
Katika Barua iliyoandikwa na ZFA Machi 4, mwaka huu, , iliyoisainiwa na Makamu wa Rais Kisiwani Unguja, ambaye pia ni Kaimu Rais wa ZFA kikatiba, Alhaj Haji Ameir, ikiwa na Kumbukumbu namba. ZFA/PRESIDENT/VOL.11/05.
Barua hiyo inasomeka Kamati ya Utendaji ya ZFA Taifa, imekaa na kujadili kwa kina ombi la kujiuzulu kwa Makungu, na kutafakari kwa makini na hatimaye kufikia uamuzi wa kulikubali ombi hilo.
ZFA Taifa imemshukuru Aman Makungu kwa msaada wake alioutoa huku wakimuomba aendelee kuwa na chama hicho wakati wowote atakapohitajika.
Nakala za barua hiyo zimetumwa kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo la Zanzibar pamoja na Msaidizi Katibu ZFA Kisiwani Pemba.
Kwa mujibu wa Katiba ya ZFA, sasa ni wazi kuwa kunalazimika kufanyika uchaguzi mwingine ndani ya siku 90.
Itakumbukwa kuwa miezi miwili iliyopita, Rais wa ZFA, Aman Ibrahim Makungu aliandika barua ya kuomba kujiuzulu nafasi hiyo kwa kile kilichoelezwa katika barua hiyo kuwa ni








.jpg)






