
Mshindi wa Miss Utalii Vipaji kutoka Mkoa wa Manyara wa kati kati akiwa na washindi wenzake wawili waliofika mpaka Tatu bora
HATIMAYE Mshiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13
kupitia Mkoa wa Manyara ameshinda tuzo ya vipaji 2012/13 na kuibwaga
mikoa mingine 29 ya Tanzania Bara na Zanzibar. Mrembo Miss Mary (19)
alionesha kipaji cha hali ya juu katika ushindani ambao ulikuwa mkubwa
hasa kutoka kwa warembo wa mikoa ya Lindi, Kagera, Dodoma, Zanzibar na
Katavi.
Hata hivyo, mchuano ulikuwa mkali zaidi kati ya Miss Utalii, Lindi
Manyara na Kagera ambao walionesha Umahili mkubwa wa kucheza ngoma za
asili na kupelekea kuingia katika hatua ya Tatu Bora. Katika Hatua hiyo
ya Tatu Bora washiriki hao walicheza wimbo mmoja ujulikanao kwa jina la
katope kutoka kundi la ngoma za asili la kibiriti ambao ni mchanganyiko
wa ngoma mbalimbali wa makabila ya ngoma za kusini.

Mshindi wa Tuzo la Vipaji akiwa anafuraha Muda Mchache baada ya kutangazwa kuwa yeye ndiye mshindi.
Hali hiyo iliwafanya wapenzi wa fani ya urembo waliofurika katika ukumbi
wa Dar Live Mbagala kuto kuamini kwamba wanao cheza jukwaani ni Mabinti
wa Kizazi kipya ambao kwa Hali ya kawaida ya sasa ni nadra sana
kumuona sister Duu tena Mrembo kucheza ngoma za asili kwa ufasaha na
umahili mkubwa.
Wapenzi hao walijikuta wakiacha viti vyao na kuanza kushangilia kwa
nguvu mwanzo hadi mwisho huku wakiwapongeza waandaaji wa shindano la
Miss Utalii Tanzania kuwa ni Hazina kubwa ya utamaduni wa Mtanzania na
Wengine wakithubutu kusema Miss Utalii ni mtambo wa kurekebisha tabia
kwa kuweza kuwabadirisha fikra za mabinti hao wa kizazi kupya mashindano
hayo kwa ya kuwa kucheza ngoma za asili ni ushamba hadi kuwafanya kuwa
wacheza ngoma mahili tena hadhalani bila ya Aibu na kwa kujivunia
utamaduni na Ngoma za Asili Tanzania.
Wapenzi hao waliohudhuria katika shindano hilo wakisika kwa nyakati
tofauti kuitaka na kuishauli Serikali na mamlaka za utalii kudhamini
shindano la Miss Utalii Tanzania kwa Faida ya Jamii na Taifa kwani
shindano hili limedhihilisha uwezo mkubwa wa sio tuuu kuhifadhi
utamaduni wa mtanzania bali pia kuhamasisha na kutangaza utalii wa
tanzania kitaifa na kimataifa.
“Shindano hili ni zuri na ni lakipekee lakini tatizo inaonekana
waandaaji hawajapata wadhamini wa uhakika, kwanini Serikali isiwasaidie
hawa,” alisema Jafary Shaibu mpenzi ma mashindano ya urembo.
Akizungumza katika Shindano hilo ambalo Mwanamuziki wa Kimataifa Che
Mundugwao alikonga nyoyo za watu kwa Muziki wake wenye asili ya
kitanzania, Mgeni Rasmi, Maabad Suleiman Hoja Mustahiki Meya wa Manispaa
ya Temeke aliwapongeza sana washiriki na washindi lakini alitoa
shukurani za pekee kwa waandaaji wa mashindano haya kwa kuipa manispaa
na wilaya ya Temeke Heshima kubwa ya kuwa wenyeji wa Tukio hili la
kitaifa lenye hadhi ya kimataifa.
Kiongozi huyo alisema Manispaa ya Temeke na Wilaya inayouwezo wa kuwa
wenyeji wa matukio makubwa ya kimataifa na kitaifa kama la Miss Utalii
Tanzania 2012/13, hivyo kutoa fursa ya pekee kwa Temeke kujitangaza
kiutalii, kitamaduni na kiuwekezaji ndani na nje ya Nchi. Pia aliahidi
kuwa Manispaa ya Temeke kuendelea kuunga mkono kwa hali na mali ili
kufanikisha fainali hizo ambazo zitafikia kilele katika ukumbi wa Dar
Live Mbagala Dar es Salaam.
Mshindi wa Tuzo hiyo ya Vipaji ambaye alishangiliwa na washiriki wote
baada ya kutangazwa kama mshindi, alizawadiwa udhamini wa kusoma kozi
ya Kiwango cha Diploma katika chuo chochote nchini.
Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na:
Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola
Kwanza, VAM General Suppries Limited,Global Publishers, TANAPA,
Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey
Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la
Taifa (BASATA )