FERGUSON ASUSIA WANAHABARI KISA KADI NYEKUNDU
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson hakuwa tayari kuzungumza na vyomb vya habari ,baada ya timu kusukmwa nje ya ligi ya mabingwa barani ulaya Dhidi ya Real Madrid katika uwanja wa
Old Trafford.
Ferguson alishindwa kumvumilia mwamuzi kutoka uturuki Cuneyt Cakir baada ya kumpa kadi nyekundu Nani baada ya kumfanyia rafu mbaya Alvaro Arbeloa
katika dakika ya 56 wakati United ilikuwa ikongoza kwa goli la kujifunga la Sergio Ramos's.
Kocha msaisizi wa United Mike Phelan
alimwakilisha Feg katika mahojiano baada ya mechi kumalizka : "Chumba cha kubadilishia sio salama kwetu Kocha mkuu amekasirsihwa na maamuzi ya mwamuzi wa leo ndio maana hayuko hapa .
na mimi ndiye nitakaye zungumza
"Sidhani kama mkufunzi mkuu atakuwa sawa kuzungumza .
Naongea haya ili muone ni kwa jinsi gani tumesikitishwa hii ni klabu kubwa duniani ."
Phelan : "Tumesikitishwa na kuumia sana tuna mashaka kwanini limetokea na kwa sababu gani limetokea .
sio rahisi mkiwa kumi kiwanjani mkacheza na real Madrid .
" Waamuzi wapo kiwanjani ili kufanya Maamuzi lakini unatakiwa kufanya maamuzi ya maana .
Najua vyombo vya habari na watazamanji duniani kote wametazama hili na watakuwa na maoni tofauti lakini tumesikitishwa sana."
NDOTO ZA MACHESTER UTD KUTWAA TAJI LA ULAYA ZAISHIA KATIKA MJADARA MKUBWA ULAYA
Ndoto za Manchester United's kutwaa ubingwa wa ulaya zimemalizka kwa mjadara mkubwa huku kocha Man u Sir Alex Ferguson na wachezaji wakikiona kiwanja cha OT ni Kikubwa kuliko wakati mwingine.
United walionekana tayari wameanza kuingia hatua ya Robo fainali mara baada ya kipindi cha pili Kuanza huku Real Madrid's ikijitia matatani mara baada ya Sergio Ramos's kujifunga mwenyewe na kuipa goli United ambalo ilikuwa likichagizwa na sare ya goli moja kwa moja katika mchezo wa kwanza uliofanyika Bernabeu.
Lakini mchezo ulibadilika baada ya Mwamuzi kutoka Uturuki Cuneyt
Cakir's Kumlima kadi nyekundu Luis
Nani baada ya kumchezea vibaya Mchezaji Real Madrid Alvaro Arbeloa
katika dakika ya 56 - kadi ambayo iliwanyong'onyesha wachezaji wa
United .
Vijana wa Jose Mourinho's , waliongeza bidii , na kutumia pengo la hilo ambapo mchezaji wa zamani na kiungo wa Tottenham Luka Modric na kijana wa zamani wa Timu hiyo Cristiano Ronaldo walitumia dakika sita kusawazisha na kufunga goli la ushindi na kusonga mbele katika hatua Robo fainali .
Baada ya luis Nani Kupewa kadi nyekundu Ferguson's alinoneka kuto kuamini kinachotokea na kumshutumu mwamuzi kuwa hakutenda haki baada kutolewa mchezaji wake .
Mourinho sasa atakuwa analisaka taji la tatu la ligi ya mabingwa barani ulaya
akiwa na klabu tatu tofauti wakati Manchester utd wanatakiwa kujikita
katika makombe ya nyumbani ambapo jumapili watakuwa wakipambana na chelsea katika kombe Fa huku wakiwa wanaongoza alama 12 dhidi ya bingwa mtetezi Manchester city .
Huenda mwaka huu ukawa kama 1996, ambapo England haikuwa na timu
yoyote kwenye hatua ya robo fainali, kwani Chelsea na Manchester City
walishatolewa na Arsenal wapo ukingoni wanapoelekea Ujerumani wiki
ijayo.
Baada ya mechi Rio Ferdinand alimwendea mwamuzi na kujidai kumpigia makofi kana kwamba anampongeza, bila shaka kuonesha kuudhiwa na uamuzi wake wa kumpa kadi nyekundu Nani, na pengine kuwanyima penati kadhaa walizodhani walistahili.
Baada ya mechi Rio Ferdinand alimwendea mwamuzi na kujidai kumpigia makofi kana kwamba anampongeza, bila shaka kuonesha kuudhiwa na uamuzi wake wa kumpa kadi nyekundu Nani, na pengine kuwanyima penati kadhaa walizodhani walistahili.
0 comments:
Post a Comment