This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, May 11, 2013

JESHI LA TANZANIA LATAMBA TENA.....LINASEMA KAZI YAKE NI MOJA TU AMBAYO NI KUWAFUMUA WAASI WA M23 HUKO KONGO


JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limesema limeanza kuwapeleka askari wake nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) kulinda amani na kuhakikisha wananyang’anywa silaha zote waasi wa kundi la M23 ili nchi hiyo itawalike.

Kutokana na hatua hiyo, JWTZ limesema halitishwi na vitisho vya M23 kutokana na kujiandaa vizuri kila idara, ikiwa ni lengo la kutaka kuona wananchi wa DRC wanaishi kwa amani, tofauti na sasa ambako kumekuwa na vitendo vya kinyama dhidi ya wanawake na watoto wadogo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, wakati wa kutoa tamko la jeshi hilo, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alisema kamwe hawatishwi na kundi la M23.

Alisema wanashangazwa na kitendo M23 kutoa vitisho, wakati askari wanaokwenda huko wanatoka nchi za Afrika Kusini, Malawi na Tanzania.

“Kwa nini iwe Tanzania pekee, sisi hatuwezi kutishwa na kikundi cha wanamgambo 1,000, tunasema tunakwenda kutimiza jukumu la Umoja wa Mataifa (UN) kuhakikisha DRC inatawalika na silaha zote wananyang’anywa,

“Tanzania tuna historia kubwa ya kuleta ukombozi na amani ndani ya nchi za Afrika, zikiwamo Commoro, Afrika Kusini, Liberia, Sudan na Lebanon, ndiyo maana vikosi vyote vitatu vinaongozwa na Mtanzania, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa.

“Tulipokwenda Commoro, tulihisi kama damu itamwagika lakini hali ilikuwa tofauti kabisa na isitoshe ni askari mmoja tu aliteleza na kuanguka majini, sasa hawa M23 wao wamepata wapi mafunzo.

“Itakumbukwa Idd Amin Dada, alikuwa anajigamba na kusema anataka kuja kunywa chai Dar es Salaam, lakini aliishia kuchungulia visiwa vya Ukerewe… majigambo ya M23 ni ishara ya kuanza kuwa na wasiwasi,” alisema Kanali Mgawe.

Alisema kikosi kilichoanza kwenda DRC,kinajulikana kama Tanzania Bataria One –DRC (TANZBATT-1 DRC) na kuongeza kwamba kila baada ya miezi sita kutafanyika mabadiliko kadri itakavyohitajika.

Alisema kutokana na vitisho hivyo, bado Tanzania ni salama na itakuwa kuwa salama na kuwataka Watanzania kuondoa hofu juu ya matukio yanayotokea hivi sasa.

Alisema vifaa vya askari, wanaokwenda Kongo vimekamilika na tayari UN imevifanyia ukaguzi na kuridhia vinakidhi mahitaji katika kuimarisha ulinzi na usalama.

Kuhusu mzozo wa Tanzania na Malawi, alisema nchi hizo bado zina uhusiano mzuri wa kidiplomasia.

Mapema wiki hii, Rais Jakaya Kikwete aliwakabidhi askari wa JWTZ bendera mkoani Pwani, ikiwa ni ishara ya kuanza safari ya kuelekea DRC.

VIDEO YA CHID BENZ ALIPOCHEZEA KICHAPO PALE MAISHA CLUB


 Jumapili hii kwenye ukumbi wa New Maisha Club, kulitokea ugomvi kati ya rapper Chidi Benz na Kalapina aliyekuwa na show yake pamoja na Kikosi cha Mizinga. 


Tukio lilitokea baada ya Chidi Benz kupanda ghafla kwenye stage na kumnyang’anya kipaza MC wa show hiyo wakati Nikki Mbishi alipokuwa kwenye stage. 

Baada ya kupanda juu, Chidi aliyekuwa amelewa alianza kuwaongelesha na kuwaimbia mashabiki waliokuwa wakimshangilia. 


“Naomba niongee kitu kimoja ambacho ninyi watu woote ambao mpo humu ndani mtasikiliza, au vipi, nimeingia na beibe beibe, nimeingia VIP halafu nimemuona Nikki Mbishi anachana hapa stage, Nikki njoo njoo Nikki njoo, sijui show ya nani kwasababu yako wewe nimekuona nilikuwa paleeee, nimepita nimekuja hapa nimekuona mdogo wangu, sasa nini sasa, piga keleleeee,” alisikika akisema Chidi huku watu wakimshangilia na baadaye microphone kuzimwa. 
 
Baadaye Kalapina alipanda kwenye stage na kuchukua microphone, “Oii ambaye hahusiki na show ashuke,” alisema Kalapina na kumfuata Chidi kisha kumpiga na kumwangusha chini. “Ninyi mnamwachia mtoto m*** apande kwenye stage,” alisema Kalapina wakati huo Chidi Benz aliyekuwa anataka kurudi tena kwenye stage kupigana akiwa ameshikiliwa na watu wa ulinzi.

