This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, February 21, 2014

Kilichosemwa na Mh.Membe kuhusu Mgogoro wa Mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

membeTanzania bado ipo kwenye mgogoro na nchi ya Malawi juu ya mpaka halisi wa nchi,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Benard Membe amesema hatma juu ya mgogoro huo inategemewa kutolewa mwezi march.
Hukumu hiyo itaamuliwa baada ya jopo la Usuluhishi litakapokaa na kusikiliza pande zote mbili ambalo litaongozwa na Rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chisano
Kupatikana kwa suluhu ya mgogoro wa mpaka huo kutawatoa hofu wananchi wanaoishi pembezoni mwa Ziwa hilo ambao wamekuwa wakitegemea shughuli za uvuvi wakiwemo wakazi wa kijiji cha Manda Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.
Wakazi wa eneo hilo wamesema kwa hivi karibuni tangu kutulia kwa vuguvugu la mgogoro huo wamekuwa wakiendelea shughuli zao za maendeleo kama kawaida ikiwemo uvuvi.
malawi

Alichosema Mbwana Samatta kuhusu Mrisho Ngassa

Home » General News » Alichosema Mbwana Samatta kuhusu Mrisho Ngassa Alichosema Mbwana Samatta kuhusu Mrisho Ngassa Posted by: TZA Sports February 20, 2014 General News, Michezo 44 views TP_MAZEMBE_SAMATA_280912Mshambuliaji wa kimataifa mtanzania anayekipiga TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mtanzania Mbwana Samatta, amesema Mrisho Ngassa wa Yanga amefanya kitu cha maana kwa kupiga ‘Hat-Trick’ mbili mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Samatta alisema idadi hiyo ya mabao si kazi rahisi kwenye mashindano makubwa kama hayo. Yanga iliifumua Komorozine ya Comoro mabao 12-2 na kuiondosha kwenye mashindano na sasa itaikabili Al Ahly ya Misri ambayo Samatta amesema si timu ya ajabu lakini si laini kama hakuna mipango ya maana. Akizungumza na Mwanaspoti kwa simu kutoka Lubumbashi, Samatta alisema: “Mabao sita ni mengi sana kufunga katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ni dalili nzuri kwake na kwa timu. “Pia yanaashiria mambo mazuri kikubwa, lakini asibweteke kwani anaweza kufanya kitu kikubwa katika mashindano hayo endapo Yanga itafanikiwa kusonga mbele. “Ngassa ni mchezaji mzuri na mwenye uzoefu, kwangu sioni kitu cha ajabu sana kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja kwa sababu nafahamu uwezo wake, lakini inaashiria pia kwa sasa yuko vizuri sana kimwili na kiakili.” Kuhusu Yanga na Al Ahly, Samatta alisema: “Al Ahly ni timu kubwa na kama ulivyoona ni mabingwa, lakini mpira ni mchezo wa ajabu, nina imani kama Yanga watajituma, wanaweza kuwavua ubingwa na wao wakasonga mbele.” Mazembe nayo imo kwenye michuano hiyo na inajiandaa na mechi dhidi ya Astres de Douala ya Cameroon. Kuhusiana na mchezo huo, Samatta ameweka wazi kuwa maandalizi yao ni ya nguvu.

TP_MAZEMBE_SAMATA_280912

Tuesday, February 11, 2014

ujenzi wa jengo linalochungulia Ikulu

IGOGO wa Wakala wa Majengo (TBA), Makumba Kimweri na Richard Maliyaga walioruhusu ujenzi wa jengo linalochungulia Ikulu wamehukumiwa kwenda jela miaka 9 kila mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni 15 kila mmoja na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar!
Maofisa hao wa serikali kwa sasa wapo mahabusu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo ndugu na jamaa wanaangaika kutafuta fedha za kuwalipia dhamana.
VIGOGOVigogo wa TBA, Makumba Kimweri (kulia) na Richard Maliyaga (kushoto) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar! (Picha na Maktaba).

CHADEMA ni Mzigo kwa Taifa….NAPE


nape
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika kata 27, ambapo CCM imeshinda kata 23.
Kimesema siri ya kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.

Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema hayo na kuongeza kuwa matokeo hayo ni ushahidi kwamba CCM inakubalika zaidi na Watanzania walio wengi.


Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.


Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.

NAPE NAUYE

“CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini,” alisema.


Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na  Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo na Santillya (Mbeya).


Zingine ni Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro), Mrijo (Dodoma).

MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA WATU 9 TARIME AFARIKI DUNIA

Mtuhumiwa wa mauaji na unyang’anyi wilayani Tarime mkoani Mara, aliyekuwa akitumia majina matatu ya Charles  Range Kichune, Josephat Chacha, Charles Joseph Msongo (38) aliyekuwa akihojiwa na Polisi, amefariki katika Hospitali ya wilaya wakati akipatiwa matibabu.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Tarime/ Rorya
JAMBAZI

Justus Kamugisha, alisema mtuhumiwa huyo alifariki usiku wa kuamkia jana wakati akitibiwa ugonjwa wa pumu na kwamba baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa huo, alipelekwa hospitalini. Kamanda Kamugisha alisema mwili umehifadhiwa  kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Alisema kabla ya kufariki, mtuhumiwa  alikiri kuhusika katika mauaji ya watu tisa katika kata za Binagi, Turwa na Kitare katika Vijiji vya Mogabiri, Kenyamanyori, Nkende na Rebu.

 Kamanda huyo alisema Range Kichune alikamatwa Februari 6, mwaka huu  mkoani Tanga baada ya Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema kufuatilia mtandao wake na kuwa ilidaiwa baada ya mauaji ya hao alikodi pikipiki kutoka kijijini kwake Kenyamanyori  hadi Musoma na kuhifadhi bunduki SMG na risasi kadhaa kwa mshirika wake mkuu.

Alipokamatwa alimtaja Marwa Keryoba kuwa mshirika wake na kuwa alihifadhi silaha hiyo kwake na Marwa aliuawa Februa 7, mwaka huu Musoma wakati akirushiana risasi na polisi alipotakiwa kujisalimisha.

Thursday, February 6, 2014

PICHA YA MTOTO WA SHAKIRA KWA FANS WAKE .....


This is cute!!!! 

Shakira and her husband Gerald Pique welcomed a baby boy some weeks ago and they named him Milan Pique!

"SIDHANI KAMA USHIRIKINA UNAFAIDA KATIKA MUZIKI"...POMMY DIMPOZZ


Baada ya taarifa kuenea katika mitandao kuhusu Diamond anatumia mganga wa jadi katika kazi zake za muziki....
 
Leo kupitia Clouds Fm double XXL katika jiwe la wiki rafiki yake wa karibu 'Ommy Dimpoz' aliweza kusema kwa upande wake hadhani kama vitu vya ushirikina vinaleta faida katika upande wa muziki na wala hajawahi kujihusisha navyo maishani mwake.


Swali:Mara ya mwisho baada ya kukutana na Diamond Platinum hamjawahi kuzungumzia mambo ya ushirikina"Kusema kweli mara mwisho nakumbuka nilikutana naye na tukazungumzia kuhusu show yangu lakini mambo mengi hatujazungumza.Ommy Dimpoz alisema