This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Sunday, July 7, 2013
LOWASSA APONGEZWA NA BAKWATA KWA KUVISHWA JOHO MAALUMU.....MILIONI 590 ZACHANGISHWA KATIKA HARAMBEE
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akipongezwa na kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawi kwa kumvika joho la kilemba baada ya kufanikisha harambee kwa ajili ya Kituo cha Redio Ikra kinachomilikiwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza.
Anayeshuhudia ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Salum Hassan Fereji.
Katika harambee hiyo zaidi ya sh. mil. 590 zilipatikana na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. mil 500.










MWANACHUO WA MWAKA WA KWANZA ALAANI KITENDO CHA KUPIGWA "EXILE" NA MADENTI WENZIE
Hali imekuwa ni tofauti kidogo kwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapa nchini ambaye yuko mwaka wa kwanza na anategemea kuingia mwaka wa pili.
Akiongea na mtandao huu kwa sharti la kutotajwa jina , mwanafunzi huyo amefunguka na kudai kuwa Exile imemuathiri sana kisaikolojia.Imemfanya aishi kama mtumwa huku taaluma yake ikiyumba kwa kasi.
Hili ni simulizi la mwanafunzi huyo:
"Maisha ya shule yana changamoto nyingi sana.Kwa mtu yeyote ambaye ni mcha mungu ni lazima itamuwia vigumu sana kukabiliana na hali hii.
"Nasema hivi kwa sababu ndani ya hosteli huwa tunaishi watu tofauti wenye malezi tofauti.Kasheshe ni kwetu sisi first year...
"Mazingira kwetu ni mageni na ndani ya hosteli tunaishi na mabraza wa miaka ya juu wenye wapenzi wao hapo hapo chuoni ambao huwaleta vyumbani na wakati mwngine hulala nao.
"Wanapokuja na wapenzi wao vyumbani ni lazima uwapishe wafanye mambo yao.Na ukiwapisha maana yake utoke kwa zaidi ya masaa matatu mpaka matano
"Ndani ya chumba changu tulikuwa tunaishi watatu, mmoja mwaka wa pili, mwingine wa tatu na mimi mwaka wa kwanza.Wote hao walikuwa na wapenzi wao hapo hapo chuoni.
"Siku zote za wikiendi walikuwa wamezigawana.Mmmoja ilikuwa ni jumamosi na mwingine jumapili.Yaani kwa kifupi ni kwamba sikuwa na uhuru wa kukaa chumbani siku za wikiendi na wakati mwingine hata siku za wiki.
"Nimeamua niwe muwazi maana hali hii imekuwa ni kero kwangu na imekuwa ikiniathiri sana kisaikilojia na kusababisha taaluma yangu iyumbe nikilinganisha na nilipokuwa naanza.
"Naomba nitoe ombi kwa wanafunzi wenzangu.Sote tuko vyuoni kutafuta maisha na zile hosteli tunazilipia kwa gharama sawa.Kwa nini umsumbue mwenzako wakati gesti zipo?..Yangu ni hayo tu"
LEO NDIO LE
BASI LA SUMMRY LAUA WATU 9 NA KUJERUHI 53
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa jina la Ntungu
Saturday, July 6, 2013
TEMEKE YALIZWA NYUMBANI MABAO 5-2 MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS
| Timu za Airtel Rising Stars zikiingia kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam tayari kwa ufunguzi rasmi wa ARS ngazi ya Taifa jana Jumanne Julai 2, 2013.. |
Timu ya Morogoro wavulana leo Jumatano Julai 3, imeifunga timu ya Temeke 5-2 katika fainali za Taifza za Airtel Rising Stars
zinazoendelea kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Morogoro waliutawala mchezo na kufanikiwa kupata magoli kupitia kwa mshambuliaji wa machachali Optatus Lupekenya ambaye alifunga magoli matatu peke yake yaani ‘hat trick’ katika dakika za 27 67 na 87.
Magoli mengine ya Morogoro yalifungwa Salum Mohamed dakika ya 72 na Evance Noshan dakika ya 80 wakati magoli ya Temeke yalifungwa na Mohamed Simba dakika ya 10 na Rajab Jumanne dakika ya 83.
Katika mchezo uliochezwa mapema asubuhi timu ya Ilala wasichana ilifanya mauaji ya kutisha baada ya kuifunga bila huruma timu ya Ruvuma 9-0 katika mchezo wa upande mmoja wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars.
Mchezo huo ulionyesha wazi ya kuwa Ruvuka wanatakiwa
kufanya kazi ya ziada ili kuinua kiwango chao cha soka.
Ilala walifunga magoli yao kupitia kwa Amina Ally (dakika ya 3, 28 na 51), Donisia Daniel (dakika ya 20 na 45), Zuwena Aziz (dakika ya 23 na 35), Madeline Sylvester (dakika ya 8) na Fatuma Bahau (dakika ya 12).
Katika mchezo uliochezwa Jumanne jioni katika uwanja huo huo, timu ya kombaini ya Mwanza (wavulana) ilitoa onyo kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo baada ya kuifunga timu ngumu ya Ilala 3-1.
Huo ulikuwa mchezo rasmi wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars Taifa 2013 ambapo mgeni rasmi Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Kassim Majaliwa aliwataka vijana kuonyesha vipaji vyao.
“Katika dunia ya leo mpira wa miguu ni moja ya vyanzo vya ajira vya kutumainiwa kwa vijana”, alisema Majaliwa na kuwahamasisha vijana hao kucheza kwa kujituma na kutumia mashindano ya Airtel Rising Stars kama fursa ya kuonyesha umahiri wao wa kusakata kabumbu. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendeleza kusaidia programu hii ya vijana.
Mchezo kati ya Mwanza na Ilala ulikuwa wa kuvutia huku timu zote zikionyesha kiwango kizuri kwa kugongeana pasi za uhakika. Mwanza walifanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya saba kupitia kwa Nassor ambaye aliwapita walinzi wa Ilala na kutia mpira wavuni. Goli hilo lilidumu hadi mapumziko.
Ilala walianza kipindi cha pili kwa nguvu na kupata goli la
kusawazisha dakika ya 50 kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Omary Hassan baada ya walinzi wa Mwanza kufanya makosa nje kidogo ya eneo la hatari. Mshambuliaji Athanas Adam aliifungia Mwanza goli la pili dakika ya 69 na Kelvin Ntalale kugongelea msumari wa mwisho dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika.

















