This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Monday, March 4, 2013
AZAM YAPONGEZWA KUITOA TANZANIA KIMASOMASO MICHUANO YA AFRIKA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa timu ya Azam ya
Tanzania Bara kwa kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la
Shirikisho iliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Ushindi
wa jumla ya mabao 8-1 ambao Azam imeupata dhidi ya Al Nasir Juba ya
Sudan Kusini si fahari kwa timu hiyo tu, bali Tanzania kwa ujumla, na
unaonyesha jinsi klabu hiyo ilivyojipanga kiushindani katika michuano
hiyo ya Afrika.
Hata
hivyo, ni vizuri Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, benchi la ufundi na
wachezaji wa timu hiyo wakautazama ushindi huo kama changamoto kwao
kuhakikisha wanajipanga vizuri zaidi kwa raundi inayofuata.
Timu
ya Azam inayofundishwa na Mwingereza John Stewart Hall ilishinda
nyumbani mechi ya kwanza mabao 3-1, na jana kuibuka na ushindi wa mabao
5-0 ugenini jijini Juba.
Kwa
kufanikiwa kuing’oa Al Nasir Juba, Azam sasa watacheza raundi ya kwanza
(raundi ya 16 bora) ya michuano dhidi ya Barrack Y.C.II ya Liberia
ambayo katika raundi ya awali iliitoa Johansens ya Sierra Leone. Barrack
ilishinda bao 1-0 nyumbani katika mechi ya kwanza na kulazimisha suluhu
katika mechi ya marudiano jijini Freetown.
Azam
itaanzia mechi hiyo ugenini kati ya Machi 15,16 na 17 mwaka huu wakati
mechi ya marudiano itachezwa Tanzania kati ya Aprili 5,6 na 7 mwaka huu.
PICHA ZA PAMBANO NGUMI LA JAPHET KASEBA DHIDI YA MANENI OSWARD 'MTAMBO WA GONGO'
Bondia Japhert Kaseba akinyooshwa mkono juu na refarii Antoni Ruta baada ya kuibuka mshindi kwa kumgalagaza Maneno Osward picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Sunday, March 3, 2013
KITENDO CHA IRENE UWOYA KUYAANIKA " MAKALIO YAKE" NI SAWA NA KUWATUSI MASHABIKI WAKE
Huu ni upotofu mkubwa wa maadili unaoendekezwa na hawa wanaojiita MASTAA.....
Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa Uwoya ni mzazi wa mtoto mmoja ambaye walizaa na Ndikumana na hatimaya wakaachana baada ya kushindana kitabia...

Swali la kujiuliza ni kwamba, Anajisikiaje kuyaanika matako yake kwa mtoto wake wa kumzaa???...Atajenga msingi upi kwa mtoto wake akikua????.....
Achilia mbali mtoto wake, vipi juu ya wazazi wake, wadogo zake, shemeji zake na ndugu na jamaa???...
Irene jitambue.....umri umeenda sasa...unayoyafanya hayaendani na umri wako.....
Umaarufu hauji kwa kukaa uchi.....Wapo akina Lady jaydee, Monalisa....Ni wasanii maarufu pengine kuzidi hata wewe....kwa nini usiige kutoka kwao
Kitendo hiki ni sawa na kuwatusi watazamaji wa filamu zako

HII NDO TUME YA WATU 15 ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda jana Jumamosi, Machi 2, 2013 amezindua Tume maalum
aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na kuwataka wajumbe wa Tume hiyo
watafute kiini cha mserereko wa kushuka kwa ufaulu kuanzia mwaka 2010
hadi 2012.
Waziri Mkuu
amezungumza na wajumbe wa Tume hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.
Amesema
kwa mujibu wa hadidu za rejea, wajumbe wa tume hiyo watatakiwa
kuangalia ni sababu zipi zimechangia kuwepo kwa matokeo hayo mabaya,
mserereko wa kushuka umekuwa ukiongezeka kwa sababu gani, usimamizi
katika Halmashauri ukoje, ukaguzi wa elimu na uhamishiwaji wa sekta ya
elimu kwenye Wizara ya TAMISEMi umechangiaje kushuka kwa kiwango cha
ufaulu.
Vilevile,
watatakiwa kuangalia mitaala na mihutasari ikoje, kuangalia uwiano
uliopo kwenye mitihani inayotungwa ikiwa ni pamoja na uhakiki wa
mitihani hiyo; kuangalia mazingira ya kufundishia, mfumo wa upimaji,
usimamizi na uendeshaji, na kutokuwepo kwa chakula shuleni kunachangiaje
kushuka kwa utendaji mbaya wa wanafunzi katika masomo yao.
Tume hiyo yenye
wajumbe 15, imepewa muda wa wiki sita kuanzia Machi mosi iwe
imekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha taarifa yao kwa Waziri Mkuu.
Tume itaongozwa na Prof. Sifuni Mchome wa Tume ya Vyuo Vikuu, na Makamu wake atakuwa Bi. Bernadetha Mushashu (Mbunge wa Viti Maalum – Kagera).
Wajumbe ni Bw. James Mbatia (Mbunge wa kuteuliwa), Bw. Abdul J. Marombwa (Mbunge wa Kibiti), Prof. Mwajabu Possi (Chuo Kikuu – UDSM), Bibi Honoratha Chitanda (CWT), Bibi Daina Matemu (TAHOSSA) na Bw. Mahmoud Mringo (TAMONGSCO).
Wangine ni Bw. Rakhesh Rajani (TWAWEZA), Bw. Peter Maduki (CSSC), Mwl. Nurdin Mohamed (BAKWATA), Bw. Suleiman Hemed Khamis (Baraza la Wawakilishi, Zanzibar), Bw. Abdalla Hemed Mohamed (Chuo Kikuu – SUZA), Bw. Mabrouk Jabu Makame (Baraza la Elimu Zanzibar na Bw. Kizito Lawa (Taasisi ya Kukuza Mitaala).
wavuti.com
ZAIDI YA ABIRIA 50 WA BSI LA SUMRY LITOKALO
SUMBAWANGA KUJA MBEYA LIMEPATA AJALI MAENEO YA SONGWE MPAKANI MWA WILAYA
YA MBOZI CHANZO CHA AJALI HIYO NI KUWA ROLI LA MIZIGO LA KAMPUNI YA
KANJILAJI LILIKUWA LINAIPITA GARI NYINGINE HIVYO KUHAMIA UPANDE WA BASI
LA SUMRY NA NDIPO DEREVA WA SUMRY AKAONA KUA WATAGONGANA USO KWA USO
AKAAMUA KULIINGIZA SHAMBANI ILI KUJIOKOA KATIKA AJALbadhi ya majeruhi wakikibizwa hospital