KUFUATIA kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya
kulevya nje ya nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga
polisi Julai 29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Idd Azzan alifika katika Kituo Kikuu cha
Polisi Posta jijini Dar na kukutana na Kamanda wa Kanda Maalumu,
Kamishna, Suleiman Kova.
“Kikubwa Azzan amemwambia Kova kwamba anataka jeshi la polisi limchunguze na kisha liwaambie wananchi kama yeye…
Na Mwandishi Wetu
KUFUATIA kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya
kulevya nje ya nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga
polisi Julai 29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Idd Azzan alifika katika Kituo Kikuu cha
Polisi Posta jijini Dar na kukutana na Kamanda wa Kanda Maalumu,
Kamishna, Suleiman Kova.
“Kikubwa Azzan amemwambia Kova kwamba
anataka jeshi la polisi limchunguze na kisha liwaambie wananchi kama
yeye anahusika na biashara hiyo au la,” kimesema chanzo chetu.
Baada
ya kupata habari hizo, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Azzan ambaye
alikiri kufika polisi na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan.
“Kila kinapofika kipindi kama hiki huwa kuna vuguvugu la uchaguzi,
hivyo maneno kama haya husemwa ili kuharibiana sifa, nimewataka polisi
wanichunguze na watakachokipata watoe taarifa kwa wananchi,” alisema.
Hivi karibuni Mbunge huyo alitajwa katika habari zilizosambazwa
mtandaoni kwamba anahusika na biashara hiyo baada ya mfungwa mmoja wa
gereza moja nchini Hong Kong kumtaja kwamba ndiye anayewatuma vijana nje
ya nchi kupeleka madawa ya kulevya.
Hata hivyo, Mbunge huyo
amekanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa hausiki kwa njia moja ama
nyingine na kutaka mfungwa huyo atajwe jina lake kamili, namba yake ya
ufungwa na hata ndugu zake waliopo hapa nchini ili ukweli ujulikane.
Barua zilizosambazwa mtandaoni ambapo jina la Mhe. Idd Azzan lilitajwa kuhusika na dawa za kulevya: