Tuesday, February 25, 2014

MREMBO AFARIKI GHAFLA GUEST ARUSHA

MREMBO mmoja ambaye alihu-dumu kwenye nyumba ya kulala wageni na baa (jina tunalo) iliyopo Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Blandina Michael (33) amekutwa amekufa kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo huku chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na vitendo vya ushirikiana.
Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye pia anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa kafara mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa, kila mwaka mtu mmoja katika biashara zake hupoteza maisha ghafla. 
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alipoongea na Uwazi juzikati alikanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni muumini mzuri wa imani yake. 
‘’Hao watu wanapotosha sana, unajua kuna mwaka mwanaume mmoja alikufa ghafla kwenye nyumba yangu ya kulala wageni, alikuja na mpenzi wake ila alimeza Viagra ambazo hata polisi walizikuta mezani. 
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema. 
Kifo cha Blandina kilitokea ndani ya chumba huku mtu mmoja anayedaiwa kuwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Timo, mkazi wa eneo hilo akihojiwa na polisi. 
Marehemu Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga, anaelezwa na bosi wake huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa familia yake kwa vile alimwamini sana. Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa na tatilo la kiafya. Bosi huyo alisema mwili wa marehemu uligundulika baada ya mfanyakazi mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2 asubuhi ambapo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa ndipo alipoamua kwenda kumgongea katika chumba hicho. Alisema baada ya kufika alishangaa kukuta mlango wa chumba chake uko wazi na alipochungulia alibaini kwamba Blandina alikuwa amefariki dunia. Hata hivyo, polisi baada ya kufika na kuufanyia uchunguzi wa awali mwili huo hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote linaloashiria kuuawa, ingawa mwili huo ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

Related Posts:

  • Mlipuko waua 40, Nigeria Watu wapata 40, wameuawa katika milipuko mikubwa miwili iliyotokea katika mji wa Kaduna, kaskazini mwa Nigeria. Katika mlipuko wa kwanza wa kujitoa mhanga watu 25 waliuawa, huku wengine 15 wakiuawa katika eneo lililokuw… Read More
  • Thamani ya pesa ya Tanzania inazidi kushuka thamani, hii inasababishwa na material inayotengenezewa, kwa mfano noti ya shili mia tano imekosa muonekano wake kabisa. kwa maelezo zaidi www.zacott.blogspot.com … Read More
  • WEMA ASHINDWA KULIPA MAPIGO YA DANGOTI  Mwana mitindo maarufu na msaani wa bongo movie wema sepetu ameshindwa kujibu mapigo ya bwana wake diamond kwa kushindwa kumpa zawadi katika siku yake ya kuzaliwa kwake… Read More
  • REDD'S MISS TANZANIA 2014 KUFANYIKA MLIMANI CITY JUMAMOSI HIIMkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo,juu ya onyesho la Redd's Miss Tan… Read More
  • FILAMU YA 'THE KARATE KID' HATI HATI KUTOKA Filamu ya The Karate Kid iliyoigiwa na Jaden Smith na Jackie Chan imepata pigo baada ya muongozaji wa filamu hiyo kujitoa katika mradi huo. Waandaaji wa filamu hiyo wameeleza kuwa muongozaji Breck Eisner ametoka kweny… Read More

0 comments: