Monday, June 24, 2013

WABUNGE NA MASHOGA WATETA.....HOFU YA KUWA NA RAIS SHOGA TANZANIA YATANDA


WABUNGE wanachama wa Chama cha Kupambana na Ukimwi (TAPAC), wiki iliyopita walikutana na kujadiliana mambo mbalimbali na mashoga katika mkutano wa mwaka wa chama hicho uliofanyika kwa muda wa siku tatu mjini  Dodoma. Katika mkutano huo, baadhi ya wabunge walionyesha wasiwasi wa taifa kupata rais shoga katika miaka ijayo kutokana na ongezeko la mashoga hapa nchini.

Mbali na wasiwasi ulioonyeshwa na wabunge, mashoga waliokuwa wakihudhuria mkutano huo, walilalamikia vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa na wanajamii wenzao na kudai watambulike na wapatiwe huduma za msingi za kibinadamu.

Akizungumza katika mkutano huo uliomalizika jana, Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy (CCM), alitahadharisha uwezekano wa nchi kupata rais shoga katika miaka ijayo, iwapo hatua za makusudi za kudhibiti hali hiyo hazitachukuliwa.

“Tabia ya kuwapeleka watoto kwenye shule za mabweni wangali wadogo wa umri wa miaka hadi miwili, itatuletea matatizo baadaye.

“Katika shule nyingi za bweni vitendo vichafu vinafanyika, vikiwamo vya ushoga. Katika vyuo vikuu hivi sasa kuna mashoga wasiopungua 40,000. Hii ni hatari, tusipojihadhari tutakuwa na rais shoga katika miaka ijayo,” alisema Kessy huku akishangiliwa na wabunge.

Mbunge huyo alitaka elimu dhidi ya ushoga na athari zake ienezwe nchini kupitia vyombo vya habari na nyumba za ibada.

Naye, mmoja wa mashoga waliohudhuria mkutano huo aliyejitambulisha kwa jina la Abdilah Ally, alieleza kuwa yeye ni shoga mwenye wanaume watatu lakini amekuwa akikutana na vitendo vya unyanyasaji kutoka ndani ya jamii inayomzunguka.

“Tunataka haki zetu. Tunanyanyaswa katika jamii hasa na polisi. Na sisi tunastahili huduma bora za afya na nyingine tuweze kujikinga na Ukimwi,”
alisema Ally, mkazi wa Dar es Salaam.

Wakati huo huo, taarifa iliyotolewa na Mshauri wa Masuala ya Ufundi wa Kampuni ya Jhpiego, Dk. Augustine Hellar, ilieleza kuwa kuna wanaume 397,458 waliotahiriwa nchini hadi Mei, mwaka huu katika mpango maalumu wa tohara kwa ajili ya kupambana na maradhi ya Ukimwi.

Dk. Hellar alitoa takwimu hizo alipowasilisha mada kuhusu tohara ya hiari kwa wanaume katika kukabili maambukizi ya Ukimwi nchini.

Alisema lengo la mpango huo ulioanza kutekelezwa Oktoba, 2011 katika baadhi ya mikoa nchini ni kutoa tohara kwa wanaume milioni 2.8 kila mwaka mmoja.

Alisema mpango huo umekabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo ya watu wazima ambao ndiyo walengwa kutojitokeza kwa wingi na baadhi ya watu kuhusisha hatua hiyo na upotevu wa nguvu za kiume.

Related Posts:

  • JB ATOA SOMO KWA WATANZANIA Na Mwandishi Wetu BONGE la Bwana, Jacob Steve ‘JB’ amewataka Watanzania kuwa na wivu wa kimaendeleo ili kuweza kufika mbali kisanaa kwa kuiga mazuri. JB alifunguka hayo muda mfupi baad… Read More
  • HUU NDIO UNDANI YA MARIDHIANO YA TFF NA SERIKALI KUHUSU UCHAGUZI WA TFF HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, zimekubaliana ujumbe kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) … Read More
  • MJADALA: ZIDANE, INIESTA NANI ZAIDI? MJADALA: ZIDANE, INIESTA NANI ZAIDI? ZINEDINE Zidane ni mmoja wa wachezaji wenye kipaji cha aina yake waliowahi kucheza soka akiwa na Ronaldo De Lima. Akiwa na umri mdogo, Zidane alikuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza ma… Read More
  • SANDRA AITETEA NDOA YAKESandra alifunguka hayo kupitia Stori 3 ambapo alisema taarifa hizo ndizo zilimpa hata mkosi kwani zilipoanza kuvuma ndiyo kipindi ambacho alipata ajali ya gari. “Sijawahi kuachwa, mimi pamoja na familia yangu tunafurahia … Read More
  • DIAMOND: NIMEMTUNDIKA MIMBA PENNY Diamond akipozi na Penny. Kwa mujibu wa Diamond, ni kweli yeye na Penny ambaye ni presenta wa Kituo cha Runinga ya DTV wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kabla hata ya ndoa waliyopanga siku zijazo. Diamond ali… Read More

0 comments: