Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando, akiongea na makatibu
wakuu wa mikoa na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina
elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
TFF jana.
Katibu mkuu mkoa wa kisoka wa Temeke, Mbarouk Mohammed (kulia)
akichukuwa karatasi wakati wa kupanga makundi na ratiba ya michuano ya
Taifa ya Airtel Rising Stars iliyopangwa kuanza mwezi Julai, 2013
uwanja…
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando, akiongea na makatibu
wakuu wa mikoa na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina
elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
TFF jana.
Katibu
mkuu mkoa wa kisoka wa Temeke, Mbarouk Mohammed (kulia) akichukuwa
karatasi wakati wa kupanga makundi na ratiba ya michuano ya Taifa ya
Airtel Rising Stars iliyopangwa kuanza mwezi Julai, 2013 uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Kushoto ni katibu wa DRFA,
Msafiri Kondo.
Baadhi
ya makatibu wakuu wa mikoa inayoshiriki michuano ya soka ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars wakifuatilia kwa makini
kanuni za mashindano hayo wakati wa semina elekezi iliyofanyika TFF
jana.
Katibu
mkuu wa DRFA Msafiri Kondo akiongea na makatibu wakuu wa mikoa na
waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya Airtel
Rising Stars iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TFF jana.
FAINALI za Taifa za michuano ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 za Airtel Rising Stars zimepangwa kuanza
kutimua vumbi uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Julai
2 kwa mabingwa watetezi Temeke wavulana kupambana na Kinondoni.
Akizungumza
wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars 2013 iliyofanyika Juni
mosi katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
(TFF), Ofisa Maendeleo wa shirikisho hilo Bw. Salum Madadi alisema ARS
ngazi ya mikoa imepangwa kuanza Juni 15 hadi 29.
Mikoa inayoshiriki
Airtel Rising Stars mwaka huu kwa upande wa wavulana ni mikoa ya kisoka
ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Mikoa mingine ni Morogoro Mwanza na
Mbeya ambapo kila mkoa unatakiwa kushirikisha timu sita. Usajili wa timu
umepangwa kuanza rasmi kesho Juni 2 na kumalizika Juni 11.
Kwa
upande wa timu za wasichana, alisema, mikoa itakayoshiriki ni Tanga,
Kigoma na Ruvuma na mikoa yote inayoshiriki Airtel Rising Stars mwaka
huu iliwakilishwa kwenye semina elekezi na makatibu wakuu ambao walipata
fursa ya kupitia kanuni na taratibu za michuano hiyo ya vijana.
Upangaji
wa ratiba uliofanyika leo ni wa fainali za taifa pekee kwa kuwa
mashindano ya ngazi ya mkoa yataendeshwa na uongozi wa mkoa husika ikiwa
ni pamoja na kupanga ratiba yake.
Kwa upande wa wasichana timu
zitakazofungua dimba katika fainali za taifa ni Ilala na Kinondoni. Kwa
ujumla timu 12 zitashiriki fainali za Taifa, sita za wasichana na sita
za wavulana.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Meneja
wa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando alitoa rai kwa makatibu
wakuu wa mikoa kuwa makini wakati wa usajili ili kupata vijana wenye
vipaji ambao wataiwakilisha vema Tanzania kwenye michuanoa ya kimataifa
ya Airtel Rising Stars. Vile vile Tanzania itawakilishwa kwenye klini
itakayofanyika chini ya makocha wa Manchester United.
Alisisitiza
alisema nia thabiti ya Airtel Tanzania kuendelea kusaidia mashindano ya
vijana kwa nia ya kuendeleza soka nchini na kuishukuru TFF na wizara
inayohusika na michezo kwa kuyaunga mkono mashindano haya.
Naye mgeni
rasmi katika semina hiyo , Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Msafiri Kondo aliwaomba wadhamini
kuendelea kudhamini michuano hiyo ili vijana wa kike na kiume waweze
kufikia malengo yao katika soka.