Raia wa Afrika Kusini wako kwenye maombolezo kwa siku
ya pili hii leo wakiwa kwenye mkesha kwa usiku nzima kwa ajili ya
kuomboleza mpendwa wao Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela,
aliyeaga dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Watu wamekuwa wakikumbuka mema yake , wakicheza na kuimba Mbele ya makazi yake ya zamani mjini Soweto.Siku ya Jumanne, itakuwa ni siku ya shughuli maalum za maombolezo ya kitaifa ambapo shughuli hizo zitafanyika katika uwanja wenye uwezo wa kukusanya watu 95,000 ulio nje kidogo ya mji wa Johannesburg.
Raia wa Afrika kusini wakiwa kwenye maombolezo
Mazishi ya Mandela yatafayika jumapili ijayo tarehe 15 kijijini kwake alikokulia,Qunu.
Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 kabla ya kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.
Serikali yake iliondoa utawala wa kibaguzi wa watu weupe ambao ulikuwa na sera za kuwagawa watu wenye asili ya weupe na weusi.
Raia wa Afrika Kusini nchi nzima wamekuwa wakisali, wakiimba nyimbo za kupinga ubaguzi wa rangi na kuwasha mishumaa, wakikumbuka maisha ya Kiongozi wao na namna alivyo wavuta kwa mtindo wa maisha yake.
0 comments:
Post a Comment