VIDEO : CHID BENZ ACHEZEA KICHAPO KWA MARA NYINGINE  TOKA  KWA  KALAPINA 

ASKARI ALIYEMUUA MTOTO MDOGO WA RISASI AKAMATWA......CHADEMA WAANDAMANA, POLISI YAJIBU MAPIGO

ASKARI Polisi wa Kituo cha Tarime mkoani Mara mwenye namba D. 4662 Koplo Mathew, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za uzembe uliosababisha kifo kwa risasi cha mwanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Rebu, Deus Jacob (9).
Kifo hicho kilitokea wakati polisi wakiwa kwenye harakati za kukamata mtuhumiwa, Marwa Bisara, mkazi wa kitongoji cha Songambele kata ya Sabasaba mjini hapa, aliyekuwa akituhumiwa kwa shambulio na kudhuru mwili.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tarime/Rorya, Justus Kamugisha, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni katika kitongoji cha Songambele, baada ya Koplo Mathew na askari wenzake wakiwa na mlalamikaji, wakifuatilia mtuhumiwa na kumkuta na wenzake katika pagala wakivuta bangi.
 
Wakati polisi wakijiandaa kumkamata, mtuhumiwa Bisara alimvamia Koplo Mathew akitaka kumnyang'anya bunduki na katika purukushani hiyo, risasi zilifyatuka na moja kumpata Deus kichwani na kumuua papo hapo baada ya kichwa kufumuka.
Kamanda Kamugisha alisema chanzo cha mauaji ni mtuhumiwa Bisara kukaidi amri ya kukamatwa. Lakini mwenzake Julius Maseke (38) mkazi wa mtaa wa Ronsoti alikamatwa akiwa na misokoto 47 na kilo 3.25 za bangi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote.
 
Polisi ilitoa mwito kwa raia wema kutoa taarifa kwa vyombo husika watakapomwona Bisara na inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele alionya wanasiasa waache kulitumia tukio hilo kisiasa kwa kuwa marehemu Deus hakuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. 
Alionya hivyo kwa alichokisema ni baadhi ya wafuasi wa Chadema kuchocheana kufanya vurugu wakihamasishana kuchukua mwili wa marehemu huyo na kufanya maandamano kwenda Bomani ziliko ofisi za Mkuu wa Wilaya na Kituo cha Polisi.
 Hata hivyo, maandamano hayo yalizimwa na Polisi kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na mwili huo uko katika mochari ya hospitali ya wilaya na unatarajiwa kuzikwa leo.

NI USIKU WA HIP HOP NA MIC KING DAR LIVE MEI 25, 2013


wakazi wa dodoma waupokea kwa kishindo msimu mpya wa clouds Fm





























Thursday, May 2, 2013

CHEKA HANA MPINZANIA TANZANIA - AMKUNG'UTA MASHALI KWA KNOCKOUT


Bondia Fransic Cheka Kushoto akipambani na Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Cheka Kushoto akimshambilia kwa makonde ya nguvu Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya nne Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya nne Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUTraundi ya nne Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' akishangilia ushindi uku akiwa amebebwa juu juu kama mkungu wa ndizi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Cosmas Cheka kushoto akipambana na Charles Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba siku ya mei mosi Cheka alishinda kwa ponti mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akimsindikiza wakati wa kupigana bondia Ibrahimu Class 'King class Mawe wakati wa mpambano wake na amos mwamakula
Bondia Amos Mwamakula kushoto na Ibrahimu Class 'King Class mawe' wakisubili matokeo ambapo class alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Thomas Mashali kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Cheka katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT



Shomari kimbau akiwa na Cheka baada ya kumvisha ubingwa wa IBF Africa aliokuwa akiutetea
Kotoka kushoto ni Kocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' mdau ambaye ajajulikana jina Mtaalishaji wa mpambano kati ya Fransic Cheka Vs Thomasi Mashali Adamu Tanaka 'Tunaluza' na MC wa mpambano huo COOL p
Rashidi Mhamila 'Ngade akiwa amepozi na Bady Boy wakati wa onesho hilo

SHEREHE ZA MEI MOSI ZILIVYOFANA MKOANI SHINYANGA

 Burudani za ngoma za asili za Kisukuma na nyimbo za taarab kutoka kwa walimu zilifanikisha vilivyo sherehe za Mei Mosi mkoani Shinyanga jana.…
 Burudani za ngoma za asili za Kisukuma na nyimbo za taarab kutoka kwa walimu zilifanikisha vilivyo sherehe za Mei Mosi mkoani Shinyanga jana.
 Mwenyekiti wa TUICO mkoa wa Shinyanga, Bw. Fue Mrindoko akimkaribisha Mhe. Ali N. Rufunga kuzungumza na wafanyakazi waliofurika katika uwanja cha Jamhuri mjini Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Rufunga akihutubia wafanyakazi jana katika uwanja wa Jamhuri wilayani Kahama.
 Maandamano ya wafanyakazi yakiongozwa na bendi wakati wakipita mbele ya mgeni rasmi, mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Ally N. Rufunga jana katika uwanja wa Jamhuri Wilayani Kahama sherehe hizo zilipofanyika kimkoa.
(Picha na Magdalena Nkulu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga)