This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, April 16, 2013

SPIKA WA BUNGE AWAVAA WABUNGE "WANAOTUMIA MATUSI" BUNGENI


Akiongea kwa uchungu , Spika wa Bunge bi Anne Makinda amewashambulia wabunge  leo asubuhi na kuwaambia suti zao walizovaa haziendani na matusi  yanatoka  katika vinywa vyao  ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana kwa  madai  kuwa mdomo  wake hauwezi kutamka matusi hayo.....
Makinda amesema matusi ndiyo yamekuwa yakitawala katika midomo ya wawakilishi hao na kuacha hoja inayojadiliwa hewani....
 
Spika wa bunge amekwenda mbali zaidi na kuwaambia wabunge hao kwamba hataangalia chama endapo mbunge atavunja kanuni za bunge kwa kuwa kanuni za bunge zinampa nafasi ya kuita polisi na kuja kumchukua mbunge huyo kwa hatua za kisheria.

Makinda  amesema ametumiwa sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake kuangalia bunge labda ajifungie chumbani.

"NIMEMSAMEHE DIAMOND INGAWA ALINISALITI KWA UWOYA....KWA SASA TUMEYAMALIZA".....HII NI KAULI YA PENNY


Katika muda ambao kila mmoja alikuwa amejaribu kuamini kuwa Diamond Platnumz ameamua kutulia na mpenzi mmoja, mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa, hivi karibuni  staa huyo ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu Irene Uwoya.....
 



Magazeti ya udaku nchini yaliandika habari hiyo ikiwa na picha inazowaoenesha mastaa hao wakichukua chumba kwenye hoteli ambako  walienda kufanya yao.
DIAMOND3
Kufuatia tetesi hizo, mwandishi wetu amezungumza na mpenzi wa sasa wa Diamond, Penny ambaye amesema kwa ufupi kuwa wameshayazungumza na Diamond na wako vizuri kwa sasa lakini akasisitiza kuwa asingependa kuliongelea zaidi suala hilo.

Katia hatua nyingine, Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa na uhusiano na Diamond amekanusha  taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la udaku kuwa amemcheka Irene kwa kunaswa kwenye himaya ya Diamond.
JOKATE
“Mimi hivyo vitu havinihusu na wanapenda kupata quotes zangu pasipo hitajika. I don’t know why? I don’t why wanatafuta story. That’s their life kiukweli with whatever they choose to do, more power to them,” amesema Jokate.

BOB JUNIOR AINGIZWA MKENGE....LAWAMA ZATUPWA TIGO


Imebainika kuwa kuna mtu aliyetengeneza line mpya kwa kutumia namba ya Bob Junior aliye barani Ulaya kwa sasa na kutaka kuwatapeli watu wake wa karibu kuwa yupo hoi na anahitaji msaada haraka.



Taarifa hiyo imetolewa na baba yake mdogo, Guru Ramadhan ambaye ni mmiliki wa G Records. Kupitia Facebook, Guru aka G Lover ameandika:

“Hii sijaipenda kabisa ni too much sasa..eti mtu yupo Europe na simu yake inaita bongo ukipiga duh kumbe mtu katengeneza line mpya na kutumia namba ya Bob Junior na pia jamaa anayetumia hiyo line ya simu eti anaomba msaada kwa watu kuwa Bob Junior anaumwa sana Ulaya anahitaji msaada wako ili arudi Bongo.

Hivi nini maana ya kusajili namba?…makampuni ya simu ya Bongo mjipange sanaaa…hili limemkuta msanii Bob Junior siku chache hizi, mpaka imeripotiwa polisi eti ndio wamejidai kui block number…t.g. mmeniboaje?..so guyz mnaosafiri muwe makini sana mkisafiri maana mnaweza kukuta madeni kibao mkafa na presha bure…wizi mtupu…I hate dat.”

CHEKA NA KATUNI ZA GPL


VIGOGO WIZARA YA ARDHI KORTINI KWA UBADHIRIFU

Watuhumiwa  hao wakiwa  mahakamani.
 Simoni Lazaro (kushoto) akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Gerald Mango.
MAOFISA watatu waandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi  leo wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za ufujaji wa pesa za serikali zaidi ya milioni 200.…
Watuhumiwa  hao wakiwa  mahakamani.
 Simoni Lazaro (kushoto) akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Gerald Mango.
MAOFISA watatu waandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi  leo wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za ufujaji wa pesa za serikali zaidi ya milioni 200.
Charles Kijuba akikwepa kamera mahakamani.
Watuhumiwa hao ni   Simon Lazaro ambaye alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa  Mipango na Sera, Gerald Mango,  Mkuu wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi , na  Charles Kijuba, Kaimu Mhasibu Mkuu.
Watuhumiwa hao wamekana mashitaka na mahakama hiyo imesema kuwa dhamana iko wazi .

SIMU NUSURA IWATOE ROHO

Wakikunjana huku Kila mmoja akidai simu ni yake
Hapa wakivutana kuelekea kule walikoiba simu
Vijana wawili walikutwa wakibishana baada ya kushutumiana kuzulumiana simu ambayo waliiba kwa mmpita njia mmoja maeneo ya Bamaga jijini Dar Es Salaam.

MHESHIMIWA AUMBUKA!

Bumbuwazi: Meneja Everson Makowa-Mwale (49), akiwa ameduwaa baada ya kunaswa akijivinjari na mke wa mfanyakazi wake.
NI aibu kubwa kuliko maelezo! Meneja wa kampuni ya kusafirisha mizigo ya Malawi Cargo, tawi la mkoani hapa, Everson Makowa-Mwale (49), raia wa nchi jirani ya Malawi amenaswa chumbani na mke wa mfanyakazi wake (jina tunalo).
Tukio hilo lililojaa fedheha lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya saa 11:25 jioni baada ya askari wa jeshi la polisi, ndugu na jamaa kufika eneo la hoteli moja maarufu jijini hapa (jina limehifadhiwa) na kumkuta chumbani akiwa mtupu akijiandaa kufanya ngono na mke huyo wa mtu.
Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo, kabla ya kuumbuka, alikuwa ameandaa mazingira yote kwa ajili ya kuvunja amri ya sita na mke huyo wa mfanyakazi wake.
Mtego wa kumnasa ulifanikiwa baada ya mtuhumiwa kutinga hotelini hapo akiwa na gari la kampuni aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 821 ASY na kunyooka moja kwa moja chumbani alikokuwa akisubiriwa na mwanamke huyo.
WASIFU WA MENEJA
Habari za uhakika zilieleza kuwa bosi huyo ni mbunge mstaafu aliyewahi kuwa Mheshimiwa wa Jimbo la Nkotakota South East nchini Malawi kwa kipindi cha miaka kadhaa.
Jamaa huyo aliangushwa na Agness Chatipwa Mandebvu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2009 nchini humo ndipo akatinga jijini hapa na kupata kazi ya umeneja wa kampuni hiyo ya usafirishaji.
MADAI MAZITO
Ilidaiwa kuwa meneja huyo ndiyo mchezo wake kwa sababu amekuwa akiwafanyia hivyo mabinti wanaofika ofisini kwake kwa ajili ya kuomba kazi ambapo huwakubalia kuwapa kazi endapo watakubali kushiriki naye dhambi ya uzinzi.
Uchunguzi ndani ya kampuni hiyo ulidaka madai kuwa tangu awe meneja, mabinti zaidi ya watano waliacha au kufukuzwa kazi walipokataa kufanya naye ngono.
Ilidaiwa kuwa wanaokubaliana na hali hiyo kutokana na ugumu wa maisha humkubalia na kupandishwa vyeo kiholela.
Sakata la tabia hiyo chafu kwa raia wa Kitanzania, lilifikia kikomo baada ya mfanyakazi mmoja (jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani wa meneja huyo kusimamishwa kazi kwa madai kuwa alichelewa kuripoti kazini.
MCHEZO WA NIPE NIKUPE
Mfanyakazi huyo ambaye alikuwa akiishi na mkewe nyumbani kwa bosi wake, alisimamishwa kazi ambapo bosi huyo alitumia mwanya huo kuanza kumchombeza mke wa jamaa huyo kwa kumwambia amkubalie ili amrudishe mumewe kazini.
Baada ya kupata usumbufu huo kwa kipindi kirefu ndipo jamaa huyo pamoja na wafanyakazi wenzake ambao walikuwa hawaipendi tabia ya bosi wao wakaandaa mtego uliomnasa kama panya bila kujinasua na kuishia mikononi mwa polisi.
WAFANYAKAZI
Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo ambao majina yake hawakutaka yaandikwe gazetini, walisema tabia ya bosi wao imekithiri na kwamba amekuwa akitumia wadhifa wake kuwalaghai watoto wa kike ili kufanya nao mapenzi.
Wafanyakazi hao walidai ni bora Idara ya Uhamiaji mkoani hapa iingilie kati suala hilo ili kuwanusuru Watanzania dhidi ya watumishi wa kigeni wanaokuwa na tabia zinazolenga kuwaondolea utu wao.
TURUDI KWENYE TUKIO
Baada ya kufumaniwa akiwa mtupu kutokana na mke wa mtu huyo kutoa ishara kwa walioweka mtego, aliomba radhi kwa mume wa mwanamke huyo ambaye ni mwajiriwa wa kampuni anayefanya kazi ya kutengeneza bustani.
Hata hivyo, msamaha wake ulikataliwa na soo likatinga polisi na sasa anasubiriwa kupelekwa mbele ya mkono wa sheria...