This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, March 5, 2013

Kiwanda cha sukari cha Mahonda visiwani Zanzibar kuzalisha Tani 400 za Sukari safi ikiwa ni sawa na Tani 40 kwa siku.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiangalia waya wa umeme aina ya shaba ambao amezuia mauzo yake hadi uongozi wa kiwanda cha sukari utapokaa pamoja na Wizara ya fedha kufikia maamuzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiuagiza Uongozi wa Kiwanda cha sukari Mahonda kukaa pamoja na Wizara inayosimamia Fedha Zanzibar ili kufikia mwafaka wa matumizi ya waya wa umeme wa aina ya shaba ambao tayari ulikuwa umeshauzwa.  
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea kiwanda cha sukari Mahonda akiwa pamoja na Uongozi wa Kiwanda hicho. Picha na Hassan Issa –Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

Polisi wasaka wauaji wa kigogo UVCCM

eshi la Polisi mkoani Arusha linawasaka wanawake wawili kufuatia kifo cha kutatanisha cha mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa kupitia Mkoa wa Arusha, Benson Peter Mollel (26). Inadaiwa kuwa wanawake hao walikuwa na Mollel kabla ya kufariki dunia ghafla juzi katika chumba cha hoteli moja jijini hapa. Tukio hilo lilitokea mchana baada ya mwili wa merehemu kugunduliwa na wahudumu wa hotel hiyo walipotaka kukifanyia usafi chumba alichokuwa amelala marehemu huyo . Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa marehemu alifika hoteli hapo, Machi 2 mwaka huu jioni na kupanga katika chumba namba 208. Alisema Polisi baada ya kupata taarifa za tukio hilo, wanaendelea na msako kuwatafuta wanawake hao ambao walikuwa na marehemu kabla ya kukutwa na mauti ya ghafla. Alisema kuwa mmoja wa wanawake hao alikwenda na marehemu hotelini hapo saa 7.00 usiku na mwingine alikwenda hotelini hapo asubuhi saa 5.00 asubuhi. Sabas alisema polisi baada ya kufika hotelini hapo walimkuta marehemu na kuchukua mwili wake na kuhifadhi hospitali ya Mkoa Mount Meru.

Monday, March 4, 2013

SIMBA CHALI ANGOLA, JAMHURI YATIA AIBU, AZAM FC YAIKOA TANZANIA KWA USHINDI MZITO SUDAN - SASA KUKUTANA NA BARRACK Y.C.II YA LIBERIA

shindi wa 5-0 dhidi ya Al Nasri Juba ya Sudan Kusini, umeipa Azam FC nafasi ya kuingia hatua ya pili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa timu hiyo kwa jumla ya magoli 8-1.

Azam FC inashiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imefanikiwa kuvuka hatua ya awali na kuingia hatua ya pili ambapo zimesalia timu 36.

Azam FC imefikisha idadi hiyo ya magoli baada ya kupata ushindi wa 3-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita na leo wakacheza mechi ya pili kwenye Uwanja wa Juba nchini Sudan Kusini na kupata ushindi mnono wa 5-0 wakiwa ugenini na kufikisha jumla ya magoli 8-1.

Kwa timu za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya CAF, ni Azam FC pekee iliyosalia baada ya timu za Simba SC kutolewa na Recreativo Libolo ya Angola kwa jumla ya magoli 5-0, na Jamhuri ya Pemba nayo ikatolewa na St. George ya Ethiopia kwa kipigo cha jumla cha 8-0 zote zilikuwa zinacheza Klabu Bingwa Afrika.

Azam FC wanabaki kuwa wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya CAF, watakutana na mshindi kati ya Barrack Y. C. II ya Liberia na Johansens ya Sierra Leone.

Katika mchezo wa leo ambao Azam FC walipata ushindi wa 5-0, magoli yalifungwa na Khamis Mcha magoli matatu ‘Hat Trick’, John Bocco na Salum Abubakar wamefunga goli moja moja.

Azam Fc katika mchezo wake wa kwanza ilipata ushindi wa 3-1 magoli ya Azam FC yakifungwa na Abdi Kassim na Kipre Tchetche aliyefunga magoli mawili.

Kikosi kamili cha Azam Fc kitarejea nchini kesho kwa maandalizi ya mchezo wao mwingine wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa kati ya Machi 15-17 mwaka huu.

AZAM YAPONGEZWA KUITOA TANZANIA KIMASOMASO MICHUANO YA AFRIKA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa timu ya Azam ya Tanzania Bara kwa kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho iliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Ushindi wa jumla ya mabao 8-1 ambao Azam imeupata dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini si fahari kwa timu hiyo tu, bali Tanzania kwa ujumla, na unaonyesha jinsi klabu hiyo ilivyojipanga kiushindani katika michuano hiyo ya Afrika.

Hata hivyo, ni vizuri Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, benchi la ufundi na wachezaji wa timu hiyo wakautazama ushindi huo kama changamoto kwao kuhakikisha wanajipanga vizuri zaidi kwa raundi inayofuata.

Timu ya Azam inayofundishwa na Mwingereza John Stewart Hall ilishinda nyumbani mechi ya kwanza mabao 3-1, na jana kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 ugenini jijini Juba.

Kwa kufanikiwa kuing’oa Al Nasir Juba, Azam sasa watacheza raundi ya kwanza (raundi ya 16 bora) ya michuano dhidi ya Barrack Y.C.II ya Liberia ambayo katika raundi ya awali iliitoa Johansens ya Sierra Leone. Barrack ilishinda bao 1-0 nyumbani katika mechi ya kwanza na kulazimisha suluhu katika mechi ya marudiano jijini Freetown.

Azam itaanzia mechi hiyo ugenini kati ya Machi 15,16 na 17 mwaka huu wakati mechi ya marudiano itachezwa Tanzania kati ya Aprili 5,6 na 7 mwaka huu.

Sunday, March 3, 2013

KITENDO CHA IRENE UWOYA KUYAANIKA " MAKALIO YAKE" NI SAWA NA KUWATUSI MASHABIKI WAKE

Huu  ni  upotofu  mkubwa  wa  maadili  unaoendekezwa  na  hawa  wanaojiita  MASTAA.....

Kumbukumbu  zangu  zinaniambia  kuwa  Uwoya  ni  mzazi  wa  mtoto  mmoja  ambaye  walizaa  na Ndikumana  na hatimaya  wakaachana  baada  ya  kushindana  kitabia...

 
 Swali  la  kujiuliza  ni  kwamba, Anajisikiaje  kuyaanika  matako  yake  kwa  mtoto  wake  wa  kumzaa???...Atajenga  msingi  upi  kwa  mtoto  wake  akikua????.....

Achilia  mbali  mtoto  wake, vipi  juu ya  
wazazi wake, wadogo  zake, shemeji zake na  ndugu  na  jamaa???...

Irene jitambue.....umri  umeenda  sasa...unayoyafanya  hayaendani  na umri  wako.....


Umaarufu  hauji kwa  kukaa  uchi.....Wapo  akina  Lady  jaydee, Monalisa....Ni wasanii  maarufu  pengine kuzidi hata wewe....kwa nini  usiige kutoka  kwao


Kitendo  hiki  ni  sawa  na  kuwatusi   watazamaji  wa  filamu  zako



 

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI



l 001 c4e42
l 002 87d6b
l 003 05ef7
l 004 11d7d
l 005 e0ac8
l 006 8bfd9
l 007 c9975
l 008 c1da8
l 009 7bff5
l 010 49daf
l 011 2fffd
l 012 0155e

UMEZISOMA HIZI?