno  akiwahamasisha  kujiunga na bima mbalimbali   Afisa ushirika mkoa wa Iringa John Kiteve akifungua mkutano mkuu wa Saccos ya  Walimu Kilolo leo Na  Francis Godwin Blog WANACHAMA...

Wednesday, February 26, 2014

Al Ahly watua Dar na vyakula, maji

WAPINZANI wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri wameonyesha wamepania kuhakikisha hawapotezi mchezo wa Jumamosi baada ya kutua nchini na maji na baadhi ya vyakula ambavyo watapikiwa wachezaji wao. Habari za uhakika kutoka Cairo, zimeeleza Ahly wamebeba chupa za maji, baadhi ya vyakula na kazi hiyo itafanywa na mpishi wao maalum raia wa… WAPINZANI wa Yanga katika mechi...

Alphonce Mawazo Meneja Kampeni wa Mgombea wa Chadema Kalenga, Achukua Nafasi ya Lema

Alphonce Mawazo, Kamanda wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Picha na Arusha Times) Arusha255 inaweza kuthibitisha uteuzi mpya wa Ndugu Alphonce Mawazo kama meneja kampeni za kumnadi mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bi Grace Tengega Mvanga katika uchaguzi mdogo wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Machi 16, 2014 katika Jimbo la Kelenga Mkoani Iringa kwa lengo la kumpata mbunge atakayewakilisha wana Kalenga baada ya...

SLAA AWANG'AKIA VIONGOZI WA SERIKALI!!

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amesema tatizo la umaskini linalowakabili Watanzania, linatokana na viongozi walioko madaraka kutokuwa waadilifu. Alisema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa vyema taifa haliwezi kuwa na watu maskini kama ilivyo hivi sasa. Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika katika Vijiji vya Igula katika Kata...

Tuesday, February 25, 2014

MAJAMBAZI WAUWAWA ARUSHA

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha Watu wanne ambao bado hawajafahamika wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa baada ya kupigwa risasi na askari Polisi. Tukio hilo lilitokea jana tarehe 21.02.2014 muda wa saa 1:00 jioni katika bar moja iitwayo Pama iliyopo maeneo ya Makao Mapya jijini hapa. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, tukio hilo lilitokea mara baada...

MREMBO AFARIKI GHAFLA GUEST ARUSHA

MREMBO mmoja ambaye alihu-dumu kwenye nyumba ya kulala wageni na baa (jina tunalo) iliyopo Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Blandina Michael (33) amekutwa amekufa kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo huku chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na vitendo vya ushirikiana. Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye pia anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa kafara mhudumu huyo. Ilidaiwa...

TASWIRA MBALIMBALI TOKA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA

Wajumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Ismail Aden Rage na Kheri Ameir wakibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuaharishwa kwa kikao jana mjini Dodoma hadi Ijumaa.   Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama (UPDP), Fahmi Dovutwa  na Mjumbe...

NYALANDU APANGUA WAKURUGENZI MALIASILI

Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewaondoa katika nyadhifa zao, Wakurugenzi mbalimbali kwa sababu zilizoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yao. Hatua ya Nyalandu imekuja ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Bunge la Desemba 22, 2013 lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza. Nyalandu...

HATIMAYE MTOTO MWENYE UVIMBE WA AJABU AKATWA MGUU NCHINI INDIA

Mtoto mwenye uvimbe wa ajabu, Hamis Liyuga akiwa anaandaliwa kupelekwa katika chumba cha upasuaji.    Hamis Liyuga akipelekwa katika chumba cha upasuaji.…   Mtoto mwenye uvimbe wa ajabu, Hamis Liyuga akiwa anaandaliwa kupelekwa katika chumba cha upasuaji.   ...Akiwa ndani ya chumba cha upasuaji. ...Akiwa chini...