Afisa ushirika mkoa wa Iringa John Kiteve akifungua mkutano huo
Mwakilishi wa CRDB Iringa akifuatilia matukio katika mtandao huu
Mwakilishi wa benk ya CRDB Iringa Bw Bruno akiwahamasisha kujiunga na bima mbalimbali
Afisa ushirika mkoa wa Iringa John Kiteve akifungua mkutano mkuu wa Saccos ya Walimu Kilolo leo
Na Francis Godwin Blog
WANACHAMA wa chama cha kuweka na kukopa cha Kilolo Teacher’s Saccos wilayani Kilolo mkoani Iringa wametakiwa kujenga uaminifu katika kulipa madeni ya mikopo ambayo wamekopeshwa badala ya kugeuza ni sadaka kwao.
Hivyo aliwataka wanachama hao kujenga utamaduni wa kurejesha mikopo kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutumia mikopo hiyo kwa maendeleo badala ya kutumia mikopo kwa anasa ambazo zitakwamisha urejeshaji wa madeni ya mikopo yao.
Pia Kiteve alisema kuwa Saccos hiyo ya walimu wilaya ya kilolo ni moja kati ya Saccos ambazo zimekuwa zikifanya vema na kuwa tofauti na saccos nyingine za walimu nchini kutokana na utaratibu mzuri wa Saccos hiyo kuwaunganisha walimu wa shule za msingi na sekondari.
Hata hivyo alisema kumekuwepo na mafanikio makubwa katika chama hicho kwa chama kuongeza wanachama kwa kasi na kuwa na jengo lake pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na taasisi za kifedha hasa benk ya CRDB
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wanachama wa chama hicho wameendelea kunufaika na mikopo na kuwa hadi sasa wanachama 35 wamekopeshwa mikopo ya ununuzi wa vyombo vya usafiri yakiwemo magari manne na pikipiki 31,wanachama 343 wamepewa mikopo ya ujenzi wa nyumba za kisasa ,wanachama 156 wamekopeshwa mikopo ya masomo ya watoto wao na wanachama 28 wamepewa mikopo ya biashara na kilimo .(P.T)
WANACHAMA wa chama cha kuweka na kukopa cha Kilolo Teacher’s Saccos wilayani Kilolo mkoani Iringa wametakiwa kujenga uaminifu katika kulipa madeni ya mikopo ambayo wamekopeshwa badala ya kugeuza ni sadaka kwao.
Wito huo umetolewa
na afisa ushirika wa mkoa wa
Iringa John Kiteve wakati akifungua mkutano mkuu wa
mwaka leo mjini Kilolo.
Kiteve alisema kuwa wapo baadhi
ya wanachama wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiomba mikopo na
mara baada ya kupewa mikopo hiyo
wamekuwa wakishindwa kurejesha mikopo hiyo jambo ambalo linachangia vyama vingi vya ushiriki
na mikopo kuyumba hapa nchini.
“
wapo baadhi ya wanachama ambao si waaminifu wamekuwa wakichukua mikopo na
wakati wakihama wamekuwa wakihama na madeni ya saccos bila
kufika ofisini za Saccos na kueleza jinsi ambavyo
atarejesha mikopo hiyo.Hivyo aliwataka wanachama hao kujenga utamaduni wa kurejesha mikopo kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutumia mikopo hiyo kwa maendeleo badala ya kutumia mikopo kwa anasa ambazo zitakwamisha urejeshaji wa madeni ya mikopo yao.
Pia Kiteve alisema kuwa Saccos hiyo ya walimu wilaya ya kilolo ni moja kati ya Saccos ambazo zimekuwa zikifanya vema na kuwa tofauti na saccos nyingine za walimu nchini kutokana na utaratibu mzuri wa Saccos hiyo kuwaunganisha walimu wa shule za msingi na sekondari.
Hata hivyo alisema
ili kuondoa matabaka katika Saccos hiyo
ni vema wanachama wote kuwa kitu kimoja badala ya kuwepo kwa
matabaka kati ya walimu wa shule za msingi na Sekondari jambo ambalo
litaua nguvu ya Saccos hiyo.
katibu wa chama hicho Fabian Chavala alisema kuwa chama hicho
kilianzishwa mwaka 2007 na kupata usajili wake IR 465 kikiwa na
wanachama 60 wakiwemo wanaume 36 na wanawake 24 ila kwa sasa kina
wanachama 516 kati yao ni walimu wa shule za msingi ni 416 na
wengine waliobaki ni kutoka shule za sekondari.Hata hivyo alisema kumekuwepo na mafanikio makubwa katika chama hicho kwa chama kuongeza wanachama kwa kasi na kuwa na jengo lake pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na taasisi za kifedha hasa benk ya CRDB
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wanachama wa chama hicho wameendelea kunufaika na mikopo na kuwa hadi sasa wanachama 35 wamekopeshwa mikopo ya ununuzi wa vyombo vya usafiri yakiwemo magari manne na pikipiki 31,wanachama 343 wamepewa mikopo ya ujenzi wa nyumba za kisasa ,wanachama 156 wamekopeshwa mikopo ya masomo ya watoto wao na wanachama 28 wamepewa mikopo ya biashara na kilimo .(P.T)
0 comments:
Post a Comment