WAPINZANI
wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri
wameonyesha wamepania kuhakikisha hawapotezi mchezo wa Jumamosi baada ya
kutua nchini na maji na baadhi ya vyakula ambavyo watapikiwa wachezaji
wao.

Habari za uhakika kutoka Cairo, zimeeleza Ahly wamebeba chupa za maji,
baadhi ya vyakula na kazi hiyo itafanywa na mpishi wao maalum raia wa…
WAPINZANI
wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri
wameonyesha wamepania kuhakikisha hawapotezi mchezo wa Jumamosi baada ya
kutua nchini na maji na baadhi ya vyakula ambavyo watapikiwa wachezaji
wao.
Habari
za uhakika kutoka Cairo, zimeeleza Ahly wamebeba chupa za maji, baadhi
ya vyakula na kazi hiyo itafanywa na mpishi wao maalum raia wa Ujerumani
ambaye amekuwa akisafiri na timu hiyo kwa misimu miwili sasa, kila
inapotoka nje ya Misri.
Mmoja wa Watanzania wanaoishi jijini Cairo, amesema waliondoka na
vifaa hivyo jana usiku na wanatarajia kuwasili Dar leo alfajiri na ndege
ya Egypt Air.
“Wamebeba kila kitu, wakati wanapita hapa airport, baadhi ya vitu
vyao vilishapita. Kwa kuwa sisi tuko hapa kazini, tulisikia wakisema
kuwa ni maji na vyakula kwa ajili ya wachezaji wa Ahly.
“Wachezaji walifuatia baadaye sana, hapa walikuja na basi maalum na
baadaye wakaingia ndani ya uwanja wa ndege. Wanaonekana wako fiti na
walikuwa wakitumia muda mwingi kutaniana na walionekana kuwa na furaha
tu,” alisema mpashaji huyo ambaye ameishi nchini humo kwa zaidi ya miaka
10 na anazungumza lugha ya Kiarabu kwa ufasaha.
Timu hiyo imekuwa ikibeba maji na vyakula ikiwa ni sehemu ya
kujiwekea tahadhari ya kuhujumiwa au kuhofia ubora wa maji katika nchi
husika wanayokwenda kucheza mechi yoyote ya kimataifa. Mfumo huo
hutumiwa pia na timu ya taifa ya Misri.
Hii si mara ya kwanza kwa timu za Kiarabu kufanya hivyo, Ahly iliwahi
kufanya hivyo ilipocheza na Yanga na kuifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar, mwaka 2008, pia Zamalek nayo ilifanya hivyo lakini ikapigwa
bao 1-0 na Simba, mwaka 2003.