Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kusimama njiani akitokea wilayani
Makete akielekea wilayani Wanging"ombe, katika ziara yake maalum ya Mkoa
wa Njombe kuhusu Chama cha Mapinduzi kilivyopokea kifo cha mpigania
uhuru wa Afrika Kusini na mtu aliyeheshimiwa sana duniani Mzee Nelson
Mandela kama alivyojulikana kama "Madiba" aliyefariki dunia usiku wa
kuamkia leo ijumaa tarehe 6, Kinana amesema CCM inatambua jinsi Nelson
Mandela alivyoipigania nchi yake na Afrika kwa ujumla, kuikomboa
mikononi mwa ubaguzi wa rangi na kuiweka huru,…
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kusimama njiani akitokea wilayani
Makete akielekea wilayani Wanging"ombe, katika ziara yake maalum ya Mkoa
wa Njombe kuhusu Chama cha Mapinduzi kilivyopokea kifo cha mpigania
uhuru wa Afrika Kusini na mtu aliyeheshimiwa sana duniani Mzee Nelson
Mandela kama alivyojulikana kama "Madiba" aliyefariki dunia usiku wa
kuamkia leo ijumaa tarehe 6, Kinana amesema CCM inatambua jinsi Nelson
Mandela alivyoipigania nchi yake na Afrika kwa ujumla, kuikomboa
mikononi mwa ubaguzi wa rangi na kuiweka huru, Ameongeza kwamba CCM na
wanachama wake pamoja na watanzania wote watakumbuka mambo mema yote
aliyoifanyia nchi yake na Afrika kwa ujumla na kuyaenzi kwa vitendo.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Cchama cha Mapinduzi Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati akizungumza nao alipozungumzia kifo cha ayati
Nelson Mandela huko Wanging"ombe mkoani Njombe leo.
Katibu
Mkuu wa Cchama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara
baada ya kukagua shule ya sekondari ya Makete Girls iliyopo katika
kijiji cha Mtweve wilayani Makete leo akiwa njiani kwenda Wilayani
Wanging"ombe, kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi
na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh.
Josephin Matiro.
Mkuu
wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kukagua
sekondari ya Makete Girls katika kijiji cha Mtweve akiwa njiani kwenda
Wanging"ombe mkoani Njombe, Kutoka kulia ni Toto Timoth ambaye ametoa
tani tano ya mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo,Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Dr.
Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
akiongozana Hosea Mpagike Katibu wa CCM mkoa wa Njombe mara baada ya
magari kukwama njiani kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Hosea Mpagike Katibu wa CCM mkoa
wa Njombe wakisubiri magari yaliyokuwa yamenasa kwenye tope wakati
msafara ukielekea wilayani Wanging'ombe leo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kutoka kulia na
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wa pili pamoja na
waandishi wahabari wakitembea kwa miguu huku magari yakiwafuata mara
baada ya kuyanasua kwenye tope.
Mkuu
wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi akimkaribisha Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili
wilayani Wanging'ombe leo, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni
Mstaafu Aseri Msangi.
"Kweli
Bini ana Huruma" Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman
Kinana akizungumza na Bibi Geremana Mrwiro mwanakijiji ambaye alileta
jembe ili litumike kwa kusaidia kunasua magari yaliyokuwa yamekwama
kwenye tope.
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza katika kijiji cha Usuka kilipo kituo cha
Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima wilayani Wanging'ombe ambapo
Katibu mkuu wa CCM alitembelea vijana walioamua kujiunga pamoja na
kuendesha kilimo
Baadhi ya vijana hao wakinyanyua kadi zao juu ili kula kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa na Ndugu Abdulrahman Kinana leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi kijana Said Mkweta.
Utulivu wa kula kiapo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo
kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi kuhuso
moja ya Power Tiller itakayotumiwa na vijana hao kulimia shamba lao ili
kuwahi mvua zinazonyesha.
Gari
lililokuwa likitumiwa na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa likinasuliwa kwenye tope mara baada ya kuteleza na
kuingia kandokando ya mtari
Juhudi za kunasua zikiendelea.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata kulia Dr.
Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kushoto na
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakitoka nje mara
baada ya katibu mkuu huyo kuzindua jengo la kitegauchumi la CCM mkoa wa
Njombe leo ambalo limepangishwa na Wizara ya Fedha.
0 comments:
Post a Comment