Friday, July 26, 2013

HII NDO HALI HALISI YA MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTER ALIYEMWAGIWA TINDIKALI


MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. 


Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

 Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki. Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.

 Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.

 Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake

Related Posts:

  • HEADLINES ZA HABARI ZA MICHEZO DUNIANI. RAFAEL BENITEZ VS JOHN TERRY  Nahodha wa Chelsea John Terry na kocha wa muda wa club hiyo Rafael Benitez wameripotiwa kuwa kwenye mzozo mkubwa kufuatia ugomvi ulioibuka kwenye kiwanja cha mazoezi cha club hiyo Cobh… Read More
  • ZAIDI YA ABIRIA 50 WA BSI LA SUMRY LITOKALO SUMBAWANGA KUJA MBEYA LIMEPATA AJALI MAENEO YA SONGWE MPAKANI MWA WILAYA YA MBOZI CHANZO CHA AJALI HIYO NI KUWA ROLI LA MIZIGO LA KAMPUNI YA KANJILAJI LILIKUWA LINAIPITA GARI NYI… Read More
  • HII NDO TUME YA WATU 15 ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana Jumamosi, Machi 2, 2013 amezindua Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na kuwataka wajumbe wa T… Read More
  • TCU INAHUSIKA JE NA UBOVU WA MATOKEO YA KIDATU CHA NNE Hoyce Temu akifundisha katika moja ya shule huko Iringa hivi karibuni alipokuwa huko kuandaa vipindi vya mimi na Tanzania Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) inatakiwa isibakie tu kuthibitisha kuwepo kwa vyuo vikuuhapa … Read More
  • ziara ya mwenyekiti wa uvccm taifa morogoro Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Hamis Sadifa Vijana machacahari Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walioihama Chadema hivi karibubi, wakiserebuka nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro, baada ya msafara wa Mwe… Read More

0 comments: