Stori: Timoth Itembe, TARIME
MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya Nyamisangura, wilayani hapa, Eliza Marwa,28, hivi karibuni amenusurika kuuawa na mumewe, baada ya majirani kufika kumuokoa kutokana na kukatwakatwa mapanga.
TARIME
MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya Nyamisangura, wilayani hapa, Eliza Marwa,28, hivi karibuni amenusurika kuuawa na mumewe, baada ya majirani kufika kumuokoa kutokana na kukatwakatwa mapanga.
“Nilichukua jukumu la kwenda kwa kutumia nauli yangu kwa kuwa muda huo mume wangu alikuwa kazini na baada ya mazishi kesho yake asubuhi Desemba kumi na saba mwaka huu nilirudi nyumbani na kumkuta mume wangu ambaye alianza kunipiga kwa mpini wa jembe kisha panga akidai kuwa sikuwa nimeenda kwenye mazishi badala yake nilikuwa nimeenda kwa mpenzi wangu.
“Alinishambulia sehemu mbalimbali za mwili hususani kichwani, kidogo anitoe ubongo, wasingekuwa majirani kuniokoa baada ya kupiga yowe naamini angeniua kwani hivi sasa siwezi hata kuamka na masikio yameziba, miguu ina ganzi, siwezi kutembea.
“Mume wangu Ogora amekuwa akinipiga mara kwa mara lakini kutokana na watoto tuliozaa naye nimekuwa nikivumilia mateso, naogopa kuondoka na kuacha watoto walelewa na mama wa kambo,”alidai mama huyo.
Ogora hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani anasakwa na dola na afisa mmoja wa polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa. Naye daktari wa hospitali aliyolazwa mama huyo, Nega Malico alikiri kumpokea mgonjwa huyo.