CHAZA NA PWEZA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiKBEuEa_Vm8HdK8d3ALZm1HbG6lnx4aNrSQNx-xpRQ1fRwK9BZab8jxMTkTNEVEq2vo111DMuS4gmObRJUyeEM4Ia16TR0Ru2MxhUBZmw49kTgIbCqhc-Zo_eVf3uSztZXFDfUtQlnFaQ/s400/prog.jpg)
POMEGRANATE
Ni
aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa
kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili
na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa
kubwa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsXLkhTINiIdidLpR25aaPFNqIAivJcOKbkuDX_2ETiyu-mesDRcUW3BUhodPqBP_hl9n3COCruMkYMRv8yUklTVapZDvEnPLZbFQIXsts7x-RlN6d5kRISTLu-Q_J9zVmBoNpZAmpbvQ/s400/1.jpg)
Tatizo
la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa
na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4
kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo
hili.
Aidha
wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume
na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa
uchunguzi kubaki na asilimia 13.
Pamoja
na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na
kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha
kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya
sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa
kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini
aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya
kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa
usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya
mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale
wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si
kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdNSjf-2vKBOdt9RSmSW_SS7oGCBmOqtAUOtmyWS127BlcCs_8wqPgI00wy3-MbOSlDXpIgLyqwdeJZfpnDNH9k-D08cS8cE6x5hHZ7njcFIuEJ5HXo4ehEx-UhUIxYK5-U1Gc7KwHhr0/s400/pili.jpg)
PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya
tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha
vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa
watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi
na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi
sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa
kujamiiana.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVUl0YYxcy7a5mnvhbDPS0zH2YZyPj3fQ_pcDlBaKbpEFAeIfqnEz8XSIWGVHUEfirWt4-eFKWmCzjsvpJH6CM4N4tpTkEbCAiKVQDu4eUHz9a-YGct3IMfYdrslsCF3Gkg8mtO368uyU/s400/ova.jpg)
NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza
juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na
yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu
unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa
hodari katika tendo la ndoa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjAAgxrR15T9LPL3VDeUqXO2AoskWrb3trl_kC0T5KtwVTRcd9cga5fNc1q886U6sscZrrWSmcemxfX_OSqAFmLYjYgUPiIfXvIuYWmlTNSE19YhQhROiRTlCVf5iSiKcJS4fFxoPbPiGQ/s400/banana.jpg)
CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu
anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake,
jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya
mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa
mawazo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-KyKaXIZFB3Yv0z3b_k6LUaoPzCAARogPQTaHqoLN9gQVjEKiB6_DJzPOe-aJbgi0ZrGOJjCTpbUsbJxFkUGCeSQqCwXuzrD7lc_diPa7wxY8WvWRH64Dxp0WwUtlOGxRgIwB_TqtFcA/s400/choxh.jpg)
MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na
kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na
baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao
wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjaZy15A4FCScBGrXKYDVLISpWdzfSxGGu76osQ-0a-FiyUweTiXDI8TniWSua1A9GpxpJ-i09pbZCQDTD2lZizeikuUNkxuEVROjoyLYFgK7aqpafcvXmcNqTBYa6FNp0X_SqpcUh0Pm8/s400/mvinuo.jpg)
MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga
husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya
njema.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiFRRZw5LE9wdmjueg00Qte6JzaQSwfK-iH2j_Ebn1Hi1jvD29ADK8KqzZGKvQcMkzFpFbEH2FDRwFdRHXh0l5DjyoBULe1x_RLFSJm3qCBru7FCx73SxkeMeWMeHJ0udPs9V4YXv_CaZg/s400/seeds.jpg)
VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjLbW-ojHvYA_X7nAiqlUdVUPqD3o9pgGUZhaXbrpWsJFkTH6GvHQUMjfETcZb_-mGHK5bXixYlZYRGcazodyEdQY6msumShgDoRSMVk0WYDnNJsA-Jb22Kkz6PM4JEIOlV403KRpNUuAE/s400/vanilla.jpg)
Mwisho
wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na
virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za
kutosha kufanya tendo la ndoa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZu066KH5smkCAdMWwingd1FDPSeAgGzbAwMn0CKlIVZc61oG79tPk0n-JyCtRZoCn6vtY1yBlw_Gbc9jGMfQKfgjPZNavb6dTlQXd63GnyPM2I3caDD3BIx_7b26AaIUR4napBA7JniA/s400/tikimaj.jpg)
0 comments:
Post a Comment