Na Mwandishi Wetu
MCHEKESHAJI wa Kundi la Mizegwe, Rashid Coster ‘Maringo Saba,’
anadaiwa kumfumania mkewe anayefahamika kwa jina la mama Zai kisha
kuamua kunywa sumu ikisemekana kuwa alitaka kujiua kwa hasira.
Chanzo
makini kilichoomba hifadhi ya jina kimenyetisha kuwa, Maringo Saba
aliandaa mtego wa fumanizi baada ya kuhisi mkewe anamsaliti kwa rafiki
yake anayefahamika kwa jina moja la Sam.
Chanzo hicho kilizidi
kushuka na mistari kwamba, baada ya staa huyo kuandaa mtego, ulizaa
matunda Jumatano ya Machi 20, mwaka huu ambapo alimfumania mkewe
akijivinjari na jamaa.
Sosi huyo alizidi kubainisha kuwa, mke wa
Maringo Saba alipoona mumewe amemjazia umati kwa fumanizi hilo, alitimua
mbio kwa vile ilidaiwa Maringo Saba alitishia kumfanyia kitu mbaya.
“Ilikuwa vurumai,…

“Ilikuwa
vurumai, watu waliokusanyika kufanya fumanizi walimtembezea kichapo Sam
kabla hajafanikiwa kuchoropoka kwenye himaya ya chumba hicho na
kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mwananyamala CCM,” kilisema
chanzo.
Chanzo kingine kilicho karibu na mchekeshaji huyo (jina
lipo) kilidai kuwa, baada ya tukio hilo, Maringo Saba alikutwa chumbani
kwake amezidiwa ndipo ndugu zake walipomkimbiza kwenye Hospitali ya
Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za
madaktari, imedaiwa kuwa staa huyo alikutwa na kiasi kikubwa cha sumu
mwilini ambayo haikujulikana mara moja ni ya aina gani.
Mara baada ya
taarifa hizo kutua kwenye dawati la Amani, waandishi wetu walifika
Hospitali ya Mwananyamala na kumkuta mchekeshaji huyo akiwa amewekewa
dripu za dawa huku ndugu zake wakisema jamaa alichanganya pombe na dawa
na siyo sumu kama ilivyodaiwa.
“Ndugu yetu hakunywa sumu,
alichanganya dozi ya malaria na pombe ndiyo maana alizidiwa ghafla,”
alisema mmoja wa ndugu hao aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Khalfan.
Hata
hivyo, maelezo ya Rashid yalipingana na ya baadhi ya wauguzi wa
hospitali hiyo ambao kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini
walikiri msanii huyo kukutwa na sumu mwilini.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa
wa Mwinjuma, Allen Mwakitalima alikiri kuwepo kwa fumanizi, lakini
kuhusu kunywa sumu alisema alisikia kwa watu mtaani ingawa kwake
hajafikishiwa taarifa rasmi.
“Habari za fumanizi kwa Maringo Saba
lilifika kwangu kiofisi, hata polisi walishakuja kuniulizia, ila kuhusu
kunywa sumu nilisikia kwa watu mtaani, lakini sijapata taarifa rasmi
kutoka kwa mjumbe wake, kwa hiyo likinifikia nitalishughulikia kiofisi,”
alisema mwenyekiti huyo.